Kagera (Bukoba) mahali pa ovyo kuwahi kutembelea

Kagera (Bukoba) mahali pa ovyo kuwahi kutembelea

Takwimu hazijawahi kuongopa,takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa miaka 3 mfululizo zinaonesha Kagera ndio Mkoa maskini Tanzania.

Huwa nikipata safari ya kwenda Bukoba unawaza hata kupata Hotel nzuri za kulala,yani Hotel na Lodge zao ni mbovu kupindukia wanazidiwa na Kigoma.
Sema huna hela kilaza wewe kwa maana mwenye hela zake anajua wapi pa kulala na huwezi ona anakuja hapa kuandika kwamba nawaza pa kulala.

Hivi mpaka sasa bado unasimama na takwimu za NBS ambayo wakusanya takwimu wao ni wale tulioonyeshwa kwamba walikuwa wanajaza takwimu wanazozijua wao kwenye madodoso waliyopewa wakiwa vyumbani mwao wakati wanafanya utafiti wa matumizi ya kaya binafsi?

Kwanza unajiita Econometrician ikimaanisha una uelewa wa uchumi na takwimu sasa twambie kutokana na takwimu hizo za NBS ni variables zipi zilitumika kujustify hilo. Takwimu ni takwimu tu lakini kuzichambua na kuzielewa ni kitu kingine kabisa na hapo ndipo unakutana na hizo mambo za sijui NBS imesema, n.k.

Mwaka jana nilishiriki kwenye kisemina fulani cha utoaji wa matokeo ya sensa na matumizi yake kwa baadhi ya maeneo ambayo walikuwa wametoa matokeo.

Ni kwamba hata watumishi wa NBS wenyewe hawaelewi hizo data wanazotolea matokeo zina maana gani na zinatumikaje kwa sababu wawasilisha taarifa yapo maswali waliulizwa lakini wakashindwa na wakaishia kutwambia takwimu zipo hivyo kama zilivyo hivyo tusihoji sana.

Kuna tafiti za matumizi ya kaya binafsi ambayo yanaonyesha watu wa mkoa X wanatumia pesa kununua kila hitaji la nyumbani kutoka dukani na watu wa mkoa Y wanapata mahitaji yao shambani moja kwa moja kwa asilimia 90 na 10 ni kutoka dukani. Ukiwaangalia hawa matumizi yao ya pesa ni tofauti kabisa lakini matokeo ya NBS yanakwambia wapo kwenye kapu moja na kwamba anayepata mahitaji yake kutoka dukani kwa asilimia 10 tu ni maskini wa kipato ukilinganisha na anayepata mahitaji yake kutoka dukani kwa asilimia 100 bila kutwambia spendings zao kwenye maeneo mengine zikoje kutokana na savings wanazozifanya
 
Mshikaji wangu alibahatisha mmoja wife material kabisaa tukiwa chuoni, first year mpaka tuna maliza had now wako wote, na alimkuta sealed, ni zaid ya five years, mshikaji wangu pale kapata mtu kweli kweli, ni bahati pia.
Sio kweli kwamba Wairaq wote ni wahuni
 
UKUAJI WA MJI.

Kwa ujumla Ukuaji wa MJI naupa 5% hakuna ujenzi mpya kabisaa tofauti na ukiingia mikoa kama Mwanza, Geita, Dodoma, ambapo ukipita Kwa mara ya kwanza Tena barabarani tu unavutiwa na majengo mapya mazuri. tofali ya nchi.5 inauzwa 1500 huku bei ya cement ikiwa 24,000. KATORO GEITA na CHATO ambazo ni jirani kabisa tofali inauzwa 1000-1200 mfuko cement ukiwa inauzwa 24,000 pia. anzisha kiwanda sasa 😂 uuze 1200 wakuue.
Ukiingia sehemu za watu jitahidi sana upate uyaelewe maeneo kabla ya kukurupuka kuandika unachodhani ni sahihi kwa kila mtu.

