Jimbi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2010
- 4,444
- 4,967
SAHIHI kabisa, mimi ni shahidi wa hiloNasikia hawaoni haibu kuvunja undugu ili wakulane wenyewe kwa wenyewe, ni kweli?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SAHIHI kabisa, mimi ni shahidi wa hiloNasikia hawaoni haibu kuvunja undugu ili wakulane wenyewe kwa wenyewe, ni kweli?
Kuhusu kupata kiwanja ni sahihi, hakuna mtu akate shamba lake lenye migomba akuuzie kwa pesa njaa. Tofautisha Mhaya na Mzaramo.
Elewa madaKuhusu kupata kiwanja ni sahihi, hakuna mtu akate shamba lake lenye migomba akuuzie kwa pesa njaa. Tofautisha Mhaya na Mzaramo.
Funza? Kwa mwaka 2025???? What the hell?Alikuwa anafocus na "ubaya"..
Kuonesha bukoba ni mbaya
Nadhani hilo ni tatizo la watu wengi ambao wakiwaona wahaya wa mjini wanategemea wakute maghorofa bukoba mjini. Wanapokutana na hiyo disapointment wanaanza kutafuta uhalali wa kuionesha ni mbaya kiasi gani
Amesahau tu na funza na shida ya maji na vyoo kwa baadhi ya sehemu. Nimemsaidia kuongeza 😁
Kila nyumba ina nyarujuHizi Sina USHAHIDI nazo mkuu sijazisikia sanaaaa
Sahihi kabisa, nimekaa Kagera miaka takriban mitano, ilikuwa shangwe na burudani. Japo mwanzo maisha yao yalinishangaza. Ni watu wema hasa kama wewe ni top boss au una pesa mingiSocio cultural difference. Labda na wewe ungesema ni mtu wa wapi na mambo yako ni yapi hasa ili tuone nini ilisababisha hayo yaliyokukuta.
Kikubwa ni ku embrace difference zetu na kuendana na mambo. Hizo tabia Tanzania sehemu nyingi zipo zinatofautiana ujazo tu. Kwa maeneo ya mikoa ambayo ni ya mjini inapungua, kwa maeneo ambayo ni ya mipakani na kuna kabila moja la asili lime dominate hayo mambo yanakuwa mengi zaidi.
Mara ya kwanza natembelea Bukoba, japo sikukaa sana lakini nilienda hadi maeneo ya ndani ndani kama vile kata ya Rubafu nikaishi nao fresh tu.
Mambo mengine ni uoga wa asili wa wazawa. Hata Pwani ukiend deepkuna namna watu wanagwaya mgeni ukiingia na kuanza mambo kama ya kutafuta mashamba, biashara n.k
Ni kama hata kwa level ya taifa tunavyoogopa kutoa uraia pacha na kuwapa wageni haki au uhuru wa kununua ardhi n.k Lakini kuna watu kibao tu wamejenga na kununua ardhi kienyeji.
Bugabo wameacha kula binadamu?Mkuu wiki Jana nilikua Rubafu hii ni TARAFA ya Bugabo.... Nimeandika kitu ambacho nimekistudy na kufanya ulinganisho na maeno mengine hapa ni too much mkuu kama ni kwenu Samahani sanaaa Sanaa ila jirekebisheni
Soma wadau wengine wanasemaje kuhusu hili
Nadhani ni kwa sababu ya udongo wa kule na uchafuFunza? Kwa mwaka 2025???? What the hell?
luambo makiadi ni ya kweli haya kuhusu Bukoba?
Tatizo ni hapo kwenye kutumia fursa.Uchambuzi gani huu? Nijiuavyo, Kagera si Bukoba wala si ya wahaya. Kwani wapo wahangaza, wanyambo, wasukuma na makabila mengine. Tatizo lako ni kutumia muda mwingi kutaka kila kitu kiwe kama unavyotaka. Kwa wanaojua ubunifu, unapokuta sehemu fulani inakosa kitu au vitu, hizo ndizo fursa na siyo lawama.
