Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari

Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari

Sijui kama mna uelewa sahihi ninyi, ashasema bajeti ni ndogo na ilitengewa watu wa Zanzibar sio watu milioni sitini wa Tanzania yote
Ninyi Machogo uelewa wenu mdogo sio?
 
Common sense is not so common!
Hizi ni nyakati za kuwaunganisha watanzania zaidi na zaidi.
Kauli za utengano ni mbaya kuliko vitendo.
Tanzania ni nchi moja 97% ikiwa ni Tanganyika (Bara).
Wenye akili washauri pande zote za muungano zitumie kauli na matendo ya hekima na busara.
Kwani lazima tuwe na Zanzibar? Sasa kwa mfano mimi Zanzibar inanisaidia nini? Eti tunu. Kuna upuuzi Nyerere alirithisha vitoto vyake alivyoongoza kama vifaranga unatugharimu mpaka leo. Mimi nikiwa Rais asubuhi basi jioni hilo limiungano limeshajifia maana halitusaidii chochote.
 
Xenophobia ilianza kupitia hisia za Wazanzibari sasa zinageuka rasmi kwa kasi kuwa matendo. Upendeleo unaofanyika hivi sasa wa kugawa sawa kwa sawa wa rasilimali za nchi ndio unaowapa kiburi.

Wananufaika sana na uchache wao kulinganisha na wingi wa Watanganyika, na hivyo kuanza kuwadharau wazi wazi na hata kuthubutu kumuita kiongozi mkuu kimamlaka wa Kitanganyika Yuda msaliti.
Acha aitwe Yuda maana hayajitambui. Matanganyika yote yaliyopo serikalini ni kama kondoo tu wanapelekwa na mchungaji wao.
 
Kama kuna vitu Nyerere alichemka ni Muungano na ujamaa. Alichemka sana Mzee wetu hapo.
Nyerere sio wakulaumiwa yeye alifanya vile kwa wakati hule na mazingira yaliyokuwepo, hapa wakulaumiwa ni hao wanajiita wasomi uchwara kushindwa kutengua taurati..kama waliona kuna makosa kwanini mpaka leo yanakumbatiwa..Babu alituachia aliyaacha nchi mikononi mwetu tena ikiwa salama..Wakulaumiwa ni sisi tena hasa Hao wanaojiita wasomi.
 
Sisi Watanganyika ndie mabunyenye wacha tupigwe tu
Wazanzibari kina Jagina nawaunga mkono kwenye jambo moja tu ili wanalo semaga misikitini kuwa 👉 kichaa wa Zanzibar ni zaidi ya Shekh wa bara na nguruwe wa Zanzibar ni zaidi ya muhumini wa bara😁😁😁😁😁
 
Dini yangu ndio muhimu zaidi , na dini yangu inafundisha niwe mzalendo wa nchi yangu pia nitende haki na uadilifu kwa watu wote regardlessly
Ndio maana Wachina wanawanyoosha tu wanadini shupavu kupitia internment camps, kulea ujinga wa aina hii huwezi kuwa na nchi bora.

Yani unaona ni bora tu nchi yako Tanganyika iharibikiwe kisa unahisi Zanzibar wanapingwa kwa sababu ya Uislamu wao!
 
Ni muda sahihi kila mkoa ukijitegemea kwenye baadhi ya mambo. Kama kuwa na bima ya afya na mambo kibao. Ili kama sio mzaliwa wa mkoa husika, usinufaike na sera zao
 
Nafuatilia kwa karibu ili kupata ukweli wa kali hizo za waziri,

na hata ikiwa ni kweli,
basi hayo yatakua ni maoni yake binafsi, na sio msimamo wa SMZ,
wagonjwa wote ambao ni wanadamu iwe ni wazanzibari na wasio wazanzibari wana haki ya kupata huduma za afya kukote watakapokua na changamoto za kiafya.

na hiyo ni haki ya msingi ya kibinadamu kimataifa.

So,
ni muhimu kupuza maoni binafsi ya huyo mumaa ikiwa ameeleza kama ilivyoripotiwa na wafuata mkumbo.

Huduma za afya zinatolewa inavyostahili Zanzibar kwa mgeni yeyote yule kutoka nje ya Zanzibar.