Kwahiyo wewe ulitegemea tofali iuzwe shilingi ngapi kama saruji inauzwa 24,000? Hata elimu ya biashara huna achilia mbali kuifanya hiyo biashara. Pale kilimanjaro kuna kiwanda cha saruji na ipo karibu na tanga lakini tofali linauzwa hadi 1,800 wakati saruji ni 14,000 hadi 16,000 kutegemea na eneo sembuse huko? Kwahiyo kuwa jirani na geita, katoro au chato ni justification au sababu ya kuwafanya hao wauza tofali nao wauze kwa 1,000 au 1,200? Maskini wa fikra na akili wewe.

Unataka kuuza kwa 1,200 hata 1,000 anzisha project yako, tafuta wateja wauzie wala usisingizie watu. Kama bidhaa yako ina ubora watanunua kama haina huwezi pata wateja na ndiyo utakuja na haya uliyoandika hapa.

Kwanza unatakiwa kujua kwamba wao wanajenga sana tena sana kwa kutumia tofali za kuchoma na watu wanauza kwa 200, 300, 500 na 600 na wote wanauza tofali zao kwa wateja wao na huwezi sikia ulichokiandika hapa eti anzisha kiwanda uuze 1,200 wakuue. Kiazi mkubwa wewe.

Wewe sema bidhaa yako ilikataliwa kutokana na ubora hafifu na sasa unatafuta sababu ya kufichia aibu yako huku washindani wako wakipeta na kuuza tu bila shida yoyote.

Ulijiuliza au uliuliza ni kwanini majengo yao mengi yawe ya serikali au watu binafsi wanatumia sana tofali za kuchoma zinazouzwa kati ya 300, 500 au 600 ambazo zinahitaji saruji nyingi wakati wa kuzijengea?
 
MAISHA

Nimeshangaa ndizi za Bukoba kuuzwa 3 Kwa 1000 Kwa Baadhi ya Maeneo ya Bukoba MJINI ilihali Dar tunanunua mpaka 6 Kwa 1000. hapa hakuna soko la wakulima AMBAPO utapata vitu Kwa bei RAHISI nyanya tunapima Kwa kilo sio kama kwetu fungu Hadi la 300 lipo..

Maisha ni ya kati sio ghali sana Wala sio RAHISI sanaaa. mzunguko wa pesa ni mdogo Sanaa sanaaaa Kwa kifupi Pesa ni ngumu hapa Bukoba. usafiri ni boda Kwa kiasi kikubwa bajaji ni chache sanaaaa hivyo ukija ujipange kidogo. maeneo ya starehe YAPO kuanzia fukwe za ziwa Victoria, club yetu pendwa (RIO), bunena (my best) nk
Endelea kushangaa kwa maana ulijibeba na mentality ya huko ulipotoka.
Ni simple tu na hiyo ni fursa kwako ingia sokoni tafuta mfanyabiashara mdadisi na tengeneza mahusiano ya kibiashara ili nawe uanze kuagiza zinakotoka kwa bei chee uje uuze kwa bei kubwa. Sasa ukifika kule kwa kina mangi si utalia kabisa na kuja kutwambia umelala njaa?

Suala la usafiri wa bajaji kwa mji kama wa bukoba siyo sehemu yake sana na wanaofanya hawategemei hizo bajaji pekee. Movememt ya watu ni kupanda na kushuka vilima vilovyozunguka huo mji na kwa kiwango kikubwa watu hawakai hapo kati wao wanaita bondeni. Labda kwa sasa ambapo wamepunguza mwinuko wa barabara ya uganda inaweza wezesha bajaji kuongezeka upande wa hiyo barabara kuelekea rwamishenye. Vinginevyo bajaji zingekuwa zinaokotwa chini kwa kushindwa kupanda milima sababu hata magari kuna wakati wanashindwa kupanda.

