Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
Wasalaam wana wa Mungu.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Zacharia Kafulila, amekosoa vikali kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A Lissu kuhusu kesi iliyopelekea kukamatwa kwa Ndege yetu na Kesi zingine mashauli yazo kushughulikiwa kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya kibiashara kama ICSID- international Center For Settlement of Investment Disputes.
====
Akikosoa kauli hiyo, David Zacharia Kafulila amenukuliwa kwenye mtandao wa tweeter akiandika haya " Sitaki kujadili suala la kesi, naomba nijadili suala moja tu la uelewa kuhusu ICSID na Uanachama wake kwani Tundu A Lissu amepotosha katika hilo na huenda akawafanya wasiofahamu kuamini kwamba Tanzania ni mwanachama wa ICSID kwa Sababu ya Udhaifu wa Mahakama na Serikali ya Tanzania katika kusimamia Uhuru wa Mahakama na majaji"
Tundu A Lissu alinukuliwa kupitia ClubHouse akieleza kuwa " Lazma ieleweke kuwa sababu ya mashauri haya ya mikataba baina yetu na kampuni za nje kushughulikiwa kwenye mabaraza haya ya usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kama ICSID inatokana na tabia ya Serikali yetu ikiwa chini ya JPM na hata Samia kuingilia mambo ya mahakama na hivyo mahakama kukosa uhuru. Hivyo mahakama zetu haziaminiki, serikali yetu haiaminiki, hatuaminiki kwasababu ya rushwa za majaji na kuingiliwa na Ikulu. ndio sababu mashauri haya yanaamuliwa ICSID "
Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.
David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa ni nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 nazo ni wanachama kama Sisi, Tumuulize Tundu A. Lissu kuwa JE? nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuonesha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?
Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?
TULIPENDE TAIFA LETU
===
" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"