Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
===
Kwanza, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya TZS 12.6BL kujenga kilometa 12.6 za Lami kuzunguka eneo la Viwanda la UMMY MWALIMU Yaani "Ummy Mwalimu Industral Park " ikiwa ni pamoja na mitaro yake pamoja na taa za barabarani,
Pili, Rais Samia Suluhu Hassan atajenga Stendi ya kisasa ya mabasi kwenye eneo hili la uwekezaji pamoja na soko la kisasa ambalo litabeba wamachinga wote wakiwemo Mamalishe,
Tatu,Rais Samia pia anajenga Stendi kuu ya mabasi ya Mbulu,mtakumbuka Kahama inatoa mabasi zaidi ya 50 ya mikoani kwa kila siku hakika hakuna kama Rais Samia Suluhu Hassan,
Nne, Rais anajenga pia Soko la Sango litakalochukua wajasiriamali zaidi ya 1,200 kwa mkupuo kiasi ambacho wanakahama wanatamani Rais Samia Suluhu asinga'tuke madarakani,
Tano, Sihivyo tu,Rais Samia Suluhu Hassan pia ametoa TZS 10.5BL kwaajili ya Ujenzi wa barabara za Mjini kilometa 10.5 pamoja na mitaro yake pamoja na taa za Barabarani .