Kagera: Mwalimu ampiga mpaka kuua mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyevunja mlango wa nyumba yake ili kuiba simu

Kagera: Mwalimu ampiga mpaka kuua mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyevunja mlango wa nyumba yake ili kuiba simu

Kwenye hili nasimama na ticha, kuna baadhi ya wanafunzi balehe inawapeleka puta, kitendo cha kuvunja kofuli ni wazi alikuwa mjeuri huyo kijana
 
Pole zake kama hakugawa mitaa, ataishi kwenye majengo ya serikali yenye ulinzi mkali kwa miaka yake takribani yote
 
Kwahio in other words Mwalimu alimpiga Mwizi aliyevunja mlango wake ?

Unajua ukiweka Mwalimu kampiga mwanafunzi hadi kumuua inapunguza / inaongeza uzito fulani.....

A lie of Omission is still a Lie....
 
Mwizi anathibitishwa na Mahakama baada ya kupitia vivid evidence zote,
Hata kumwita Mwizi tu ni kosa coz bado haijathibitishwa na Mahakama kua amekua convicted,
Huyo ni mtuhumiwa,Suspect.
Mwizi anathibitishwa na mahakama baada ya kupewa ushahidi na hao wanaomwona kuwa ni mwizi..!!
 
Na Mwalimu angechelewa, labda angemalizwa yeye...tungekuwa tunasema story nyingine saa hizi hapa...
Maelezo yanasema "mwanafunzi alikua anajaribu kukimbia".
Labda kama useme "mwanafunzi alikua anajaribu kumshambulia mwalimu" tungeongea mengine.
Pia inaonekana kijana ni mdokozi tu sio yule mwizi wa kusema ni tishio kiusalama wa uhai ndio maana mwalimu kaweza kumdhibiti na kumtwanga.
Angekua amekubuhu kama vitoto vya Tandale au Manzese si tungekua tunaongea mengine hapa!?
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Igurwa, Adrian Tinchwa (36) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua Phares Buberwa mwananfunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Igurwa

Inadaiwa Mwalimu Adrian alifika nyumbani kwake na kukuta kufuli la mlango wa nyumba yake limevunjwa

Alipoingia ndani alikutana na Mwanafunzi Phares akijaribu kukimbia kisha kumkamata na kumshambulia kwa kumpiga ngumi pamoja na nondo

Phares alipelekwa nyumbani kwao na baadae kupelekwa Kituo cha Afya cha Rwambaizi kwa ajili ya matibabu ambapo alipofariki dunia

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Blasius Chatanda tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024 katika kijiji cha Kanoni Wilaya ya Karagwe saa 8:00 mchana

Kamanda Blasius amedai chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kutoa adhabu iliyopitiliza kwa marehemu hadi kufikia hatua ya kukimbizwa kituo cha afya kwa ajili ya matibabu
Kuna somo hao walimu hufundishwa wakiwa mwaka wapili.

MEASUREMENTS & EVALUATIONS ni muhimu Sanaa otherwise ndio maana yametokea ya kutokea.
 
Back
Top Bottom