much know
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 11,461
- 17,183
Mwizi sio binadamuIla itamtesa maisha yake yote,kumuua Binadamu sio jambo dogo,itamtafuna maisha yake yote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwizi sio binadamuIla itamtesa maisha yake yote,kumuua Binadamu sio jambo dogo,itamtafuna maisha yake yote.
Anafungwa tena anafungwa mchana kweupe.Hiyo ni kuua bila kukusudia akipata wakili mzuri kesi nyepesi hiyo
Bado haileti justification ya kumpiga namna ile.Ameingia kwenye nyumba kama mwinzi na sio kama Mwanafunzi
Una uhakika gani alikuwa mwizi?Ticha kaua mwizi, alichokosea ni kumpeleka kwa wazazi.. angemtelekeza huko jizi hilo
kwaiyo hapa sheria inamlamba kama kawaidaBado haileti justification ya kumpiga namna ile.
Alitakiwa amfikishe mamlaka husika.
Na usikute hajafika miaka 18 huyo kijana.
Ni nini maana ya kuwekwa jela za watoto!??
Mwizi anathibitishwa na Mahakama baada ya kupitia vivid evidence zote,Mwizi sio binadamu
Inamlamba tena sana.kwaiyo hapa sheria inamlamba kama kawaida
Kwahiyo alimpiga mwizi?Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Igurwa, Adrian Tinchwa (36) kwa tuhuma za kumuua, Phares Buberwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Igurwa.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne Septemba 24, 2024 na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Blasius Chatanda imesema mwalimu huyo ambaye ni mkazi wa Kata ya Kanoni wilayani Karagwe, inadaiwa alimshambulia marehemu kwa kumpiga ngumi kwenye paji la uso na kutumia nondo kumpiga nayo miguuni na mikononi baada ya kumtuhumu kuiba simu yake.
Soma pia: Mwalimu adaiwa kumpiga ngumi mwanafunzi na kumng'oa jino, eti Kisha kapata alama 29 za Hisabati
"Tukio hili lilitokea Septemba 18, 2024 saa 8:00 mchana katika kijiji cha Kanoni Wilaya ya Karagwe, ambapo mtuhumiwa awali mnamo tarehe hiyo saa 3 asubuhi, imedaiwa alifika nyumbani kwake na kukuta kufuli la mlango wa nyumba yake likiwa limevunjwa na alipotaka kuingia ndani alikutana na Phares Buberwa mlangoni akiwa anatoka ndani huku akijaribu kukimbia," amesema.
"Na ndipo mtuhumiwa alimkamata na kuanza kumshambulia hadi kusababisha kupata majeraha makubwa mwilini mwake na baadaye mtuhumiwa alimpeleka hadi nyumbani kwa wazazi wake na kumkabidhi kisha wazazi wake walimpeleka katika Kituo cha Afya cha Rwambaizi kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu," amesema Kamanda Chatanda.
Source: Mwananchi
Duh inasikitishaInamlamba tena sana.
Aombee huyo kijana awe ana miaka 18 kwenda juu.
Kwasababu kitendo cha kumshambulia kwa wingi basi kinaonesha amedhamiria alichofanya.
Kwa nini?Kwa sababu ya kutokuiombea nondo dua njema isimuue mwizi anapompiga nayo?asitoke huyo