Kafulila: Milango iko wazi kwa mtu au kikundi kununua vichwa na mabehewa ya SGR kisha kuyaendesha kwa miundombinu ya serikali kwa sharti la ubia

Kafulila: Milango iko wazi kwa mtu au kikundi kununua vichwa na mabehewa ya SGR kisha kuyaendesha kwa miundombinu ya serikali kwa sharti la ubia

David nadhan ana MKE Bora sana anayempa utulivu wa akiri ama ana MKE MSOMI na mtaalam wa BIASHARA au anasoma Sana. Asingekuwa MAFUPI Nadhani angeona mbali Sana kimaono....TUMPE MUDA.
Kwani ufupi unazuia maono?
 
Bakhressa kawekeza treni Uganda kwa ajili ya mizigo yake? Kawekeza au ni mteja?
Namaanisha anatumia treni kusafirisha mizigo yake?, mwekezaji yeye anafanya operations. Kuna kitu unachanganya maana ya kuwekeza na kuwa mteja, mfano mm ni natumia bandari ya dar kujngiza mizigo yangu hiyo haimaanishi mm ni mwekezaji wa bandari
Hata hivyo shirika la reli Uganda halina mwekezaji.

Hiyo treni ya utalii nadhani jiridhishe tena na hiyo taarifa, au naomba uniwekee hiyo taarifa nione. Maana SGR ni njia moja tu haiwezi treni hiyo unayosema kusimama hata masaa hayo manne kusubiri mtalii aliyeshuka kufanya utalii
Unauhakika na uñachokisema??!!
 
Pole kwa kuchelewa kukujibu nilikuwa busy kidogo.

Sasa iko hivi,

Kenya, Ghana na Tanzania zipo ligi moja kwenye viwango vya kimataifa kiuchumi.

Tena nashangaa kusikia mtu anaitaja Ghana kama mfano bora kiuchumi kulinganisha na Tanzania.

Kifupi Ghana inakabiliwa na matatizo makubwa kiuchumi kuliko Tanzania.

Ni moja ya mataifa yenye mgogoro mkubwa wa madeni. Hata Singapore ni special case ambayo huwezi kuifananisha sio tu na na Tanzania bali nchi yoyote ya Africa ,

Asia na hata Ulaya labda kwa mifano ya kukariri maana leo Singapore ni miongoni mwa nchi10 zenye maisha bora duniani. Imezipita nchi za ulaya zaidi ya 20 sembuse Tanzania.. kwaiyo kuihukumu Tanzania kwa ulinganisho wa Singapore ni kutofahamu vzr kwamba Singapore ni exceptiona case duniani.

Sasa unauliza eti taja mfano 1 tu wa PPP, haya ni maswali ya mtu asiejua maana ya PPP, au hajui kinachoendelea Serikalini.

Haya,

Mkataba wa Songas ni PPP, Mkataba wa TICS ulikuwa PPP, na hata mkataba wa sasa bandari na Adan ni PPP, Mkataba wa DPW ni PPP, TANESCO ina mikataba lukuki ya IPPP kwa kusaini PPA zote zile ni PPP.

kifupi IPP ni PPP. labda urudi shule kidogo utaelewa hili.

Siumesikia Juzi tu mamlaka ya DDC hapo Kariakoo imesaini mkataba wa PPP wa 37bn na kampuni ya TOSH kwa ujenzi na uendeshaji wa Business Complex.

Ukisema Tanzania imefeli kila sekta a wakati leo taasisi zinazofanya credit rating kama Moodys zinaipa daraja la juu kuliko nchi yoyote Afrika mashariki sijui unamaanisha hizo nchi zingine zina hali gani? World Economic Forum wanasema Tanzania inaongoza kwa uchumi jumuifu afrika kusini ya jangwa la sahara afu unasema hakuna inachokiweza.

Ni vema tusijadili kwa mizuka jukwaa la Great Thinker kama JF. Muhimu kujenga hoja kwa facts na reference na kama hujui unauliza badala ya kuhitimisha utadhan unajua. Maswali yote 5 nadhan hayana msingi baada ya hapa.
Usipumbazwe na ratings za kina moody..wakati serikali ndio mtoaji wa takwimu, ndie amelipia zoezi lote wanalofanya..ratings wanazofanya ni sawa na taarifa za kihasibu za fedha (financial statements) kwa makampuni..zinaweza zisikupe picha halisivile zinategemea takwimu ulizonazo..usidanganyike ndugu!
Hivi ubora wa nchi kiuchumi na maendeleo kwa ujumla unapimwa kwa kuangalia matatizo ya kiuchumi waliyonayo na kiwango cha madeni nchi inayodaiwa..?
Kwa hiyo Singapore raia wake wana vichwa viwili kila mmoja, au uspecial unaousema ni upi hasa..
Kama biashara ya Almas Botswana wanafanya vzr kuliko sisi huo uhakika wa mafanikio ya miradi ya PPP unaujenga kwenye msingi upi?
Hiyo miradi uliyotaja kwanza hakuna mahali popote inatajwa km flagship projects za PPP..nipe reference pse! lkn siyo vipaumbele kwa PPP.. Mwaka jana kulifanyika marekebisho ya sheria ya PPP sabb hata kanuni tu hazikuwepo..sijui hiyo miradi unataja ilikuwa inalindwa na kanuni zipi..
Hakuna sabb ya kufika mbali, the bottom line is...huwezi kufanya PPP pasina uhakika wa mradi unaofanya kuwa utafanikiwa, na hivyo ni muhimu kuwa na majaribio kwanza, ndio maana ya kusema Fanya kwanza huo mradi wa DART kabla ya kuingia kwenye miradi mingine..haraka ya nini? Huyo mbia aliyetajwa wa DART hata hajulikani lini anakuja, hata kipande tu cha karatasi ya makubaliano hakipo, mara unarukia SGR! Kwa hiyo siku hizi ufanisi unapimwa kwa kuorodhesha matarajio na mipango?
 
Nashauri,
Serikali awe ni mjengaji na msimamizi wa miundo mbinu uendeshaji waiachie sekta binafsi. Serikali ipate gawio la asilimia fulani kwa kila tiketi inayouzwa iwe ni mrabaha kwake kwa ajili ya monitoring and evaluation!
 
Naungana

Hoja nzuri sana hii
 
Wapi huko kasema?
Tumia akili unapojibu, soma na uelewe. Ukishaona neno kafulila hata kusoma vizuri hutaki, tumia akili, naamini hata kafulila hapendi nyie muwe kama marobots hivi

Kuna mtu nilikua nabishana nae kuhusu bakhressa kuwekeza reli ya Uganda, huyo jamaa hapo ndio kaja kuniambia nisibishe Jambo ambalo kafulila kasema, ndio nikamuuliza kwani afulila kasema bakhressa kawekeza reli ya uganda
 
Basi endelea na mada zako na watu wako

Back
Top Bottom