Bodaboda ni usafiri namba moja na wenyeji hawalalamiki zaidi ya wa kuja lakini utashangaa unaenda mwendo mrefu anakucharge 1,500 au 2,000 wakati ungekuwa mikoa mingine kwa umbali sawa na huo ingekutoka 3,000 au 4,000. Ukitafiti utapata majibu ni kwanini daladala ziliondoka mjini na kusalia za kutoka mjini kwenda vijijini au wilaya jirani.

Kuna maeneo kama bugabo kuna daladala zinaenda huko kutokea mjini kwa 2,000 au 3,500 lakini watu wengi wako tayari kupanda bodaboda kwa 7,000 au 10,000 ila si kusubiri hiyo daladala ijae au iende inasimama kujaza abiria tena kwa kusimama.
 
Mkuu merckme nimejaribu kupitia majibu Yako Kwa Kila alieandika kwenye huu uzi na muandiko wako unasema mengi na ya Ziada kuliko maandishi Yako. Nikupongeze Kwa Kila herufi Yako iliyodhihirisha niliyoyaandika...... JIREKEBISHENI au Bakini na Ujinga wenu
 
Socio cultural difference. Labda na wewe ungesema ni mtu wa wapi na mambo yako ni yapi hasa ili tuone nini ilisababisha hayo yaliyokukuta.

Kikubwa ni ku embrace difference zetu na kuendana na mambo. Hizo tabia Tanzania sehemu nyingi zipo zinatofautiana ujazo tu. Kwa maeneo ya mikoa ambayo ni ya mjini inapungua, kwa maeneo ambayo ni ya mipakani na kuna kabila moja la asili lime dominate hayo mambo yanakuwa mengi zaidi.

Mara ya kwanza natembelea Bukoba, japo sikukaa sana lakini nilienda hadi maeneo ya ndani ndani kama vile kata ya Rubafu nikaishi nao fresh tu.

Mambo mengine ni uoga wa asili wa wazawa. Hata Pwani ukiend deepkuna namna watu wanagwaya mgeni ukiingia na kuanza mambo kama ya kutafuta mashamba, biashara n.k

Ni kama hata kwa level ya taifa tunavyoogopa kutoa uraia pacha na kuwapa wageni haki au uhuru wa kununua ardhi n.k Lakini kuna watu kibao tu wamejenga na kununua ardhi kienyeji.
Upo sahihi sana. Kimsingi mtoa mada ni mshamba tu. Asiyejua kutofautisha na kubadilika kutokana na mazingira
 
Uchambuzi gani huu? Nijiuavyo, Kagera si Bukoba wala si ya wahaya. Kwani wapo wahangaza, wanyambo, wasukuma na makabila mengine. Tatizo lako ni kutumia muda mwingi kutaka kila kitu kiwe kama unavyotaka. Kwa wanaojua ubunifu, unapokuta sehemu fulani inakosa kitu au vitu, hizo ndizo fursa na siyo lawama.
Kwa hiyo na takwimu za uchumi wa mkoa wenu huwa anaandaa yeye!
 
Hehe nimesoma yote, nahisi upo kwenye hamashauri za bukoba, pole sana kaka. Hapo kwenye halmashauri ndo kwenye kitovu cha huo ukabila. Sababu humo kunq comprise wazee wa baraza ambao ni typical wakabila. Anyway nimewahi kuwa na rafiki wa kihaya kipindi tupo chuo. Nlichelewa kugundua kuwa jamaa alikua rafiki kwangu sababu ya umaterial issues. Kwa maana alitamani kuwa karibu yangu sababu ya resources nlizonazo, nlipozipoteza zile resources nlihisi angekua mtu wa kumtegemea .. ooh.. bojo ndo alikua mtu wa kwanza kuzungusha maneno kwamba nimefulia nimeuza gari, nauza vitu vya ndani .. asivokua na aibu nliporudi kwenye game at a higher profile than before jamaa akawa anansumbua nkam ignore. Point of reference ni kwamba bora marafiki wachagga wanajua kuwa na staha wanapomshobokea mtu ili wapate kitu ila sio wahaya man.
 
