Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

Kwakweli hii sinema ya Kagoda naipenda sana, ngoja nitafute nafasi nzuri na ninunue na popcorn nione mwisho wake! Je sterling atauwawa? hii siyo sinema ya kihindi sterling hawezi kuuawa kwahiyo tusitegemee RA kuhusishwa na Kagoda hata siku moja labda ikitokea mabadiliko kwenye serikali yetu na hiyo ni 2015 labda!
 
- Hawa watu wanacheza na time tu, lakini wanajua kua haya maneno yao ni uongo wa mchana, wanajaribu kusikia public opinion on it sasa ni vizuri tukaendelea kwuakumbusha kua waache kutupa ujinga ujinga, maana we know better,

- Rostam ndiye aliyesaini mkataba na serikali kwa niaba ya Kagoda, huku Mgonja akisaini kwa niaba ya serikali, baada ya hapo Rostam akaanza kumtumia karani wake mmoja kama co-ordinator betweeen Kagoda na serikali, moto wa Richimonduli ulipowaka akaihamishia hii kitu kwa Manji,

Hapa the only solution ni kuwaomba wabunge walivalie njuga hili ili ipewe kamati maalum ya bunge, lakini kwamba ati watalimaliza hili la Kagoda kwa njia za ujanja ujanja haitatokea kamwe, nina wasi wasi sana kuwa kuna mzito sana kwenye hili la Kagoda maana haiwezekani likawa linayumba yumba hivi, huyo mzito ni nani hasa wa kuwatetemesha hata kina DPP ambao tayari wameshaifkisha mpaka mawaziri wa zamani Kisutu?
 
Nimepenyezewa taarifa kuwa suala la Kagoda AL limekuwa gumu mno kwa DPP. Watu wengi wamekuwa wakimhusha Rostam na Kagoda AL na ushahid pekee ni Wakurugenzi wa Kagoda AL kutumia anwani ya Caspian Cosnstruction Ltd ambayo ni Kampuni ya Rostam Aziz.

Kwa mujibuwa trifa hizo, imeshindikana kabisa kumhusisha Rostam kwa kuwa hakuna sehemu nyingine yoyote ya kumuhusihsa Rostam zaidi ya anwani ya Caspian Construction LTD. Habari zinapasha kuwa Manji ndiye hawezi kukwepa Kashfa ya Kagoda na ameshafuatwa mara nyingi na Makachero na hilo ndilo limesababisha Manji kuugua yale magonjwa ya 'Kuchnganyikiwa' na kutaka kujimaliza.

Kama Kagoda ni ghost/haina mwenyewe si ndo vizuri, serikali itaifishe mali zake. Halafu tuone mlalamiakaji.
 
Ndo raha ya kuwa shemeji mkuu wa nchi kila kitu unakingiwa kifua.
 
hapa serikali inataka kutuchezea mchezo mchafu ambao tulijua utachezwa, swali ni hili uwezi kuwapa watu watumie adress yako kama huna interest nao hata kidogo, huwezi kuwapa watu watumie address yako bila kujua wanafanya biashara gani, hapa ROSTAM anahusika kwa asilimia nyingi tu
tatizo lililokwepo ni kwamba utakapomwaka RA kwenye court ile
 
Wabunge kuibana serikali kuhusu Kagoda, Richmond
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Source: Mwananchi
Date::1/25/2009

BUNGE linatarajiwa kuanza mkutano wake keshokutwa mjini hapa, huku baadhi ya wabunge wakipania kuibana serikali kuhusu suala la Richmond, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Kampuni ya Kupakua Mizigo Bandarini (Ticts).

Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wabunge zinaeleza, ingawa hivi karibuni kamati za bunge zinazohusika zimekaa kujadili, lakini wanadhani bado hawajapata majibu mwafaka kutoka serikalini juu ya kiini cha matatizo yanayokabiliwa kampuni hizo na hatua zilizochukuliwa na serikali.

