Kwani hujui wanaowavisha matairi wezi wanavunja sheria? Wakishawachoma moto wezi ulishawahi kuona kuna mtu anabaki hapo? Wote ukimbia na kimwacha mwizi akiungua kwa sababu wanajua walichofanya ni kinyume cha sheria.wezi wa kuku mwenye thamani ya 10000 anavishwa tairi hawa wa mabilioni unataka tuwapetipeto?
Ndani ya vyumba vya mahakama za Uingereza, India na Afrika Kusini, watuhumiwa hawaruhusiwi kupigwa picha wakiwa ndani ya vyumba vya mahakama, au mikononi mwa polisi. Kama sisi tumerithi sheria za Uingereza, kwa nini tuende kinyume cha wenzetu, unless kwa kufanya hivyo, ndio maendeleo yenyewe!.
Unaweza ikawa ni mazoea lakini siyo sheria. Ni kweli hayo uliyosema yanafanyika sana.Mbona huo ni utaratibu wa kawaida pale mahakamani. Mtuhumiwa akitoka ndani ya Mahakama wakati anasubiri karandinga anatakiwa kuchuchumaa ili asikimbie. Huu utaratibu umekuwepo kwa muda tu. Nashangaa leo kuna watu mnajitoa fahamu! Au kwa kuwa ni Singasinga na Ruge!? Inapelekea kuamini kwamba Bwana Pascal Mayalla umeshachukua bahasha kutoka huko kunako "Dude".
Umesahau ya kwamba Yona na Mramba nao walichutama wakati wanasubiri karandinga!?
Kwaiyo ibara 13 ya mwaka 1977 imeonekana baada ya singasinga na ruge kupigishwa magoti? Mngeenza na wanyonge kwanza ambao ata kuweka mawakili tatizoNakubaliana na mtoa mada, kosa ni kosa haijalishi kafanyiwa nan iwe Kina TID na wenzie au Rugemarila na mwenzie, ni kinyume cha utaratibu wa sheria na taratibu ambazo tunazifata kama nchi, ukiangalia Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inakataa vitendo vya udhalilishaji kama hivi..Tukiendelea kunyamaza ni kulea kosa
Una uhakika na ulichoandika! Uhuru wa mawazo hauna maana kuandika uzushi!Huu ni unafiki tu NAZANI kuna kitu nyuma yenu hayo mambo yanafanyika ktk mahakama zote tu..Leo mmekula Pesa zao mnaanza kuwatetea ooh wamedhalilishwa daaah!jiandaeni kisaikolojia tu na kuwapelekea chai
Huyu jamaa singa kupiga goti udhalilishaji??? na wale watuhumiwa wengine mbona hajawahi andika??Double standard... gazeti lefu kisa singa singa kapigishwa magoti na bado!!!!
Wanadhalilishwa kina mnyika bungeni umenyamaza hili la jana ndo linakumiza...
Na ndio maana nikasema ni "Utaratibu" mkuu. Not necessarily iwe sheria. Kuna mambo mengi hapa Tanzania tunafanya kwa Taratibu na sio sheria....ikiwemo hilo la kuchutama nje ya Mahakama wakati unasubiri karandinga. Au unapovuliwa viatu na mkanda wakati unashikiliwa katika kituo cha Polisi.Uniweza ikawa ni mazoea lakini siyo sheria. Ni kweli hayo uliyosema yanafanyika sana.
Safi kabisa kaka, mwambie Pascal Mayalla, huku mtaani boda boda wanachapwa fimbo na magogo, mwizi wa ndoo na sufuria ni kasheshe (hapo wana bahati kama hawajauawa), ila hatujoana zikiletwa kwenye bodi, kama sio unafiki nini nini?!wezi wa kuku wakidhalillishwa sawa tu ila kwa rugemalila ni udhalilishaji nyie wabongo kwa kujipendekeza ni mabingwa
Wanabodi,.
Ni sahihi kabisa mkuu. Kuna gazeti moja la leo jina limenitoka, limeandika Mtuhumiwa mmoja kati ya hao wahujumu amekamatwa akiwa Uwanja wa Ndege akiondoka nchini.sio mwanasheria ila nilipita jkt. navyojua ziko kanuni zinamuhusu mtuhumiwa. ukiwa chini ya ulinzi kama mtuhumiwa hauko huru unakua umekamatwa. ndio maana unawekwa pingu askari lazima awe amekutia mkononi. unaweza kupigishwa magoti. kwa ufupi askari anakudhibiti usitoroke. inafanyika hivyo kwa watuhumiwa wote hua tunaona. sasa hawa watuhumiwa wawili matajiri wanashutuma za utapeli wa kimataifa uliyoletea nchi hasara kubwa na watu wengi wana hasira nao. kwa nini paskali unaona watendewe tofauti. tena hawa ndio hatari wanaweza kutoraka kiajabu polisi lazima wawe macho kodo.