Mwalimu wa Shule ya Msingi Igurwa, Adrian Tinchwa (36) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua Phares Buberwa mwananfunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Igurwa
Inadaiwa Mwalimu Adrian alifika nyumbani kwake na kukuta kufuli la mlango wa nyumba yake limevunjwa
Alipoingia ndani alikutana na Mwanafunzi Phares akijaribu kukimbia kisha kumkamata na kumshambulia kwa kumpiga ngumi pamoja na nondo
Phares alipelekwa nyumbani kwao na baadae kupelekwa Kituo cha Afya cha Rwambaizi kwa ajili ya matibabu ambapo alipofariki dunia
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Blasius Chatanda tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024 katika kijiji cha Kanoni Wilaya ya Karagwe saa 8:00 mchana
Kamanda Blasius amedai chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kutoa adhabu iliyopitiliza kwa marehemu hadi kufikia hatua ya kukimbizwa kituo cha afya kwa ajili ya matibabu