Sema Watu wengi mnapicha tofauti sana ya Kahama! Kinachoikuza Kahama si Madini.. japo yameipa umaarufu mkubwa.
Kinachoikuza Kahama ni Kilimo tena.. Mchele. 🙂 Na Biashara. Kama imekuwa soko tangu miaka hiyoooo.. Watu wanafuata mitumba na wakati wa magendo kwa sababu ya kuwa strategically located.
Tangu mtikisiko wa kiuchumi uanze ujumlishe na Corona juu Kahama imeendelea kukua.. Na sasa inajipanga Kuwa Manispaa. Wale washavuka mji wa kukua ama kufa kwa kutegemea mitikisiko ya kiuchumi..
Kingine tunachokosea ni namna tunayoipima miji hii.. per capita ya mkoa haimaanishi fedha hiyo inatumika Njombe.. ila inapatikana kupitia Njombe. Cha kupima ni matumizi.. kiasi gani kinatumika ndani ya njombe!? Kinahama mikono ndani ya njombe!?
Kwa mzunguko mkubwa wa fedha ni dalili sehemu tajwa ni kubwa.. sasa kwa ukubwa siwezi kulinganisha Njombe na Kahama.. Kahama is almost double the size ya Njombe.. kwa mzunguko wa kifedha sidhani kama Tunapaswa kuliangalia.. kwa kanda ya ziwa Kahama iko nyuma ya Kwanza tuu.. kwa kupitia njia ya kati mpaka dsm inazidiwa na Dodoma, Morogoro na DSM pekee.. 🙂
Kahama per capita lazima iwe ndogo unapokuwa umezungukwa na wilaya za Ushetu, Msalala, Kishapu, Shinyanga Vijijini zenye mapato ghafi kidooogo sana.. huku mzalishaji mkubwa akiwa Kahama TC na Shinyanga MC pekee.