Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika tukio zito kama hili la kufariki watoto wadogo 10 maneno ya mkuu wa mkoa ni mepesi sana na kama kwamba kuna mengine ya chini anayakusudia kwa waislamu na shule zao.Kama ni watoto wa kikristo au tukio hili lingetokea Ulaya huenda jeshi la nchi nzima lingehamia huko na kufanya siku za maombolezo kitaifa huku wakihusisha na ugaidi na huenda misikiti ya karibu na masheikh wangehusishwa na watu wasiojulikana wangepata sababu ya kuondoka na wengi.Watoto 10 wamefariki na sita kujeruhiwa vibaya kufuatia moto ulioteketeza bweni la wavulana shule ya Msingi Islamic Byamungu iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera. Hadi sasa chanzo moto huo hakijajulikana.
Watoto waliopoteza maisha ni wa umri wa miaka sita hadi 12.
Taarifa zaidi inakuja...
Wanafunzi 10 wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya bweni la shule yao ya Byamungu English Medium Primary School iliyoko wilayani Kyerwa kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo ambalo chanzo cha moto hakijajulikana
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesitisha shughuli za malazi katika shule hiyo kwa muda.’’ Nachukua hatua nyingine za ziada, hatua ya kwanza na ya awali kabisa tunasitisha huduma za malazi katika shule hii watoto wote waliokuwa wakilala katika huduma ya hosteli au bweni huduma hiyo sasa imesitishwa mbaka itakavyoelekezwa vinginevyo’’, amesema Brigedia Jenerali Marco Gaguti alipotembelea eneo la tukio.
Amesema Sambamba na ameelekeza kamati za usalama za ngazi zote kataika mkoa wa kagera kufanya mapitio upya ya shule zinazotoa malazi, kuhakiki kwamba shule hizo kama zinavyo vibali halali vya serikali na ubora wa majengo yanayotumiwa na wanafunzi, na kuangalia mifumo ya uzimaji moto na kujiokoa inapo.
Amesisitza kuwa kama sifa hizo hazitakua zimekidhi basi hatua zichukuliwe za kufungia huduma hizo katika shule husika.
Awali Mwenyekiti wa kijiji Bw. Munaraka Muhammod aliwaomba watu walioko katibu na Itera wafike kusaidia kuuzima moto huo uliowaka kuanzia jana usiku .
Chanzo za ajali baado hakijajulikana.
Eti hatua ya mwanzo ni kusitisha huduma za malazi shuleni hapo.Hapana jambo la mwanzo ni kuahidi kujua chanzo na kuwatafuta wahusika halafu atoe pesa haraka kujenga mabweni yaliyoungua kwa sababu tunataka kufa na kuungua kwa shule isiwe sababu ya kufungia shule nyengine za kiislamu ambazo huenda kwa unyonge walionao mabweni labda sio kama yale ya shule za kanisa zinazopokea pesa kutoka Marekani na Ulaya.
Kwa sababu ni kipindi cha kampeni za uchaguzi na matukio yamejirudia sana kwenye shule za kiislamu hii pia ingepaswa kuzungumziwa kwenye ajenda za wagombea,kwamba wakiingia madarakani watachunguza sababu za kuungua shule za kiislamu mfululizo.