MOJA YA CHANGAMOTO ILIYOKUWA INALIKUMBA ENEO HILI NI MAJI SASA MAMBO NI MOTO WAMEUNGANISHA MAKAMBAKO RUJEWA NA WANGINGOMBE πππππMradi huo unaogharimu kiasi cha Dola Milion 20,379,000.58 ambazo sawa na Shilingi 50, 927,124,011.00. Mradi unatajia kuzalisha maji kiasi cha lita za ujazo 41,000,000 kwa siku. Hata hivyo Eng. Lestus Linda ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Rujewa (RUJUWASA) amesema mradi huo unategema kunufaisha Mji wa Rujewa, Kata ya Ubaruku, Imalilo-songwe na Igava. Pia Mji wa Wanging'ombe na Makambako ni miongoni mwa wanaufaika wa program hiyo.
Mradi huo unatekelezwa kupitia Mkandarasi M/S Larsen and Toubro Kampun
i ya India chini ya Mshauri WAPCOS wa India. Mradi unategemea kukamilika mwaka 2025 ikiwa ni muda wa awali wa mkataba. Mradi huu ni kazi kubwa anayoendelea kuifanya Raisi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuhakikisha changamoto za maji zinapungua kwa kiasi kikubwa.
#NasimamanaRaisimheshimiwaDaktSamiaSuluhuHassan