Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Kumbe ndo mana Mkuu alikuita Njaa wewe....nikisoma na matangopori yako uliyokuwa unaandika mwaka 2014 juu ya hili sakata napata jibu.
Sasa ushasema kuwa sababu ni kuwazuia wasitoroke chini ya ulinzi alafu unatoa hoja zako nyepesi za utetezi za unene na uzee.
Utajiri kwa fedha haramu haujawahi kumuacha mtu salama maisha yake yote hapa duniani.
 
Kukomoa, kudhalilisha, kukashifu, ndio aina mpya ya utawala wetu kwa sasa, haya mambo aliyaanza bashite na anayaendeleza sana hamkemei ila kwa sababu kalasinga kashindwa kuchuchumaa ndio mmeamua kusema?! Wale walemavu waliburuzwa barabarani, walinyanyuliwa kama chura wala haikukemewa, kweli pesa ina nguvu ya shetani.
 
Mimi jana nilipoona hiki kitu kiliniuma sana, lakini kwasababu sizijui vizuri sheria niliogopa kuhoji kama ni halali kuanza kuwatesa watuhumiwa hawa wasio hata na uwezo wa kukimbia pale walipokuwepo. Alafu kibaya zaidi unayemshauri abadirishe hicho kitabia cha unyanyasaji wa watuhumiwa bado anakaimu nafasi yake ili athibitishwe lazima Rais afurahi, sote tunafahamu ili umfurahishe Rais aina ya Magufuli unatakiwa uwe mtu wa tabia gani
 
Mm natamani hata wachapwe risasi na familia zao hiyo ndiyo itakuwa hukumu stahiki hao siyo viumbe ni mashetani kabisa wakiukumiwa kunyongwa ndo nitamuunga mkono magufuli
 
Ni kweli kabisa hawa jamaa wanastahili 'fair trial'. Hata hivyo, kwa wizi wa IPTL wa wazi mchana kweupe na dharau ya kuwahonga viongozi wetu mapesa kana kwamba wanagawa njugu, napata shida sana kuwaonea huruma hawa jamaa.

Banafsi naamini wanaweza wakachomoka kutokana na mambo ya IPTL na viongozi wa awamu zilizopita ya sasa kuwa kama yai na kuku. Wakishinda, basi ushindi utakuwa wao na viongozi wabadhirifu. Sisi wananchi itakuwa ni maumivu tu. Sasa walau na sisi wanyonge tupate 'Poetic Justice' kupitia kudhalilika kwa hawa jamaa kwa kupigwa picha nyingi mpaka wajukuu wao wajue babu zao ni wezi na kwa kuendelea kumaliza haja kwenye ndoo mpaka Julai 3 au pale mahakama itakapoamua vinginevyo.
 
Huu ni unafiki tu NAZANI kuna kitu nyuma yenu hayo mambo yanafanyika ktk mahakama zote tu..Leo mmekula Pesa zao mnaanza kuwatetea ooh wamedhalilishwa daaah!jiandaeni kisaikolojia tu na kuwapelekea chai
 
sio mwanasheria ila nilipita jkt. navyojua ziko kanuni zinamuhusu mtuhumiwa. ukiwa chini ya ulinzi kama mtuhumiwa hauko huru unakua umekamatwa. ndio maana unawekwa pingu askari lazima awe amekutia mkononi. unaweza kupigishwa magoti. kwa ufupi askari anakudhibiti usitoroke. inafanyika hivyo kwa watuhumiwa wote hua tunaona. sasa hawa watuhumiwa wawili matajiri wanashutuma za utapeli wa kimataifa uliyoletea nchi hasara kubwa na watu wengi wana hasira nao. kwa nini paskali unaona watendewe tofauti. tena hawa ndio hatari wanaweza kutoraka kiajabu polisi lazima wawe macho kodo.
 
@Pascal Mayalla msomi wa sheria na mwandishi wa habari. Natumai pia ulipiga kelele pale Godbless Lema alipokuwa anapigwa ping pong mahakamani na akasotea dhamana yake kwa miezi minne. La sivyo, itakuwa ni yale ya matajiri kuonewa huruma kwa kisingizio cha sheria na maskini kukandamizwa bila kujali sheria.
 
Harafu huyo singasinga alikamatiwa airport alikua anasepa.
 
Pachal bana. Sasa hapo udhalilishaji ni UPI? Maana tangu Jana unahangaika kufanya research mpaka kwa classmates wako wa sheria hapo Mlimani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…