Wabunge wanataka kusikia kauli ya serikali kuhusu Kampuni ya Makaa ya Mawe ya Kiwira ambayo inahusishwa na familia yas Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Tayari Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema kama serikali itashindwa kuzungumzia suala la Kiwira katika mkutano ujao wabunge wataihoji.

Kamati ya Bunge ya Miundombinu imesema kuwa itawasilisha bungeni ushauri wake kuhusu masuala mbalimbali ambayo kamati hiyo imekutana nayo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohammed Missanga alisema kamati yake itafanya hivyo kwa kufuata utaratibu wa masuala kama hayo bungeni.

"Ni kweli yapo mambo mbalimbali tutakayoyatolea ushauri kwa serikali, tutafanya hivyo kwa utaratibu uliopo wa kawaida," alisema Missanga.

Alisema kuwa hilo halikwepeki kwa kuwa kamati yake ilikuwa ikifanya kazi kwa mujibu wa sheria za bunge kwa manufaa ya Watanzania.

Hata hivyo, alisema kuwa mambo mengine wanayotarajia kuwasilisha bungeni bado si ya kuwekwa hadharani kwa sasa hadi yatakapopata kibali cha bunge.

"Yapo mambo tunawajibika kuwasilisha bungeni kuishauri serikali, lakini kwa sasa siwezi kukuambia. Subiri yaive yatatoka na utasikia," alisema Misanga ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kusini kwa tiketi ya CCM.

Mambo ambayo yapo chini ya kamati hiyo ni Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ambayo ilisimamishwa huduma zake kwa karibu mwezi na kuanza safari zake juzi kwa kusuasua, Kampuni ya Reli (TRL) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Kamati hiyo pia inahusika katika kushughulikia masuala yanayohusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambapo pia imekuwa ikifanyia kazi suala la mgogoro wa mkataba kati ya Kampuni ya Uwakala wa Utoaji Mizigo Bandarini (TICTS) na serikali ulio na utata, huku wabunge wakitaka ama uvunjwe au ufanyiwe marekebisho makubwa.

Pia wabunge wanataka kusikia kauli ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya bunge juu ya zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni tata ya Richmond Development (LLC) mwaka 2006.

Katika bunge lililopita serikali iliahidi kutoa taarifa za utekelezaji wa azimio la bunge lilokuwa limependekeza pamoja na mambo mengine kuwajibishwa kwa watendaji wakuu wa serikali akiwamo, Katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapugi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Kashfa ya Richmond Februari mwaka jana ilisababisha aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Nadini, Nazir Karamagi na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahim Msabaha kujizulu.

Mpaka sasa mmiliki wa kampuni ya Richmond, Naeem Adam Gire, amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuhusika katika wizi wa fedha za serikali.

Vile vile, serikali inatarajia kutoa kauli yake kuhusu uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) linaloendelea kususasua.

Suala lingine ambalo wabunge wamepania kusikia serikali ikilitolea ufafanuzi wa kina ni kuhusu walipo wamiliki wa Kampuni ya Kagoda inayotuhumiwa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania ambao mpaka sasa bado ni kitendawili.

Miswada mingine ambayo inatarajiwa kuwasha moto bungeni ni pamoja na mswada wa sheria ya kurekebisha sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2008, unaotoa mwanya kwa vyama kuungana.

Maswali ambayo wabunge wengi wanajiuliza ni kama serikali inaweza kubadilisha katiba ili kutoa mwanya kwa sheria hiyo mpya, kwa kuwa katiba ya sasa inatambua chama kimoja kimoja.

Mkutano huo unatarajia pia kutoa maazimio kadhaa yakiwapo ya kuridhia itifaki ya kuanzisha Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki na azimio la kuridhia itifaki ya Jumuia ya Afrika Mashariki kuhusu kuanzishwa kwa chombo cha kusimamia usalama na ulinzi wa anga mwaka 2007.
 