Suala la Ushirikina likoje huko Bukoba?Shida ni kutujua tu. Ukishatuelewa mbona sisi watu poa sana kabisa. Kama hujamfahamu mhaya atakuwa anakukera kila wakati. Wewe unaweza fikiria kuwa anajisifu kumbe mwenzio anaongea kawaida hapo hajaanza kujisifu maana akianza utazimia.
Pia kujichanganya ilikuwa ni changamoto maana unaambiwa kabisa usije kutulete mnyamahanga, yani watu ambao si wahaya ukazaa au kuoa. Lakini mambo yanabadilika. Mimi sijaoa lakini nimeza na mchaga, ndugu zangu wote wameolewa na wachaga na mmoja kaolewa na msukuma, na sidhani kama ntaoa mhaya.
But kiburi na sifa at some point kuna watu huwa wanasema wewe jamaa una kiburi cha wahaya, kitu ambacho mimi sinotice kama ninacho na wala nakuwa sijalenga kuwa na kiburi.
Wekeza kwenye kilimo cha ufugaji kwani chakula huwa hakibaguliwi. Simpo. Anzisha biashara ya kukamata senene watanunua. Pia, jifunze kihaya au jitahidi kuwaonyesha kuwa unawajli na unajitahidi kujifunza lugha yao.Tatizo ni hapo kwenye kutumia fursa.
Uncle wangu alifanikiwa kupata eneo mjini na kufungua Lodge, akaanza kutafuta Wadada wa Kihaya ili kumsaidia kwenye kutoa huduma kwa Wateja....Wale mabinti wakawa wanakatazwa na Wazazi wao kufanya kazi pale kwa sababu ni Lodge ya Mtu wa kuja so walikuwa wanafanya kazi wiki kadhaa wanaondoka...mpaka Mjomba baadae alishindwa kuendesha lodge lakini hatimaye akaagiza mabinti kutoka Dsm, Singida n.k
Wahaya wana dawa za mitishamba nyingi nyingi za kutibu magonjwa lakini ushirikina si kwa kiasi kikubwa kama mikoa mingine. Ni vigumu sana kama umesihi kagera kusikia sijui mambo ya chuma ulete, sijui nini... japo ushirikina pia upo na kuna vijiji zamani vilikuwa vinaogopwa hadi wakazi wa huko walikuwa waogopa kujitambulisha kuwa wanatoka huko. Kuna kijiji kama buzi.Suala la Ushirikina likoje huko Bukoba?
Ukweli mtupu.Kwa mara ya kwanza nafika nilifurahia mazingira mazuri, ukijani mwingi na Hali ya hewa tulivu kabisaaa ikiambatana na mvua hasa nyakati za asubuhi. Baadhi ya Maeneo yana muonekano mzuri wa ziwa hivyo kufanya Mkoa huu kuwa kuwa na view nzuri hasa Kwa wageni.
Kwa kuwa ni mzee wa Fursa Cha kwanza nilichokiona ni UWAZI mkubwa maeneo nikajipa moyo kwamba ardhi ni sehemu ya kwanza ya kuwekeza kama ntabahatika kukaa Kwa muda mrefu.
LAauhala...... Siku mbili tu naanza kupata majuto makubwa na kuchukia Mkoa na watu wake. Twende Wote.
PICHA LINAANZA kutafuta nyumba ya kupanga nyumba zote nazopekekwa ni local vibaya mnooooo zenye ahueni bei haieleweki na ni chache vibaya sanaaa kimsingi kama una hela njoo wekeza kwenye majengo (ila sikushauri ntakwambia kwanini)
BIASHARA ndo kizungumkuti Ile costumer care tulioizoea Kagera (Bukoba) haipo hapa mchoma mahindi anaringa hata Moo hagusi. hakuna karibu hakuna ahsante, kauli nzuri Kwa mteja huku ni ndoto za mchana.
Mbaya zaidi wageni wote walojaribu kufanya BIASHARA wameshindwa kutokana na ukabila ulokubuhu wakija wataongea kihaya usijpojibu kesho usitegee atarudi... ukimuweka MUHAYA watachunguza kujua mwenye BIASHARA wakijua umeumia.
ARDHI.
Eneo kubwa lipo wazi likiwa na migomba hapa naongelea km 5-10 kutoka mjini katikati ila gusa unase kiwanja cha 20*20 Wahaya wanataka million 8 ukibahatisha utakutana na 5 MILIONI nunua kiwanja DODOMA ila sio hapa, hii inasababisha wageni kutonunua ardhi na wengi kununua mikoa ya Mwanza na Geita.. wahaya wanaachwa na ardhi Yao ikiwa na migomba na majivuno Wasijue miaka kadhaa ijayo huenda ikawa Mkoa duni kuliko popote TANZANIA.
UKUAJI WA MJI.
Kwa ujumla Ukuaji wa MJI naupa 5% hakuna ujenzi mpya kabisaa tofauti na ukiingia mikoa kama Mwanza, Geita, Dodoma, ambapo ukipita Kwa mara ya kwanza Tena barabarani tu unavutiwa na majengo mapya mazuri. tofali ya nchi.5 inauzwa 1500 huku bei ya cement ikiwa 24,000. KATORO GEITA na CHATO ambazo ni jirani kabisa tofali inauzwa 1000-1200 mfuko cement ukiwa inauzwa 24,000 pia. anzisha kiwanda sasa 😂 uuze 1200 wakuue.
MAISHA
Nimeshangaa ndizi za Bukoba kuuzwa 3 Kwa 1000 Kwa Baadhi ya Maeneo ya Bukoba MJINI ilihali Dar tunanunua mpaka 6 Kwa 1000. hapa hakuna soko la wakulima AMBAPO utapata vitu Kwa bei RAHISI nyanya tunapima Kwa kilo sio kama kwetu fungu Hadi la 300 lipo..
Maisha ni ya kati sio ghali sana Wala sio RAHISI sanaaa. mzunguko wa pesa ni mdogo Sanaa sanaaaa Kwa kifupi Pesa ni ngumu hapa Bukoba. usafiri ni boda Kwa kiasi kikubwa bajaji ni chache sanaaaa hivyo ukija ujipange kidogo. maeneo ya starehe YAPO kuanzia fukwe za ziwa Victoria, club yetu pendwa (RIO), bunena (my best) nk
MAJUNGU
Sijawahi kuishi sehemu kama hiii narudia SIJAWAHI, Kufuatiliana maisha huku ndo nyumbani, MAKUNDI ya WhatsApp ya MAENDELEO ya Mkoa yamejaa MAJUNGU, kusemana, unafki, ukabila na ubinafsi uliokithiri Kuna kamtu kanaitwa KIMODOI ndo Kigogo wao huku😂😂😂 ndo kanaendesha Mkoa kakisema Kila mtu Hadi Mkuu wa Mkoa anatetemeka kajamaa kanaishi MAREKANI so wadau ndo wanakaabudu kinoma kana MAJUNGU, kanafki, MAKUNDI badala ya kujadili Maendeleo kutwa kucha ni kusema watu voice note kama 1000 zote za MAJUNGU tu sasa usiombe Wahaya wakuchukie 😂😂 ebwanaaa eeeeee kama ni mtumishi maisha Yako yatakua ya shidaaa Kwa kifupi BUKOBA ni ya Wahaya Wageni wote hakuna anaetamani kuwepo hili eneo.
SIASA
😂😂 oya wakuu kama unataka kugomebea hata uenyekiti wa MTAA Na si mzawa huku sio kwako... mikutano ya hadhara ni ya kihaya wegeni tunaduwaa tu... Majungu na Kukwamisha Maendeleo Ili kumfelisha kiongozi Fulani ndo siasa za Kagera (BUKOBA)... mbunge wao BYABATO chamoto anakipata aseee jamaa miradi haetekelezeki Kwa sababu ya CHUKI na uBINAFSI...
