Kagasheki awaasa kiaina Watanzania kuhusu kauli ya ukomo wa Urais kwa kutumia mfano Paul Kagame 2012

Kagasheki awaasa kiaina Watanzania kuhusu kauli ya ukomo wa Urais kwa kutumia mfano Paul Kagame 2012

Madikteta wote ninaowafahamu... Kwa kusoma au kwa kuwashuhudia moja kwa moja....
Mara zote hawakubali moja kwa moja kuwa watang'ang'ania madaraka...
Ila mienendo ya wapambe wao na maneno ya vinywa vyao ni ishara mojawapo kuwa nia yao ni thabiti...
Enyi ndugu wenye macho na akili...
Hamjashuhudia dalili zozote hadi sasa??
Sasa hao si ni madikteta? Huu Uzi unamzungumzia Rais J.P Magufuli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani pia si sahihi kwako kutuhukumu/tuhumu - whatever - tunaosema ni naivety kuamini eti hatang'ang'ania madarakani kipindi chake kikiisha (be it 2020 or 2025).

hakuna anaye draw conclusion yoyote hapa but tunasema uwezekano huo upo hata kwa kuangalia tu behaviours za peers wake anao rub shoulders nao (remember birds of the same feathers.......?). this is where am coming from.

so, hatumhukumu but tuna kila sababu ya kuwa na mashaka kwa kuangalia circumstances.
Ukiongelea uwezekano tu, unaweza kuongelea chochote.

Kuna uwezekano kwamba wewe ni Magufuli unatuchora tu hapa kupima upepo.

Let's stick to the facts please.

Fact 1. Katiba haimruhusu Magufuli ku violate term limits.
Fact 2. Magufuli amesema hatavunja katiba.
Fact 3. Kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajatenda ni kumuonea.

Katiba imeweka ukomo wa urais.Kuvunja ukomo huu ni kuvunja misingi ya katiba.

Katiba hiyo hiyo imempa Mtanzania yeyote haki ya presumption of innocence. Everybody is considered to be innocent until proven guilty. Si guilty until proven innocent.

In fact this is a seminal foundation of the international rule of law and morality.

Sasa, kama mnaipenda sana katiba na haki, msichague chague tu sehemu hii mnaipenda, hii mnaipotezea.Misingi hii ya haki manipenda, hii mnaipotezea.

Presumption of innocence is a pillar of any democratic modern society.

Mnataka kuongea siasa au principle? Mimi naongea principle, ndiyo maana Magufuli nampinga sana, lakini, tukija kwenye principle, mkianza kumuandama kwa kuvunja principle, inabidi nitetee principle na kwa hivyo kumtetea Magufuli.

Msichague kushikilia term limits, wakati hapo hapo mnadharau presumption of innocence.

Magufuli haja violate term limits, hata term ya kwanza hajamaliza. In fact amesema hata violate term limits.
Kumsema kwa kumhukumu kwamba ata violate term limits, ni kuvunja msingi wa katiba wa presumption of innocence.

Tukianza hivi, tutafika mpaka kwenye kukamatana wizi kwa makosa yatakayotokea 2025.

Mtu anaingiza data zako kwenye database. Umezaliwa wapi? Manzese kwa Mfuga Mbwa.

Una umri gani? Miaka 18. Wa jinsia gani, wa kiume.

Kwa kulingana na uchunguzi wa wanasayansi na wanasaikolojia, asilimia 99 ya vijana wa Manzese kwa Mfuga Mbwa wanaotimiza miaka 23 wanakuwa wezi tayari.

Kwa hiyo tukufunge tu kwa wizi utakaoufanya ukiwa na miaka 23.

Hapo vipi?