Hizo hela zilipelekwa CRDB. Kwa hiyo CRDB wanaweza kutusaida sana katika hili. Kwanza wakati wa kufungua akauti ni lazima wapitie process ya " Know your customer" hapo wanapata details zote za wakurugenzi, aina ya biashara kampuni inafanya nk.Inasemekana kwamba baada ya pesa kuingia kweye akaunti, wale wakurugenzi (makarani wa RA) waliwapa watu wengine "power of attorney" ya kuendesha hizo akaunti. RA angeweza kuwaachia hawa makarani babilioni yote. CRDB waseme ni nani alikuwa akichukuwa pesa kwenye hizi akaunti.
 
Mimi nashindwa kuelewa kama JK kwa RA Hageuzi basi hatuna Rais hapa , JK anachoogopa ni nini kama akifanya kweli na akapata back up ya watanzania nia wote kwenye hilo tuu , RA atatushinda wote kweli ndani ya nchi yetu ?
 
DCI ageuka mbogo kuzungumzia Kagoda

Siku sita baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, kuueleza umma kwamba jalada la Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, liko kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ofisi ya DCI `imeviwakia` vyombo vya habari ikihoji sababu za kufuatilia suala hilo.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu DCI, Samson Kasala, kwa nyakati tofauti jana na Ijumaa ya wiki iliyopita, baada ya Nipashe kumtaka aeleze uchunguzi wa Kagoda ulipofikia tangu jalada hilo lirejeshwe katika ofisi hiyo kama DPP Feleshi alivyosema Alhamisi iliyopita.

Nipashe ilimhoji Kasala, baada ya bosi wake, DCI Robert Manumba, kueleza kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo na kumtaka mwandishi awaulize wasaidizi wake kwa vile yeye yuko likizo.

Baada ya maelekezo hayo ya Manumba, Nipashe iliwasiliana na Naibu DCI, Peter Kivuyo, ambaye alimwelekeza mwandishi awasiliane na Kasala akisema kwamba, ndiye aliyekuwa kwenye Timu ya Rais iliyochunguza upotevu wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na pia, yeye (Kivuyo) Ijumaa wiki iliyopita alikuwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu, mkoani Shinyanga.

Kufuatia maelekezo ya DCI Manumba na Naibu wake, Kivuyo, Ijumaa ya wiki iliyopita Nipashe iliwasiliana na Kasala ambaye alisema kuwa hajui lolote kuhusu jalada la Kagoda kwa vile wakati Manumba anakwenda likizo, hakuwapo ofisini.

Hata hivyo, Kasala alimtaka mwandishi ampe muda hadi Jumatatu wiki hii (jana) ili apate wasaa wa kutafuta jalada hilo akisema kwamba ofisi ya DCI ni kubwa na inahifadhi majalada mengi.

``Naomba usubiri mpaka ni-find out (nilitafute), Jumatatu nipigie,`` alisema Kasala.

Jana (Jumatatu), Nipashe iliwasiliana na Kasala, lakini katika hali ya kushangaza licha ya kukumbushwa kutimiza ahadi yake, Kaimu DCI huyo alibadilika na kumhoji mwandishi sababu za kufuatilia nyaraka za serikali.

``Kwanini unafuatilia nyaraka za serikali?`` alihoji Kasala na alipojibiwa na mwandishi kuwa ni kutokana na suala hilo kugusa maslahi ya umma, alisema: ``Unataka uambiwe yaliyomo kwenye nyaraka za serikali?`` kisha akakata simu.

Kauli hiyo ya Kasala imetolewa siku tano tu baada ya DPP Feleshi kukaririwa na gazeti hili akisema kwamba, ofisi yake ilipokea jalada la Kagoda inayokabiliwa na tuhuma za wizi wa Sh. bilioni 40 kwenye EPA, lakini wamelirejesha kwa DCI kwa uchunguzi zaidi.

Feleshi ambaye alizungumza katika mahojiano maalum na Nipashe alisema kwamba ofisi ya DCI inatakiwa kufanya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kutafuta vielelezo vingine kutoka nje ya nchi kuhusu Kagoda.

Kagoda inadaiwa kujichotea kiasi cha Sh. bilioni 40 za EPA kwa njia ya kifisadi, ikiwa ni miongoni mwa makapuni 22 yaliyojinufaisha na Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika akaunti hiyo katika mwaka wa fedha wa 2005/06 ndani ya BoT.