Hapa unadhihirisha ni namna gani ulivyoandika ili kujionesha unajua kuandika mihemko uliyonayo na members wamekuprove wrong. Rejea ulichoandika kwenye thread yako na ulichokiri hapa.

Thread yako nikianza kuichambua kipengele kwa kipengele utajiona ni namna gani ulivyo jinga kama ulivyoanza kujionesha hapa maskini mkubwa wewe.

Unaongelea ardhi kuuzwa bei ghali na wakati huo huo unasema hakufai. Sasa hiyo ardhi ulitaka kununua ili ikufaidishe namna gani wakati hakufai? Kwanini uhangaike na pasipo faa badala ya kuhangaika na ardhi ya kwenu kunakofaa au sehemu nyingine?

Kwanza unapaswa kuelewa ya kwamba huko hakuna eneo wazi lisilo na mwenyewe na usidanganyike kuona unapita sehemu kuko wazi na kumezungukwa na miti ya kupanda ukafikiri hakuna matumizi, pole sana. Hiyo kijani unayoiona haipo kwa bahati mbaya bali ni jitihada za jamii husika kutunza uoto wakipata support pia ya mvua. Ukifika sehemu tumia muda wako kuijua na si kujibeba beba na thread zisizokuwa na mbele wala nyuma.

Ungeongelea suala la siasa huko labda ningekuelewa lakini mengine unapuyanga puyanga kwenye umande.
Ni mtu wa kusikiliza akili za wengine sio kutumia za kwake...ndo maana anashindwa kuadapt.
Bukoba ukiachana na siasa...mengine ni kawaida tu....ni kutafuta gape na kuanzisha biashara.
Watu kama hao ni kutowajibu. Maana wana akili ndogo
 
Kwa mara ya kwanza nafika nilifurahia mazingira mazuri, ukijani mwingi na Hali ya hewa tulivu kabisaaa ikiambatana na mvua hasa nyakati za asubuhi. Baadhi ya Maeneo yana muonekano mzuri wa ziwa hivyo kufanya Mkoa huu kuwa kuwa na view nzuri hasa Kwa wageni.

Kwa kuwa ni mzee wa Fursa Cha kwanza nilichokiona ni UWAZI mkubwa maeneo nikajipa moyo kwamba ardhi ni sehemu ya kwanza ya kuwekeza kama ntabahatika kukaa Kwa muda mrefu.

LAauhala...... Siku mbili tu naanza kupata majuto makubwa na kuchukia Mkoa na watu wake. Twende Wote.

PICHA LINAANZA kutafuta nyumba ya kupanga nyumba zote nazopekekwa ni local vibaya mnooooo zenye ahueni bei haieleweki na ni chache vibaya sanaaa kimsingi kama una hela njoo wekeza kwenye majengo (ila sikushauri ntakwambia kwanini)

BIASHARA ndo kizungumkuti Ile costumer care tulioizoea Kagera (Bukoba) haipo hapa mchoma mahindi anaringa hata Moo hagusi. hakuna karibu hakuna ahsante, kauli nzuri Kwa mteja huku ni ndoto za mchana.

Mbaya zaidi wageni wote walojaribu kufanya BIASHARA wameshindwa kutokana na ukabila ulokubuhu wakija wataongea kihaya usijpojibu kesho usitegee atarudi... ukimuweka MUHAYA watachunguza kujua mwenye BIASHARA wakijua umeumia.

ARDHI.

Eneo kubwa lipo wazi likiwa na migomba hapa naongelea km 5-10 kutoka mjini katikati ila gusa unase kiwanja cha 20*20 Wahaya wanataka million 8 ukibahatisha utakutana na 5 MILIONI nunua kiwanja DODOMA ila sio hapa, hii inasababisha wageni kutonunua ardhi na wengi kununua mikoa ya Mwanza na Geita.. wahaya wanaachwa na ardhi Yao ikiwa na migomba na majivuno Wasijue miaka kadhaa ijayo huenda ikawa Mkoa duni kuliko popote TANZANIA.

UKUAJI WA MJI.

Kwa ujumla Ukuaji wa MJI naupa 5% hakuna ujenzi mpya kabisaa tofauti na ukiingia mikoa kama Mwanza, Geita, Dodoma, ambapo ukipita Kwa mara ya kwanza Tena barabarani tu unavutiwa na majengo mapya mazuri. tofali ya nchi.5 inauzwa 1500 huku bei ya cement ikiwa 24,000. KATORO GEITA na CHATO ambazo ni jirani kabisa tofali inauzwa 1000-1200 mfuko cement ukiwa inauzwa 24,000 pia. anzisha kiwanda sasa 😂 uuze 1200 wakuue.

MAISHA

Nimeshangaa ndizi za Bukoba kuuzwa 3 Kwa 1000 Kwa Baadhi ya Maeneo ya Bukoba MJINI ilihali Dar tunanunua mpaka 6 Kwa 1000. hapa hakuna soko la wakulima AMBAPO utapata vitu Kwa bei RAHISI nyanya tunapima Kwa kilo sio kama kwetu fungu Hadi la 300 lipo..

Maisha ni ya kati sio ghali sana Wala sio RAHISI sanaaa. mzunguko wa pesa ni mdogo Sanaa sanaaaa Kwa kifupi Pesa ni ngumu hapa Bukoba. usafiri ni boda Kwa kiasi kikubwa bajaji ni chache sanaaaa hivyo ukija ujipange kidogo. maeneo ya starehe YAPO kuanzia fukwe za ziwa Victoria, club yetu pendwa (RIO), bunena (my best) nk

MAJUNGU

Sijawahi kuishi sehemu kama hiii narudia SIJAWAHI, Kufuatiliana maisha huku ndo nyumbani, MAKUNDI ya WhatsApp ya MAENDELEO ya Mkoa yamejaa MAJUNGU, kusemana, unafki, ukabila na ubinafsi uliokithiri Kuna kamtu kanaitwa KIMODOI ndo Kigogo wao huku😂😂😂 ndo kanaendesha Mkoa kakisema Kila mtu Hadi Mkuu wa Mkoa anatetemeka kajamaa kanaishi MAREKANI so wadau ndo wanakaabudu kinoma kana MAJUNGU, kanafki, MAKUNDI badala ya kujadili Maendeleo kutwa kucha ni kusema watu voice note kama 1000 zote za MAJUNGU tu sasa usiombe Wahaya wakuchukie 😂😂 ebwanaaa eeeeee kama ni mtumishi maisha Yako yatakua ya shidaaa Kwa kifupi BUKOBA ni ya Wahaya Wageni wote hakuna anaetamani kuwepo hili eneo.

SIASA

😂😂 oya wakuu kama unataka kugomebea hata uenyekiti wa MTAA Na si mzawa huku sio kwako... mikutano ya hadhara ni ya kihaya wegeni tunaduwaa tu... Majungu na Kukwamisha Maendeleo Ili kumfelisha kiongozi Fulani ndo siasa za Kagera (BUKOBA)... mbunge wao BYABATO chamoto anakipata aseee jamaa miradi haetekelezeki Kwa sababu ya CHUKI na uBINAFSI...

Kiongozi mstaafu Yuko tayari kukwamisha mradi ila aliepo asifanikiwe. NI AIBU MAKUNDI yaliyopo Kagera hasa. BUKOBA niaibuuuuu viongozi WA Mkoa wakiongozwa FATMA MWASSA, mbunge NEEMA LUGANGIRA Ndo kabisaaaaa UKISIKIA VITA KISIASA NA FITNA NJOO BUKOBA na sijui CHADEMA Mnafeli wapi.