Kumfunga mtu hivyo kuna tofauti gani na kumhukumu Magufuli kwa makosa atakayoyafanya mwaka 2025?
 
nadhani pia si sahihi kwako kutuhukumu/tuhumu - whatever - tunaosema ni naivety kuamini eti hatang'ang'ania madarakani kipindi chake kikiisha (be it 2020 or 2025).

hakuna anaye draw conclusion yoyote hapa but tunasema uwezekano huo upo hata kwa kuangalia tu behaviours za peers wake anao rub shoulders nao (remember birds of the same feathers.......?). this is where am coming from.

so, hatumhukumu but tuna kila sababu ya kuwa na mashaka kwa kuangalia circumstances.
Mtu akisema wapinzani wa Magufuli hawana hoja, wanalialia tu, mara nyingi anakuwa anasema hivyo kwa sababu za kisiasa, na kukosa msingi wa haki wa kusema hilo.

Lakini, akisema hivyo katika hili la term limits, anaweza kuwa na logic.

Kwa sababu, mnalialia kuhusu kosa ambalo halijafanyika na mnayemtuhumu amesema hatalifanya.

Hivi, mmekosa makosa ya Magufuli ambayo kashayafanya ya kumvalia njuga, mpaka muende kukopa makosa ambayo hayajafanyika bado?
 
A love, declared for days to come, is as good as none.
- Tracy Chapman "If Not Now".

A hypothetical crime, declared for years to come, is as good as none.
 
I hardly believe the entire posting is from you!

Mstari huo tu nilioweka hapo unaonyesha kwamba mwandishi mwenye jina lililowekwa hapo juu sio mhusika. Labda awe 'under duress'.
Hapana.

Tatizo ni kwamba, hunifahamu, halafu unafikiri unanifahamu.

Mimi nasimamia principle, siangalii chama wala mtu.

Siasa za Tanzania mara nyingi si za principle, ni za kuangalia mtu na chama.

Ndiyo maana mtu anapinga kuvunja msingi wa katiba, kwa kuvunja msingi mwingine wa katiba.

Na katika hili la kumhukumu Magufuli kwa makosa ya kukisia atayafanya mwaka 2025, wakati amesema hatafanya hilo, ni kumuonea, ni kuvunja misingi ya presumption of innocence.

Kiranga ni yule yule.

Mama's first born, son
Like Genghis Khan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa Kizalendo wa Jamhuri ya Muungano wa Puetorica atapumzika 2025

Msuko suko wa ndani ya Chama cha PNP kutoka kwa Wazee wa Chama ni Mkubwa sana kiasi kwamba kutuliza hali ya hewa imebidi atolee ufafanuzi kutuliza hali

Raia wa Nchi hiyo wanapaswa kuamini asemacho Rais wao

Kwa taarifa yako anasema kuwa atatoka ili kupima upepo, akiona watu wananyamaza ataongeza, na akiona watu hawaafiki atatafuta mbinu za kuwanyamazisha wanaompinga waziwazi. Rejea kazi ya kundi la watu wasiojulikana. Hii kunajisi box la kura ni ili kupata watu wa chama kimoja ambao wataingia bila ridhaa ya wananchi kama uchaguzi wa SM, kisha wataagizwa kubadili katiba kibabe. Utetezi utakuwa hakuna anayeweza kuleta maendeleo kama yeye.
 
Ni kitu kibaya sana kumhukumu mtu kabla hajatenda kosa.

Ni ujinga kumhukumu mtu mwenye makosa mengi, kwa kuacha makosa aliyoyatenda, na kutumia makosa mnayofikiri atayatenda.

Mimi si mtetezi wa Magufuli. La hasha. Nimemsema sana hapa.

Lakini, katika hili la term limits, amesema hatavunja katiba. Haikuwa lazima aseme hilo, lakini amesema.

Kumzonga kwa hilo, ni kukosa heshima, kukosa adabu, kukosa umakini na kukosa hoja.

Kwa sababu, kila siku Magufuli anafanya makosa. Kwa maneno na matendo.

Amefanya makosa makubwa mengi. Kuanzia kuapisha watu kuwa mawaziri kabla hawajaapishwa ubunge mpaka kukataza mikutano ya hadhara ya kisiasa inayoruhusiwa na katiba.

Kuanzia kusema atapiga mpaka shangazi za wapinzani mpaka kuingilia biashara ya korosho na kuangusha mapato ya bidhaa za kilimo kwa asilimia 55 ndani ya mwaka mmoja.