Hadi sasa, ni watuhumiwa 21 tu wamefikishwa mahakamani kuhusiana na tuhuma za wizi wa fedha hizo, lakini kumekuwa na hisia miongoni mwa jamii kwamba, Kagoda inayoonekana kama muasisi wa wizi wa EPA ikikingiwa kifua na wakubwa kwa sababu zao.

Kauli ya Feleshi ilifuatia kauli ya Wakala wa Serikali wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), kwamba jalada la Kagoda lilipelekwa kwa Timu ya watu watatu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa nia ya kufanyiwa uchunguzi.

Timu hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika.

Wajumbe wengine wa Timu hiyo walikuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.

Awali, Mwanyika alilieleza Nipashe kwamba, hajui lolote kuhusu Kagoda kwani walikwisha kukabidhi ripoti yao kwa Rais na kwamba vyombo vya serikali viulizwe juu ya kampuni hiyo.

Hivi karibuni Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe alikaririwa akisema kwamba, serikali haiwezi kuipeleka mahakamani Kagoda kwa maelezo kwamba, haijapata ushahidi wa kufanya hivyo na kumtaka mtu yeyote mwenye ushahidi aupeleke.

SOURCE: Nipashe
 
Kama Kagoda ni ghost/haina mwenyewe si ndo vizuri, serikali itaifishe mali zake. Halafu tuone mlalamiakaji.

Mali gani? ushasema ghost maana yake haipo, haina ofisi, anuani feki, kwa hiyo mali hawana imeanzishwa kuchota wakachota wakaishia na wapo wanatesa na hakuna wa kuwagusa, haoooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hizo hela zilipelekwa CRDB. Kwa hiyo CRDB wanaweza kutusaida sana katika hili. Kwanza wakati wa kufungua akauti ni lazima wapitie process ya " Know your customer" hapo wanapata details zote za wakurugenzi, aina ya biashara kampuni inafanya nk.Inasemekana kwamba baada ya pesa kuingia kweye akaunti, wale wakurugenzi (makarani wa RA) waliwapa watu wengine "power of attorney" ya kuendesha hizo akaunti. RA angeweza kuwaachia hawa makarani babilioni yote. CRDB waseme ni nani alikuwa akichukuwa pesa kwenye hizi akaunti.

Inasemekana hizo documents zilizotumiwa kufungua akaunti CRDB na zile hundi zillizotumika kuwalipa hao Mafisadi hazipo! CEO wa benki ya CRDB Dr. Kimei anatakiwa ichukuliwe hatua na BoT kwa kuruhusu pesa chafu zipitie kwenye Benki yake.
 
Salaam!

toleola24.jpg

Mengine yaliyomo.. ni wewe kugundua...

Kupata nakala yako kila wiki kwa barua pepe fuata maelekezo ukurasa wa mwisho wa kijarida. Kuwa wa kwanza kujua, na wende nawe ukawe "Cheche"!
 
Attachments

DCI ageuka mbogo kuzungumzia Kagoda

2009-01-27 10:22:43

Na Muhibu Said

Siku sita baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, kuueleza umma kwamba jalada la Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, liko kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ofisi ya DCI `imeviwakia` vyombo vya habari ikihoji sababu za kufuatilia suala hilo.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu DCI, Samson Kasala, kwa nyakati tofauti jana na Ijumaa ya wiki iliyopita, baada ya Nipashe kumtaka aeleze uchunguzi wa Kagoda ulipofikia tangu jalada hilo lirejeshwe katika ofisi hiyo kama DPP Feleshi alivyosema Alhamisi iliyopita.

Nipashe ilimhoji Kasala, baada ya bosi wake, DCI Robert Manumba, kueleza kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo na kumtaka mwandishi awaulize wasaidizi wake kwa vile yeye yuko likizo.

