Pole kwa kuchelewa kukujibu nilikuwa busy kidogo.
Sasa iko hivi,
Kenya, Ghana na Tanzania zipo ligi moja kwenye viwango vya kimataifa kiuchumi.
Tena nashangaa kusikia mtu anaitaja Ghana kama mfano bora kiuchumi kulinganisha na Tanzania.
Kifupi Ghana inakabiliwa na matatizo makubwa kiuchumi kuliko Tanzania.
Ni moja ya mataifa yenye mgogoro mkubwa wa madeni. Hata Singapore ni special case ambayo huwezi kuifananisha sio tu na na Tanzania bali nchi yoyote ya Africa ,
Asia na hata Ulaya labda kwa mifano ya kukariri maana leo Singapore ni miongoni mwa nchi10 zenye maisha bora duniani. Imezipita nchi za ulaya zaidi ya 20 sembuse Tanzania.. kwaiyo kuihukumu Tanzania kwa ulinganisho wa Singapore ni kutofahamu vzr kwamba Singapore ni exceptiona case duniani.
Sasa unauliza eti taja mfano 1 tu wa PPP, haya ni maswali ya mtu asiejua maana ya PPP, au hajui kinachoendelea Serikalini.
Haya,
Mkataba wa Songas ni PPP, Mkataba wa TICS ulikuwa PPP, na hata mkataba wa sasa bandari na Adan ni PPP, Mkataba wa DPW ni PPP, TANESCO ina mikataba lukuki ya IPPP kwa kusaini PPA zote zile ni PPP.
kifupi IPP ni PPP. labda urudi shule kidogo utaelewa hili.
Siumesikia Juzi tu mamlaka ya DDC hapo Kariakoo imesaini mkataba wa PPP wa 37bn na kampuni ya TOSH kwa ujenzi na uendeshaji wa Business Complex.
Ukisema Tanzania imefeli kila sekta a wakati leo taasisi zinazofanya credit rating kama Moodys zinaipa daraja la juu kuliko nchi yoyote Afrika mashariki sijui unamaanisha hizo nchi zingine zina hali gani? World Economic Forum wanasema Tanzania inaongoza kwa uchumi jumuifu afrika kusini ya jangwa la sahara afu unasema hakuna inachokiweza.
Ni vema tusijadili kwa mizuka jukwaa la Great Thinker kama JF. Muhimu kujenga hoja kwa facts na reference na kama hujui unauliza badala ya kuhitimisha utadhan unajua. Maswali yote 5 nadhan hayana msingi baada ya hapa.