ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Miradi ya Maendeleo inayostahili mikopo sio hiyo tuu aliyotaja Bali na mingine Mingi tuu kwenye sekta zote.
Mhe David Kafulila Mkurugenzi Mkuu wa Ubia nchi PPP amewatoa hofu Watanzania kuwa Serikali yao ya awamu sita ina nia na dhamira njema dhidi yao.
Kafulila akihojiwa Katika kipindi Cha amesema si kosa nchi kukopa kwaajili ya miradi ya maendeleo ila ni dhambi kukopa ili kugharamia mambo kama mishahara na mambo mengine yasiyo ya kimaendeleo yaani matumizi ya kawaida.
Kafulila ameenda mbali mpaka kuwakumbusha namna Ulaya ilivyojengwa kwa mikopo toka Marekani (MARSHALL PLAN ) baada ya Vita kuu ya Pili vya Dunia miaka ya 1948.
Hata hivyo Kafulila ameonesha si kweli kwamba Uchumi wa Tanzania unajengwa kwa Mikopo pekee ila ni Kwa sehemu tu,
Kafulila anasema, Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu tumekopa nje kiasi cha US$ 5 bilioni wakati Uchumi wetu katika kipindi hicho umekua kwa US$ 20 bilioni sawa na tofauti chanya ya US$ 15 bilioni.
Mkurugenzi Kafulila amemsifu zaidi Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoipokea nchi na kwa kasi hii ya Uchumi ambayo hakuna nchi yoyote Africa Mashariki na Kati kwa miaka mitatu imefikia kiasi na kiwango chake.
Sio tuu Ulaya Hadi China imejengwa Kwa pesa za mikopo ,kukopa kunakupa fursa ya kufanya Kwa haraka na uzalishaji kuanza fasta huku unalipa mdogo mdogo kutokana na fursa zilizoletwa na miradi hiyo ya mikopo.
Na ndio maana Nchi zote Duniani zinapambana kutafuta mikopo.Kwa Nchi kubwa kama hii ambayo hakuna Barabara za kutosha,reli,maji,umeme nk bila kupata pesa za kuifungua ni wazi watu watazliwa maskini na kurithisha vizazi vyao ufukara.
Nashangaa Kwa nini Serikali inasita sita kukopa kisa ujamaa mentality.Nyerere alikopa Kwa Ajili ya vita Uganda,alikopa Kwa Ajili ya reli ya Tazara nk nk.