Ukiingia sehemu za watu jitahidi sana upate uyaelewe maeneo kabla ya kukurupuka kuandika unachodhani ni sahihi kwa kila mtu.
Kwahiyo wewe ulitegemea tofali iuzwe shilingi ngapi kama saruji inauzwa 24,000? Hata elimu ya biashara huna achilia mbali kuifanya hiyo biashara. Pale kilimanjaro kuna kiwanda cha saruji na ipo karibu na tanga lakini tofali linauzwa hadi 1,800 wakati saruji ni 14,000 hadi 16,000 kutegemea na eneo sembuse huko? Kwahiyo kuwa jirani na geita, katoro au chato ni justification au sababu ya kuwafanya hao wauza tofali nao wauze kwa 1,000 au 1,200? Maskini wa fikra na akili wewe.
Unataka kuuza kwa 1,200 hata 1,000 anzisha project yako, tafuta wateja wauzie wala usisingizie watu. Kama bidhaa yako ina ubora watanunua kama haina huwezi pata wateja na ndiyo utakuja na haya uliyoandika hapa.
Kwanza unatakiwa kujua kwamba wao wanajenga sana tena sana kwa kutumia tofali za kuchoma na watu wanauza kwa 200, 300, 500 na 600 na wote wanauza tofali zao kwa wateja wao na huwezi sikia ulichokiandika hapa eti anzisha kiwanda uuze 1,200 wakuue. Kiazi mkubwa wewe.
Wewe sema bidhaa yako ilikataliwa kutokana na ubora hafifu na sasa unatafuta sababu ya kufichia aibu yako huku washindani wako wakipeta na kuuza tu bila shida yoyote.
Ulijiuliza au uliuliza ni kwanini majengo yao mengi yawe ya serikali au watu binafsi wanatumia sana tofali za kuchoma zinazouzwa kati ya 300, 500 au 600 ambazo zinahitaji saruji nyingi wakati wa kuzijengea?