Kafulila: Anayetaka kuwekeza TANESCO na aje,Tanzania inajengeka kwa Kasi mno mwaka 2050 tutahitaji zaidi ya Megawatt 60K wakati leo tuna Megawatt 4K

Hujui unachoandika naona
 


Tanzania nchi ya ajabu sana. Kuna wawekeaji wamekuja kuanzia Songas na wengine. Wakija wanaombwa rushwa na hao hao wanasiasa halafu wanalalamika mikataba mibaya baada ya kupata 10%. Tukivunja mikataba ni madeni.

Kafukila atueleze serikali imelipa kiasi gani kwenye kesi za uwekezaji Tanesco kwa miaka 15 iliyopita?
 
Hujui unachoandika naona
Na hicho ndio unifanya kuwa bora kila kukicha sababu nafahamu kwamba sijui hivyo kujifunza kupembua na kutafuta ukweli wa kila jambo na sio kama wewe kulishwa kila unacholishwa na kukikubali kama kilivyo...
  • Hawa madalali unawaoamini kila wanachokwambia na kuwapa leeway kwamba watafutie mwarobaini shida zetu ndio walitaka kutuingia chaka na ADANI katika umeme na huyu akiwa dalali namba moja (one has to think labda alikuwa naive au amekula mlungula) na sababu hatuna uhakika ngoja tuangalie yenye uhakika
  • Je hawa watu wangempenda mwananchi wangempelekea mitungi ya gesi ambayo mwisho wa siku gharama ni Tshs mia tatu na ushee wakati ageweza kutumia umeme kwa gharama ya Tshs 100 /=?
Punguza kuwa cheerleader na kupembua hoja na unachoambiwa hata kama unalipwa sidhani kama malipo hayo yanazidi gharama ambayo utatumia maisha yako yote kwa kupikia iwapo tutaendelea na LPG badala ya Umeme at an affordable Cost....
 
Wewe hayo maswali peleka TANESCO
 
Kwa nini awekeze Tanesco? Hawezi kuwa na shirika lake likawa linauza umeme kwa Tanesco? Huyu jamaa anyone Tanesco inapona kutoka mikataba ya hovyo, kila siku anawaza kuirudisha Tanesco ilkotoka. Hovyo kabisa.

Muwekezaji, Atafute chanzo cha umeme kisha aiuzie Tanesco, alipwe kwa anachouza, sio capacity charges
 
Kwa akili ya CCM ya kugawa t-shirt na chumvi Kwa wapiga Kura itawezekana?
 
Ninamaana sekta binafsi.
Kwani umekatazwa ? Hata jana au Juzi au miaka kadhaa iliyopita haukukatazwa kuzalisha (Ndio kina Mobisol walivyokuwa wanafanya kwa kuuza Solar) Au Makamba alivyoingia Mikataba na wale mimi ninaowaita Matapeli ili wazalishe Solar na kuuzia Tanesco kwa bei mbaya, hakuna tofauti na kina Dowans, Symbion na watu kama hao... Ndio maana nilishasema na nitaendelea kusema yoyote anayeweza kuzalisha na azalishe ila Tanesco wanunue na kusambaza na wanunue iwapo tu cost itakuwa ni ndogo kuliko Tanesco anavyoweza kufanya mwenyewe...

 


Shida zaidi ni hao media wenyewe nchi ina energy plan, ambayo ni ya hovyo kwenye finance tu.

Yaani wana mipango ya projects za kuanza utekelezaji miaka mitano baadae na estimated costs, udhani kama wana inflation adjustments.

Worst katika hiyo mipango yao hakuna sehemu inayozungumzia industry structure to attain that goal.

Anachoongea Kafulila na strategic panning ya serikali ni vitu tofauti,

Mambo kama haya ni possible kwenye ‘banana republic’ kama Tanzania.
 
Tanzania haiwezi kufikia umeme huo unaotajwa, huo ni 20 times threshold ya SA, uliopo sasa haupo stable unakatikatika kila wakati. Kwanini hamsemi ukweli. Kwa culture hii ya kutekana mtapata wawekezaji wa ovyo labda watoke China, Vietnam na Turkey waliozoea mambo ya kutoheshimu haki za binadamu, na hao wawili wa mwanzo watawafanyisha kazi kama punda. Hawawajali ninyi waafrica.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…