Sasa mtu ambaye akifungua mdomo tu inatoka harufu ya ujinga, kwa nini mnamhukumu kwa makosa ambayo atayafanya 2025, wakati kuna makosa mengi kafanya ndani ya miaka minne iliyopita?

Mnawapa msemo wanaosema wapinzani wa Magufuli wanapinga tu, bila hoja.

Ukizushiwa kwamba utaiba mwaka 2025 na kuhukumiwa kwa kosa hilo ambalo hujalifanya bado, utaona hilo ni sawa?

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Kingine, wapinzani wa Magufuli wanapoongelea kwamba atavunja katiba na kuendelea kuwa rais baada ya term limits kuisha, hilo lina maana kwamba 2020 wameshakubali Magufuli atashinda?

Kama hawamkubali Magufuli, kwa nini wasipige kampeni aondolewe 2020?

Ukilalamikia uchaguzi wa 2025 wakati wa 2020 hatujafanya, ni kama umekubali tayari Magufuli kashinda 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umewaza mbali sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mtu akisema wapinzani wa Magufuli hawana hoja, wanalialia tu, mara nyingi anakuwa anasema hivyo kwa sababu za kisiasa, na kukosa msingi wa haki wa kusema hilo.

Lakini, akisema hivyo katika hili la term limits, anaweza kuwa na logic.

Kwa sababu, mnalialia kuhusu kosa ambalo halijafanyika na mnayemtuhumu amesema hatalifanya.

Hivi, mmekosa makosa ya Magufuli ambayo kashayafanya ya kumvalia njuga, mpaka muende kukopa makosa ambayo hayajafanyika bado?
it's very unfortunate unaonekana kutumia nguvu nyingi sana katika vitu vinavyohitaji simple mental application.

there's no harm in being hypothetical when talking of probabilities.... it's inevitable.

and the binary hypotheses are:
1) JPM may vouch for extending the presidential term limit, all circumstances considered
2) JPM may not vouch for the presidential term limit extension

so, the probability could be 50/50 either way... and you cannot say am wrong with this perspective.

kapish???
 
Mtu akisema wapinzani wa Magufuli hawana hoja, wanalialia tu, mara nyingi anakuwa anasema hivyo kwa sababu za kisiasa, na kukosa msingi wa haki wa kusema hilo.

Lakini, akisema hivyo katika hili la term limits, anaweza kuwa na logic.

Kwa sababu, mnalialia kuhusu kosa ambalo halijafanyika na mnayemtuhumu amesema hatalifanya.

Hivi, mmekosa makosa ya Magufuli ambayo kashayafanya ya kumvalia njuga, mpaka muende kukopa makosa ambayo hayajafanyika bado?
nimekujibu hapo juu tayari.
 
Wasiwasi wenu ni upi? Kati ya mambo ambayo huyu mzee hatofanya ni kuongeza muda wa kukaa madarakani. Tuzifufue hizi nyuzi 2025.
Huyu jamaa hawezi achia madaraka haya majamaa ya ccm mazwazwa ikifika 2025 utaona yatatengeneza vikundi kutoka vijijini wenye kuimba aendelee wa kwanza yule aliye hamia chato sup iika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa Kizalendo wa Jamhuri ya Muungano wa Puetorica atapumzika 2025

Msuko suko wa ndani ya Chama cha PNP kutoka kwa Wazee wa Chama ni Mkubwa sana kiasi kwamba kutuliza hali ya hewa imebidi atolee ufafanuzi kutuliza hali

Raia wa Nchi hiyo wanapaswa kuamini asemacho Rais wao
Nashangaa sana watu wanashikia bango suala la 2025, wakati nchi ina uchaguzi 2020.

Ina maana washakubali kwamba wameshindwa uchaguzi wa 2020?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumhukumu Magufuli kwa makosa ya kinadharia anayodaiwa kuwa atayafanya mwaka 2025 ni ujinga.

Hususan ikiwa Magufuli tayari ana makisa mengi sana ambayo kayafanya tayari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama si ubishi tuliouzoea kutoka huko hata katika mambo yaliyo wazi, inaelekea kwako neno "uzoefu" halina maana yoyote.
 
Back
Top Bottom