Kiongozi mstaafu Yuko tayari kukwamisha mradi ila aliepo asifanikiwe. NI AIBU MAKUNDI yaliyopo Kagera hasa. BUKOBA niaibuuuuu viongozi WA Mkoa wakiongozwa FATMA MWASSA, mbunge NEEMA LUGANGIRA Ndo kabisaaaaa UKISIKIA VITA KISIASA NA FITNA NJOO BUKOBA na sijui CHADEMA Mnafeli wapi.
UTENDAJI WA VIONGOZI
Hapa naongelea Ngazi ya Mkoa mpaka Watendaji wa kijiji.. NGAZI ya Mkoa hakuna kitu Mama MWASSA anajua KUJINUFAISHA tu kupitia wafanyabiashara Kuandaa na kuhudhuria matamasha ya hovyo tu akiambatana na Chawa wake (Kuna naskia kijamaa kinaitwa Mtu Mfupi na KIGOGO wao Kimodoi natamani sana kuwaona hawa)... Mkuu wa Wilaya SIMA na WAKURUGENZI wake ndo kabisaaa miradi ya serikali inajiendeaaa tu Hakuna HATUA zozote zinazochukuliwa Kwa wazembe... ila nashindwa kuwalaumu mana Wahaya wenyewe ni sehemu ya kukwamisha Maendeleo Yao binafsi.
ELIMU
Kizazi Cha Prof TIBAIJUKA kikiisha Kagera itahitaji msaada wa serikali kuinuka Tena. ELIMU hapa ni duni mnoooo mnoooo... majivuno mengiiii ila uhalisia ni sifuri.
HITIMISHO.
Kagera (Bukoba,) sio ya wageni ni Moja ya sehemu za hovyo kuwahi kwenda nimeishi Tabora, Dodoma, Arusha, Tanga, Pwani, Moro, Dar, Mwanza, Shinyanga, Geita, Kilimanjaro na maeneo mengine nimepita ila huu MJI 🙌 hakuna mgeni anaetamani kuwepo hapa UKABILA, MAJUNGU, FITNA, UBINAFSI NA CHUKI vinawaangamiza Wahaya kimya kimya...
Huu ni Mkoa mkongwe sana ilaa MIAKA kadhaaa utakua Mkoa duni kuliko maelezo. BUKOBA ni MANISPAA inayodumazwa na tabia za Wenyeji na ni swala la muda hata Geita ilopewa MANISPAA juzi itaipiku ukiachilia mbali KAHAMA na MANISPAA zingine. inahitajika mabadiliko makubwa sana ya kifikra kuwakomboa Wahaya na Mkoa wao. mabadiliko haya yanahitajika pia kiutawala.
Mwisho RIO DE JENEIRO ni club nzuri mnoo na inapendezesha na kuchangamsha mji ila haiondoi ukweli kwamba sheria zimekiukwa.
WAHAYA SAMAHANINI ILA NI MUUKUBALI UKWELI AU MBAKI NA UKABILA WENU mi naondoka NIMEPACHOKA. KITUO KIFUATACHO BAADA YA MUDA MREFU NARUDI GEITA IKIWA MANISPAA
[emoji1][emoji1][emoji1] wazee wa kuchakata mbususuWarembo vipi wanalika au mpaka uwe muhaya ndio unapewa?
Zote ni kweli na ni za kwetu!!! Tunaishi nazoThibitisha hizo tuhuma.
Wa maruku hawa..Bro walangila ni wenyeji wa bukoba na ukisema mlangila unakuwa unamaanisha jamii ya bukoba ambayo ni loyal family .
Specifically kuniita mlangila ikimaanisha mtu aliyezaliwa katika familia za kichifu mfano akina lwekamwa wote wanajiita walangila sababu ni chimbuko la familia ya kichifu
😀Niko nao hapa dasalamu mzee lkn wanavyo ongea kii iraqw aseeh........
Utasikia tuu gariima, sijui khqaawe ..... surrrua ..... milhaa aani zaidi ya hayo sijui kingine
Ingekuwa kibantu ni rahisi kidogo
Wa iraqw shikamoo nii....