Pengo anajielewa hawezi fanya hivyo, Kama ni kuzungumza ataongelea kupatikana kwa suluhu[/Q
Nakubaliana na wewe.Kwanza yeye hawezi kutoka na kutolea msimamo kwa Wakatoliki wote bila idhini ya Maaskofu wenzie.Kwa kuwa UKUTA si issue ya kitaifa kama kuna ulazima wa Kanisa kutoa maoni au maelekezo yeyote kazi hiyo itafanywa na Baraza la Maaskofu kupitia Raisi wake au idara zake zinazohusiana na mambo ya Haki na Amani.
Kwa hiyo yawezekana akaongelea suala hilo lakini haiwezi kuwa kwa muktadha wa Wakatoliki wote.Wakatoliki wako CCM pia na vyama vingine na wengine hawana vyama kabisa ikiwemo yeye mwenyewe na viongozi wengine waandamizi wa Kanisa Katoliki.
Na ikitokea kweli akaongelea suala la UKUTA itakuwa kwa nafasi yake kama Mtanzania na kwa hali hiyo hatoweza ku-address Wakatoliki wote Tanzania au Jimbo la Kuu la Dar Es Salaam.