UTENDAJI WA VIONGOZI

Hapa naongelea Ngazi ya Mkoa mpaka Watendaji wa kijiji.. NGAZI ya Mkoa hakuna kitu Mama MWASSA anajua KUJINUFAISHA tu kupitia wafanyabiashara Kuandaa na kuhudhuria matamasha ya hovyo tu akiambatana na Chawa wake (Kuna naskia kijamaa kinaitwa Mtu Mfupi na KIGOGO wao Kimodoi natamani sana kuwaona hawa)... Mkuu wa Wilaya SIMA na WAKURUGENZI wake ndo kabisaaa miradi ya serikali inajiendeaaa tu Hakuna HATUA zozote zinazochukuliwa Kwa wazembe... ila nashindwa kuwalaumu mana Wahaya wenyewe ni sehemu ya kukwamisha Maendeleo Yao binafsi.

ELIMU

Kizazi Cha Prof TIBAIJUKA kikiisha Kagera itahitaji msaada wa serikali kuinuka Tena. ELIMU hapa ni duni mnoooo mnoooo... majivuno mengiiii ila uhalisia ni sifuri.

HITIMISHO.

Kagera (Bukoba,) sio ya wageni ni Moja ya sehemu za hovyo kuwahi kwenda nimeishi Tabora, Dodoma, Arusha, Tanga, Pwani, Moro, Dar, Mwanza, Shinyanga, Geita, Kilimanjaro na maeneo mengine nimepita ila huu MJI 🙌 hakuna mgeni anaetamani kuwepo hapa UKABILA, MAJUNGU, FITNA, UBINAFSI NA CHUKI vinawaangamiza Wahaya kimya kimya...

Huu ni Mkoa mkongwe sana ilaa MIAKA kadhaaa utakua Mkoa duni kuliko maelezo. BUKOBA ni MANISPAA inayodumazwa na tabia za Wenyeji na ni swala la muda hata Geita ilopewa MANISPAA juzi itaipiku ukiachilia mbali KAHAMA na MANISPAA zingine. inahitajika mabadiliko makubwa sana ya kifikra kuwakomboa Wahaya na Mkoa wao. mabadiliko haya yanahitajika pia kiutawala.

Mwisho RIO DE JENEIRO ni club nzuri mnoo na inapendezesha na kuchangamsha mji ila haiondoi ukweli kwamba sheria zimekiukwa.

WAHAYA SAMAHANINI ILA NI MUUKUBALI UKWELI AU MBAKI NA UKABILA WENU mi naondoka NIMEPACHOKA. KITUO KIFUATACHO BAADA YA MUDA MREFU NARUDI GEITA IKIWA MANISPAA
Kwa kiasi fulani ulichoongea kina ukweli,lkn changamoto huwa hazikimbiwa kaka bali unakabiriana nazo,, penye uzito kuna wepesi,,mlango mmoja ukifungwa fungua mlango mwingine hapo hapo,,nilikuwa hapo kipindi fulani,kuna jamaa alipigwa vita sana lkn hakukata tamaa,anatokea huko kaskazini,nadhani wajua hawa jamaa wanavojua biashara,kwasasa anaendelea vyema na tanpoint yake,ametanuka,na kawafanya wenyeji waamke mapema kufungua biashara zao,maana walizoea kuamka hadi saa nne ati mtu ndo anafungua duka lake!!
Supermarket ilikuwa ni fidodido tu ya wahindi fulani,kwa sasa hata wenyeji wamefungua zao, midomo imefungwa watu wamechangamka sasa,majungu yanapungua japo kwa taratiibu sana.
 
