Naamini wewe sio mgeni hapa Tz,unaelewa vyema mbinu zao za kutest zali na kupigia debe upupu kabla ya kutuingiza kwenye majanga,Kila janga lilikuja baada ya kupigiwa debe na kupambwa matumaini kibao, kauli yake na Zito kabwe kuhusu TANESCO ikafuatiwa na ziala zake za kutafuta wawekezaji kwenye barozi za kigeni na posti zake kwenye mitandao ongeza na baadhi ya watu walioteuliwa kuwa na mgonhano wa kimaslahi na makampuni yaliyo tuumiza huko nyuma,jumlisha na kauli ya Muhongo bungeni hivi karibuni utapata majibu wapi tunaelekea. Haina Shaka subiri utashuhudia mwenyewe.
Bado unachanganya mambo...
Kwenye sekta ya umeme kuna maeneo makuu matatu... Generation, Transmission, na Distribution. Kwavile maeneo yote hayo yanahitaji nguvu ya kutosha in terms of finance and human resources, serikali ikaonelea maeneo mengine, hususani eneo la Generation, sekta binafsi ihusishwe lakini Transmission SHOULD STRICTLY remain in the hands of TANESCO!!
Tafuta na soma what's so-called
Power System Master Plan!! Hapa nitakuwekea sehemu tu ya
Updated version ya 2020 kipindi cha huyo huyo Magufuli ambae unadai baada ya yeye kufariki, watu wanataka kuleta yao.
Ningekuwa 2008 PSMP Comprehensive Version lakini utasema hiyo ya 2008 "Ndo walewale"
Sehemu ya Power System Master Plan 2020 Update inasema:-
Huo ni mpango wa Wizara ya Nishati chini ya huyo huyo The Late Magufuli?! Na hapa nasisitiza huko sio kubinafsisha TANESCO kama wengine wanavyodai!
Na kaa ukijua, dunia ya leo kuna kitu kinaitwa Power Generation Mix! Hili lifahamike kwa sababu suala la Nyerere Dam wengine linawafanya wadhani tatizo la umeme ndo BYE BYE for good, huku wakisahau lile ni bwawa tu, na ufanisi wake unategemea mvua!
Tukipigwa ukame wa miaka 3 mfululizo hapa , tena kwenye maeneo tu yanayo-supply maji kwenye bwawa la Nyerere, hapo lazima watu watafutane. Na ndo hapo wengine wataanza kusingizia "kwavile Magufuli amefariki, watu wameanza kuziba maji" kumbe it's just science!!
Hata hivi sasa, ingawaje credit anapewa Magufuli, hii nafuu inatokana na gas ya Mtwara kupitia bomba la Kinyerezi!
Zaidi ya 55% ya umeme uliopo kwenye grid ya taofa hivi sasa unatokana na Gesi ya Mtwara na Songosongo!! Sasa jiulize kama sio hiyo gas hali ingekuwaje hata kama tayari kuna umeme unaozalishwa kwa maji!
Ni kutokana na hilo, ndo maana suala la Power Generation Mix haliepukiki! Kama serikali inajenga Bwawa la Nyerere, hiyo haiwezi kuwa sababu ya kutokuwa na vyanzo vingine vya umeme... ama vinavyomilikiwa na serikali au sekta binafsi!!