Pre GE2025 Kahama: Paul Makonda ataka Caroline apewe eneo la Serikali, Mkurugenzi asema kumiliki Ardhi ni jambo la kisheria sio siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Labda angesema inaongoza kwa Wilaya ambazo hazipo mwenye Majiji
 
Nakupongeza kwa majibu yenye utafiti.
Hata kama huyo Mkurugenzi wa Kahama anasingiwa ni vema akabadilishiwa kituo cha kazi kwa ajili ya heshima ya CCM.
Hata hivyo,nasikia huyo Mkurugenzi ni mjanja sana.Akipata tuhuma za aina hii huwa anahonga watu fulani wanaohusika ili asiondoke hapo.Si ajabu hata mleta mada amepitiwa na maokoto ya huyo kiongozi.
 
Nasikia kwa kazi nzuri na Uadilifu wake Full Council imekuwa ikisita kuacha jamaa aondolewe ili Kahama iwe Mkoa
 
Kwani hilo eneo unalitaka wewe? Kwani Serikali ikiamua kumpa ardhi mwananchi wake ni kosa? Wewe ungepewa ungelikataa!!

Haya turudi kwenye hoja kwamba wewe hilo sakata unalijua vizuri. Kwanini hukujitokeza kulitolea ufafanuzi!?

Hujajipanga bwashee, amekutuma Mkurugenzi lakini hujaliwasilisha vizuri. Utamuharibia kazi
 
Akili yako haina akili,

1. Kama ametumwa kwanini amuharibie kazi aliyemtuma wakati aliyemtuma kwamantiki yako ndio in yeye aliyeandika?

2. Kwani kunasehemu mleta mada kasema Mkurugenzi asichukuliwe hatua ikibainika ni kweli kafanya makosa?

3. Mleta mada ametoa dukuduku lake na katoa rejea tatizo liko wapi hapo au rejea zimetoa taarifa tofauti?

4. Nadhani mleta mada anania nzuri ya kutaka mwenezi aongeze umakini katika ziara zake.

5. Mleta mada pia anataka Mkurugenzi anayetetea mali ya Umma awe credited sio yule mama tapeli,
 
1.Mkurugenzi yuko sahihi 100%

2. Makonda ajaribu kufanya tathmin kabla ya kulaumu

3. Kama mahakama imeamua Mkurugenzi hana say hapo
 
Mkurugenzi Usikate tamaa komaa mwanangu hii nchi Wakurugenzi wengi hawana muda na mali za umma,

Hapo ungeamua kushirikiana na huyo mwanamke uaingekosa hata hekta 3 za kwako,

Komaa uzalendo unalipa sana hapo baadae.
 

Aisee..Shukrani sana
 
Hiyo ni kawaida ya mahakama za Kangaroo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…