Kafulila: Ifikapo mwaka 2050 kipato cha kila Mtanzania kitakuwa kati ya TZS 12M na 20M pato la Taifa litafikia $700bn mara 9 zaidi ya leo

Sawa!
Je. (Net Present Value) , Thamani ya fedha hiyo ya wakati huo ujao itakuwa sawa na thamani ya shilingi ngapi kwa sasa?
Actual jibu huwezi pata ila projection utapata.

Pia Kwa kuwa Nguvu ya Uchumi wetu inaongezeka automatically Dolla itakuwa ndogo zaidi.

Mwisho hakuna sababu ya kutumia Dola kupima thamani ya pesa yetu Bali pesa yetu itakuwa na uwezo wa kununua vitu kiasi gani? Purchasing power parity ndio jambo la msingi.
 
Nabubujikwa na machozi ya furaha, mitano Tena kwa Mama!
 
Kuna kitu kinaitwa inflation, Mwaka 2050 hii elf 10 nyekundu itakuwa ya kununulia pipi

Mwaka 2000 nauli ya daladala ilikuwa shilingi 10, chipsi yai shilingi 100

Leo hii 2024 shilingi 100 utanunulia pipi mbili tu
Kwanza swala la mfumuko wa bei inategemea na sera za Nchi husika na usikariri.

Kwa miaka yote mfumuko wa bei wa Tanzania ni chini ya 5% ,hivyo basi hata baada ya miaka hiyo 25 Bado sera yetu itakuwa pegged not more than 6% kitu ambacho ni very affordable.

Mwisho inflation ndio stimulus ya bei na production so usikariri.
 
Hata kama kipato cha mtanzania kitakuwa kati ya milioni 12-20 ifikapo mwaka 2050, bado kinaweza kuonekana kuwa ni umaskini kwa wakati huo. Hii ni kwa sababu ya kupungua kwa dhamani ya pesa kutokana na mfumuko wa bei na gharama za maisha kupanda na mabadiliko mengine ya kiuchumi.
 
Mnatufanya mafala sana mln 12 kwa mwaka mbona ndogo sana tena 2050
 
Hapa anazungumziwa yule Mtanzania wa chini kabisa lazima uelewe ambae Leo kwa siku hata buku hakamati
 
Je, bidhaa na huduma zitabaki kuwa na bei ya leo?!!
 
Je, bidhaa na huduma zitabaki kuwa na bei ya leo?!!
Hapana lakini Kwakuwa mnyumbuliko wa Pato la kila mtu mmoja mmoja ni mkubwa na kuimarika kwa Shilingi ya Tanzania hiyo ni pesa nyingi sana tuzidishe tu kuomba uhai yajayo yanafurahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…