Baada ya maelekezo hayo ya Manumba, Nipashe iliwasiliana na Naibu DCI, Peter Kivuyo, ambaye alimwelekeza mwandishi awasiliane na Kasala akisema kwamba, ndiye aliyekuwa kwenye Timu ya Rais iliyochunguza upotevu wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na pia, yeye (Kivuyo) Ijumaa wiki iliyopita alikuwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu, mkoani Shinyanga.

Kufuatia maelekezo ya DCI Manumba na Naibu wake, Kivuyo, Ijumaa ya wiki iliyopita Nipashe iliwasiliana na Kasala ambaye alisema kuwa hajui lolote kuhusu jalada la Kagoda kwa vile wakati Manumba anakwenda likizo, hakuwapo ofisini.

Hata hivyo, Kasala alimtaka mwandishi ampe muda hadi Jumatatu wiki hii (jana) ili apate wasaa wa kutafuta jalada hilo akisema kwamba ofisi ya DCI ni kubwa na inahifadhi majalada mengi.

``Naomba usubiri mpaka ni-find out (nilitafute), Jumatatu nipigie,`` alisema Kasala.

Jana (Jumatatu), Nipashe iliwasiliana na Kasala, lakini katika hali ya kushangaza licha ya kukumbushwa kutimiza ahadi yake, Kaimu DCI huyo alibadilika na kumhoji mwandishi sababu za kufuatilia nyaraka za serikali.

``Kwanini unafuatilia nyaraka za serikali?`` alihoji Kasala na alipojibiwa na mwandishi kuwa ni kutokana na suala hilo kugusa maslahi ya umma, alisema: ``Unataka uambiwe yaliyomo kwenye nyaraka za serikali?`` kisha akakata simu.

Kauli hiyo ya Kasala imetolewa siku tano tu baada ya DPP Feleshi kukaririwa na gazeti hili akisema kwamba, ofisi yake ilipokea jalada la Kagoda inayokabiliwa na tuhuma za wizi wa Sh. bilioni 40 kwenye EPA, lakini wamelirejesha kwa DCI kwa uchunguzi zaidi.

Feleshi ambaye alizungumza katika mahojiano maalum na Nipashe alisema kwamba ofisi ya DCI inatakiwa kufanya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kutafuta vielelezo vingine kutoka nje ya nchi kuhusu Kagoda.

Kagoda inadaiwa kujichotea kiasi cha Sh. bilioni 40 za EPA kwa njia ya kifisadi, ikiwa ni miongoni mwa makapuni 22 yaliyojinufaisha na Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika akaunti hiyo katika mwaka wa fedha wa 2005/06 ndani ya BoT.

Hadi sasa, ni watuhumiwa 21 tu wamefikishwa mahakamani kuhusiana na tuhuma za wizi wa fedha hizo, lakini kumekuwa na hisia miongoni mwa jamii kwamba, Kagoda inayoonekana kama muasisi wa wizi wa EPA ikikingiwa kifua na wakubwa kwa sababu zao.

Kauli ya Feleshi ilifuatia kauli ya Wakala wa Serikali wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), kwamba jalada la Kagoda lilipelekwa kwa Timu ya watu watatu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa nia ya kufanyiwa uchunguzi.

Timu hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika.

Wajumbe wengine wa Timu hiyo walikuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.

Awali, Mwanyika alilieleza Nipashe kwamba, hajui lolote kuhusu Kagoda kwani walikwisha kukabidhi ripoti yao kwa Rais na kwamba vyombo vya serikali viulizwe juu ya kampuni hiyo.

Hivi karibuni Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe alikaririwa akisema kwamba, serikali haiwezi kuipeleka mahakamani Kagoda kwa maelezo kwamba, haijapata ushahidi wa kufanya hivyo na kumtaka mtu yeyote mwenye ushahidi aupeleke.

SOURCE: Nipashe
 
Inasemekana hizo documents zilizotumiwa kufungua akaunti CRDB na zile hundi zillizotumika kuwalipa hao Mafisadi hazipo! CEO wa benki ya CRDB Dr. Kimei anatakiwa ichukuliwe hatua na BoT kwa kuruhusu pesa chafu zipitie kwenye Benki yake.

