Uchaguzi 2020 Kahama: Polisi wapiga mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliojaa nje ya hotel aliyofikia Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Kahama: Polisi wapiga mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliojaa nje ya hotel aliyofikia Tundu Lissu

Violence Alert Tanzania Election

"Tunapigwa mabomu nje ya hotel ya Gaprena Kahama, kwasababu watu wamesindikiza gari na hawataki KUONDOKA"

Inadaiwa Mtu mmoja amepigwa mguuni na risasi ya moto.

Aliyepigwa risasi alikuwa mpita njia, anafahamika kwa jina la Kiwasha Masele.. Anapelekwa Hospitalini

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene ameandika hivi; Very sad! Polisi Kahama, wanatumia silaha, yakiwemo mabomu kuwatawanya wananchi wa mji huo waliokuwa wanamsindikiza kwa amani Mgombea Urais wa JMT wa CHADEMA Mhe. Tundu Lissu kwenda hotelini baada ya mkutano wa kampeni alioutumia kuwasalimia maelfu ya wanaKahama!
Kumbe polisi ni adui namba 1 wa haki na utu
 
Kundi la watu wengi usiku siyo zuri maana wote hawana nia moja , lakini madhara ya haya mabomu yanayopigwa yanaweza kuleta usugu kwa raia na wasiyaogope tena.
 
Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ndiyo adui mkubwa wa hawa mafisiem na wao wanajua hivyo na ndiyo sababu wanavihofia sana na hawataki hata kuvisikia.
Ndio suluhisho...KATIBA MPYA
 
Tatizo viongozi wetu wa chadema hamtaki kutii sheria..matokeo yake mnatuingiza sisi kwenye matatizo ya kupigwa na kuumizwa kwa ajili yenu.....hii si haki bali ni kutuburuza.
 
Geita hawakupiga mabomu,nimeskia RPC ameondolewa na kupelekwa chuo cha polisi ili ajifunze tena kazi.Pia OCD naye kang'olewa.

Waengine wanatetea unga wao,usione hivi.
Mkuu huyo jamaa hafai alitushambulia tukakimbilia ofisi za ccm kalangalala bado akatufuata huko, kijana wetu mmoja walimngoa meno,
 
Shida ya wanasiasa wetu wanatengeneza mazingira ya crowd bila ulazima wa kufanya hivyo.. Yanapotokea Maafa lawama ni kwa serikali, Acheni hizo bana...

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Tunawapa lawama polisiccm kwa sababu kuna ushahidi wa kutosha tu wa matendo yao maovu kwa Chadema kwa miaka chungu nzima sasa.
Lakini hili pia limefanyika kwa usalama wa mgombe sababu humjui mbaya nan ktk huo mkusanyiko, ndugu zangu vitu vingine tunawapa lawama polisi sijui kwa kutokujua nn tunafanya au la!
 
Mkuu tunapaswa kukwepa mitego ya polisi ili wasipate sababu ya kufanya hayo waliyoyafanya vinginevyo sisi ndio tutakua tunawalazimisha wafanye ivyo.
 
Wananchi wakisimama kidete tarehe 28 October CCM inaangukia pua!
 
..WHY?

..Hao watu usiku ukizidi kuingia wataondoka wenyewe.

..Polisi wetu hawana akili kabisa.
Haya mnayataka wenyewe, mipango yenu yote inafahamika. Wahenga walisema ''serikali ina mkono mrefu'' nyie mnafikiria hao mashoga watawasaidia kuleta machafuko.
 
Lissu kwenye kampeni zake kishatembea mikoa mingi Nchini na pamoja na kwamba kulikuwa na umati mkubwa wa watu hakukuwahi kutokea maafa popote pale na leo watu walikuwa na furaha tele za kuwa na kipindi chao hivyo hakukuwa na sababu zozote za polisiccm kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi ili tu kuanzisha vurumai.
Shida ya wanasiasa wetu wanatengeneza mazingira ya crowd bila ulazima wa kufanya hivyo.. Yanapotokea Maafa lawama ni kwa serikali, Acheni hizo bana...

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom