Kaburi la Hayati Magufuli: Wakati umetoa majibu na kuumbua watu

Kaburi la Hayati Magufuli: Wakati umetoa majibu na kuumbua watu

Kuna wale wapuuzi walosema eti kaburi lipo kwenye banda, niliwambia muwe wapole kuna mjengo una shushwa pale.

Sikutaka kuweka hapa picha nilitaka mzitafute wenyewe.

Sasa vipi hela ya serikali haijawauma? Rais jpm ana heshima zake duniani kote sema wajinga tu ndo wanapinga hadi leo.😏😏

Ujenzi unaendelea kwa nje kuna kitu kinatengenezwa sio kila mjinga mjinga anaingia hovyo. Itakuwa tiyari soon kabla ya kumaliza matanga mwakani.
 
245154501_909088446394865_5514189208103415052_n.jpg

Alikuwa dhalimu, tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika fullstop.
 
Asante kwa kumsitiri vyema shujaa wetu,ingawa alikuwa na mapungufu yake Ila Mimi wiki hii nimeanza kumuona alikuwa Ni shujaa, toka nipate tetesi eti tunatafuta wawekezaji waje tuizike TANESCO na wakati huohuo Nyerere Dam inaanza kutapika umeme mwakani kwa gharama zetu halafu waje watu kuvuna tu!
Nilikuwa natarajia kuanza kupika kwa jiko la umeme na tayari nimeshanunua na pasi na mengineyo kwa kujidai Kama alivyo tuahidi mwendazake kuwa atatupatia umeme kwa Bei nafuu tuachane na mkaa.
Halafu mnakuja na mbwembwe ati mnataka watu Kati madalali Kweli?
Nimem miss Sana huyo mzee alale kwa amani namuahidi tutapambana nao.
Hizo tetesi umesikia wapi?
 
Ndio kashakufa mkuu, hakuna haja ya kutumia gharama kubwa haisaidii chochote

Mimi nikindei hata baharini mnitupe, fresh tu
Mimi nataka wanipige moto then majivu wakatupe mtoni, haya mambo ya kufukiana na makaburi ni wastage of space tu, tamaduni zilizopitwa na wakati
 
kufanya uwekezaji kwa serikali sio vibaya,kwanza serikali kufanya biashara haiwezi kujitwisha huo mzigo ni vizuri sana,hebu imagine sasaivi teknolojia ya mawasiliano ilipofikia na uko nyuma ilivyokuwa ttcl ndio utaelewa
Hivi tutajiamini lini Kama taifa tunasomesha watu kwa ajili ya Nini? Hebu ona CHINA RAILWAY, CCECC,CCCC,CRBC, na mengine mengi Ni makampuni ya serikali ya China Leo wanatujengea Hadi Reli kwa Nini hatujiulizi tunakwama wapi Kama taifa ili tupige hatua? Lakini hata huko kwenye ubinafsi hatujafanikiwa bado nitajie hata kampuni moja tu ya kizalendo yenye uwezo wa kujenga hata km 50 tu za lami.
Tuna safari ndefu Sana maana hata ma professor wetu Akina Muhongo alitudanganya juzi tu hapa eti umeme wa maji umepitwa na wakati Tena wa Bei ghali ka,Kama Prof anaweza kusema hivyo tutarajie Nini katika hii nchi, watu toka asubuhi Hadi jioni wanatafuta namna ya kutupiga tumuamini Nani sasa ee. Tuchukue hatua hatujachelewa.
 
Asante kwa kumsitiri vyema shujaa wetu,ingawa alikuwa na mapungufu yake Ila Mimi wiki hii nimeanza kumuona alikuwa Ni shujaa, toka nipate tetesi eti tunatafuta wawekezaji waje tuizike TANESCO na wakati huohuo Nyerere Dam inaanza kutapika umeme mwakani kwa gharama zetu halafu waje watu kuvuna tu!
Nilikuwa natarajia kuanza kupika kwa jiko la umeme na tayari nimeshanunua na pasi na mengineyo kwa kujidai Kama alivyo tuahidi mwendazake kuwa atatupatia umeme kwa Bei nafuu tuachane na mkaa.
Halafu mnakuja na mbwembwe ati mnataka watu Kati madalali Kweli?
Nimem miss Sana huyo mzee alale kwa amani namuahidi tutapambana nao.
Kidogo kodogo mtamuelewa tu Magu.....
 
Mimi nataka wanipige moto then majivu wakatupe mtoni, haya mambo ya kufukiana na makaburi ni wastage of space tu, tamaduni zilizopitwa na wakati
Ni kweli mkuu, kwa wanaoishi Uyole,Mbeya watakuwa mashahidi mpaka sasa burial sites zilizofungwa ni kama 3, halafu ni maeneo makubwa si kidogo, kibaya zaidi eneo la nne nalo linaenda kujaa si muda mrefu!

Hayo ni matumizi mabaya ya ardhi, bora utaratibu wa cremation utiliwe mkazo hapa Bongo itasaidia
 
Back
Top Bottom