Kafulila: Tanzania ni nchi yenye deni dogo ukilinganisha na nchi zote zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hongera Rais Samia

Kafulila: Tanzania ni nchi yenye deni dogo ukilinganisha na nchi zote zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hongera Rais Samia

Naona anataka tuendelee kukopa ili nasi tuzifikie hizo nchi zilizotupita, na kwa spidi ya kukopa tunayoenda nayo asijali, lengo lake litafikiwa haraka, hizi teuzi zinatafutwa kwa shida sana.
Anataka mama amuangalie kwa jicho la huruma
 
Ila Kafulila huwa napenda Sana hoja zake kwa unazungumza kwa data,

#Uishi milele brother,

Haya BAVICHA njooni mlete data na ninyi ili kumpinga Kafulila,
Teuzi za mbeleko zinaondoa akili.
 
Hiki ndicho alichokiandika RC Mstaafu David Kafulila kwenye akaunti yake ya tweeter baada ya mjadala mkali Bungeni na hofu ya Watanzania juu ya ukubwa wa deni la Taifa kwa Sasa

Huenda Kafulila ndio mtu makini na mwenye hoja zaidi kwa Sasa Tanzania asiye na cheo chochote Serikali baada ya kupigwa chini U-RC kule Simiyu

Ila mtumie sms Kafulila, afanye kazi nyingine, uteuzi asahau hata asifie kufa kupona, uteuzi haupo tena kwake, akalime plz, anapoteza muda, akalime au afanye biashara.
 
Hiki ndicho alichokiandika RC Mstaafu David Kafulila kwenye akaunti yake ya tweeter baada ya mjadala mkali Bungeni na hofu ya Watanzania juu ya ukubwa wa deni la Taifa kwa Sasa

Huenda Kafulila ndio mtu makini na mwenye hoja zaidi kwa Sasa Tanzania asiye na cheo chochote Serikali baada ya kupigwa chini U-RC kule Simiyu

Kwahiyo bado tunakopesheka sio!? Basi sawa tuongeze kasi sasa
 
Aache uongo nimeresearch nikakuta hivi
Screenshot_2022-11-12-19-25-55.png
 
Anakuja mtu anavamia nyumba yako na kuanza kuwakata mapanga kwenye mikono. Unauliza kwanini unafanya hivi anasema shukuru mbona Familia yako hatujaikata vibaya nyumba za jirani wamekatwa miguu na macho. Nyinyi mna afadhali. Alisikika mlevi mmoja akijisemesha
 
Tatizo na uwezo wa kulipa. Sidhani kama tuna vyanzo vizuri na vingi kama Kenya. Mkopo unachukuliwa kasoro ya uwezo wa kulipa. Wakopeshaji hawakopeshi wahamisha madeni,wapiga mizinga,betting. Wanakopesha mtu anaweza thibitisha anaenda zungusha na kuleta marejesho.
 
Back
Top Bottom