Dr. Kimei angeweza kuchukuliwa hatua na Bank Kuu kama angekuwa hajafuata maelekezo/ushauri kutoka Bank Kuu (BoT). Katika hatua zote za kiBank, BoT ilihakikishia Bank husika kuwa pesa zile zilikuwa halali. Na hapo ndipo anapoponea Dr. Kimei
 
atawaka sana mwaka huu kama ana pressure ni bora ajiuzulu tu maana kizazi hiki ni cha nyoka hakiogopi mtu yeyote ati
 
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), bado kimeng’ang’ania kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishiriki katika ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Akauti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika amesema hatua ya serikali ya kushindwa kumfikisha mahakamani mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, iliyochota zaidi ya Sh. 40 za EPA kunaitia doa serikali.

“Hapa kuna ‘utatu usio mtakatifu’ kati ya CCM, Kagoda na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz. Hili ndilo linasababisha kampuni ya Kagoda kushindwa kufikishwa mahakamani,” anasema Mnyika.

Mnyika, mwanasiasa kijana na jasiri, anasema kwamba chama chake bado kinaamini kwamba CCM ilihusika na uchotaji fedha ndani ya BoT.

“Sisi bado tunasisitiza kwamba Kagoda ni mali ya Rostam,” anasema Mnyika katika mahojiano yake yaliyochapishwa na gazeti hili. Gazeti la MwanaHALISI

Akizungumzia tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wa Chadema wana mahusiano na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, Mnyika anasema “huo ni sehemu ya mkakati wa CCM kukichafua Chadema.”

Anasema, “Tunaamini kwamba wanaotutuhumu wanatumiwa na wapinzani wetu wa kisiasa. Tunafahamu mahusiano ya karibu yaliyopo kati ya baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi na viongozi wa CCM.”

“Nani asiyejua kuwa Ismail Jusa Ladhu (Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), aliyetuhumu viongozi wa Chadema, ana uhusiano wa karibu na Rostam Aziz?

Jusa aliwahi kusema hivi karibuni kwamba mbunge wa Viti Maalum, Grace Kiwelu, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Mkurugenzi wa Fedha Athony Komu, wana uhusiano na watuhumiwa wa ufisadi.

Anasema Chadema haijihangaishi kujibu kauli za Jusa. Inajua kuwa hizo ni kauli za Rostam Aziz ambaye ni mshirika wake na Rostam ni mmoja wa watuhumiwa wakuu.

“Chadema ingejibu kauli hizo kama zingekuwa zimetolewa na Kiongozi wa Upinzani bungeni Hamad Rashid, au Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba au Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad.

Anasema wanapata nguvu zaidi kutokana na mahojiano ya Jusa kuchapishwa katika gazeti la Rai wiki mbili zilizopita. Gazeti hilo linamilikiwa na Rostam.

Hata hivyo, Mnyika anakiri kwamba Kiwelu na Komu wana uhusiano wa kifamilia na Esther Komu ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa wizi wa fedha BoT.

Anasema pia kwamba Zitto ana uhusiano wa karibu na kiongozi wa CCM, Rajabu Maranda, ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa katika kesi hiyohiyo.

Kuhusu matumizi ya fedha kutoka nchi za nje, Mnyika anasema siyo sahihi kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao za kila siku kwa fedha kutoka nje.

“Chadema hakipokei fedha kutoka nje kwa ajili ya kujiendesha. Chama chetu kinaendeshwa kwa ruzuku ya serikali na michango ya wanachama,” amesisitiza.

Anasema, hata hivyo, kuwa wanachama na viongozi ndio wachangiaji wakuu wa chama na kwamba wabunge wa Chadema wamekuwa wanachanga fedha kila mwezi kutoka kwenye mishahara yao ili kuendesha chama.

“Fedha tunazopata kutoka nje, tunazitumia kwa mafunzo ya viongozi wa ngazi mbalimbali. Haziwezi kuendesha shughuli za kila siku za chama. Kwanza, ni kidogo, lakini pia siyo sera ya Chadema wala wale wanaozitoa,” anafafanua.
 
Back
Top Bottom