Kwa kiasi fulani ulichoongea kina ukweli,lkn changamoto huwa hazikimbiwa kaka bali unakabiriana nazo,, penye uzito kuna wepesi,,mlango mmoja ukifungwa fungua mlango mwingine hapo hapo,,nilikuwa hapo kipindi fulani,kuna jamaa alipigwa vita sana lkn hakukata tamaa,anatokea huko kaskazini,nadhani wajua hawa jamaa wanavojua biashara,kwasasa anaendelea vyema na tanpoint yake,ametanuka,na kawafanya wenyeji waamke mapema kufungua biashara zao,maana walizoea kuamka hadi saa nne ati mtu ndo anafungua duka lake!!
Supermarket ilikuwa ni fidodido tu ya wahindi fulani,kwa sasa hata wenyeji wamefungua zao, midomo imefungwa watu wamechangamka sasa,majungu yanapungua japo kwa taratiibu sana.
Kaka nakuelewa sanaaa ila Kwa tunao jitafuta hii Sio sehemu sahihi kuwepo
 
ukifika kule wenyewe wanachapa kihaya tu hawajali kama wewe ni mgeni wao yamkini utajisikia vibaya.Wahaya shemeji zangu ila kwajinsi mlivyo na mambo ya hovyo nimechukia wahaya wote hadi dada yenu,sitokubali wanangu warithi ukabila,tabia za hovyo..n.k😂

Watu gani nyie kuvunja undugu kwenu ni jambo la kawaida tu.🙌
Wasamehe bure tu - udongo uliowaumba ulikuwa wa mwisho mwisho
 
Nilitoka mkoa mwingine nikahamishiwa dodoma nikiwa shule ya msingi na nilipata the same treatment, nilibaguliwa haswaaa kwa kuonekana najidai kwa sababu nilitokea kwenye mji mkubwa kuliko Dodoma, na siku zote wangenicheka accent yangu hadi walimu waliniita mjinga natakiwa nirudishwe darasa mbele za wanafunzi wenzangu. Kiufupi nilikuwa broken vibaya mnoo na Ilinichukua zaidi ya miezi 6 na nikaishi nao na kurudi kwenye round ya best students hapo ndo nikapona kiasi

Nimetoka dodoma nikaingia mkoa flani, huko issue ilikuwa the worst, na sio tu kwa kunyanyapaliwa, mkoa ule wa kusini ni walozi hadi mtoto wa form one anakushauri muende kwa mganga kwa sababu daftari uliloibiwa linaenda kuchawiwa. Unaingia kwenye paper unaona karatasi nyeupeee peee na machozi yanatoka tuu hadi nikashuka sana paper ya form two lakini home hawakunishangaa kwa sababu walikuwa wanajua ni nini nilikuwa napitia maana nilikonda sanaaa.

Siwezi kuongelea mengi zaidi kwa sababu ni rahisi kujulikana Ila jua tu nimeishi mikoa mingi ambayo inatawaliwa na wenyeji including Kagera. Issue ya lugha ni kawaida maana bukoba hata ukienda makanisani wanatumia kihaya na kila pahali na tena bora leo hii kuliko zamani.

Kwa hiyo ukiingia miji midogo kwa mentality ya wao wanatakiwa kubadili system ya maisha yao ili wakuaccomodate wewe badala ya wewe kuwa adaptable. Utakosea kwa sababu ni same scenerio dunia nzima kwenye issue ya wageni vs wenyeji,


ulichokipitia nakielewa lakini usijifiche katika hiyo trauma mkuu, move on kwa sababu nilipitia mazito zaidi ya hayo lakini SIJAWAHI kuwaita watu mashetani au kulaumu shortcomings zangu. Take full responsibility of your life mkuu ili uweze kurudisha total control kwako.. Heal mkuu
Umemfafanulia vyema mkuu. It seems ana matatizo makubwa kuliko hata hao anaowaita mashetani.
 
Back
Top Bottom