Hata hivyo,
kaumu waziri kwa uchache wa maelezo, naona kama vile waziri hakusema wagonjwa ambao sio wazanzibari wasitibiwe, ila amesema SMZ haina uwezo wa kubeba gharama za matibabu ya watu million 60 kwa bajeti ya trillion 8. So, watu wakatibiwe tu kwa gharama zao kama kawaida tufanyavyo bara.🐒
 
Boss, mpango wa tiba Bure ni kwa wanzibar ila kama unalipia matibabu basi huduma ni kwa wote,shida iko wapi hapo?


Binafsi naamini kabisa lau Zanzibar isingekuwa kwenye muungano wangefika mbali sana
My point exactly, huu muungano uvunjike tu kwani hata kwa Tanzania Bara(Tanganyika) unaielemea na ni hasara tupu. Mbona wenzao Ngazija wana-survive kivyaovyao.
Hata wao bara waache kutibiwa kwenye hospitals za serikali na huduma zote za kijamii iwe wanapewa kipaumbele wa Bara hao Wazenji wawe wanahesabika kuwa ni wageni.
 
Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa Watu wasio Wazanzibar.

Saada ametoa kauli hiyo Juni 8, 2026 wakati akijibu hoja kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia vikao vinavyoendelea vya kujadili bajeti mbalimbali.


“Mtu ambaye sio Mzanzibar anakwenda katika hospitali zetu anaonesha matibabu kadi, pili Watu kuzuiwa nadhani nilitoa maelezo sana, sio ZHF inaanza bali inaendelea kuwasajili wengine ambao sio wa sekta ya umma”

“Wakati Wanachama wa ZHF wakiendelea kusajiliwa kulikuwa na Matibabu Kadi zikitolewa unakwenda kwa Sheha unachukuliwa taarifa zako unakwenda hospitali hakuna anayekurudisha ilo moja, la pili kilichokuwa kikibainika kwa wenzetu wa hususan kwa ngazi ya Masheha si waaminifu, Mtu si Mzanzibar anakwenda kwenye hospitali zetu anaonesha matibabu kadi na wale waliokuwa wanakaa pale wanamwambia atoe kitambulisho cha Mtanzania”

Soma Pia: Zanzibar: Naibu Waziri wa Vijana, Hassan Khamis: Wanaofanya kazi kwenye Mahotel Zanzibar siyo wazawa inabidi tufanye Mapinduzi

“Bajeti yetu ya trilioni 8 tutaweza kuwatibu Watu milioni 60 ? Tumeona wengine sio Wazanzibar wanatibiwa kwa kutumia matibabu kadi,”amesema Kaimu Waziri wa Afya.

N.B: Huyu mama tukumbuke alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya Muungano

Hii ndoa ilishakua ngumu wanaoi ng'ang'ania hatujui ina maslahi gani maana hata kiusalama haijalishi tuna Zanzibar hatuna Alishabab wakiamua kutukalisha wanatukalisha tu..
 
Boss, mpango wa tiba Bure ni kwa wanzibar ila kama unalipia matibabu basi huduma ni kwa wote,shida iko wapi hapo?


Binafsi naamini kabisa lau Zanzibar isingekuwa kwenye muungano wangefika mbali sana
Mimi siamini kama wangefika mbali sana.

Znz haibanwi na Tanganyika kwenye mapato na huchangiwa mpaka bajeti.

Wangeweza kua mbali sana hata sasa
 
Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa Watu wasio Wazanzibar.

Saada ametoa kauli hiyo Juni 8, 2026 wakati akijibu hoja kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia vikao vinavyoendelea vya kujadili bajeti mbalimbali.


“Mtu ambaye sio Mzanzibar anakwenda katika hospitali zetu anaonesha matibabu kadi, pili Watu kuzuiwa nadhani nilitoa maelezo sana, sio ZHF inaanza bali inaendelea kuwasajili wengine ambao sio wa sekta ya umma”

“Wakati Wanachama wa ZHF wakiendelea kusajiliwa kulikuwa na Matibabu Kadi zikitolewa unakwenda kwa Sheha unachukuliwa taarifa zako unakwenda hospitali hakuna anayekurudisha ilo moja, la pili kilichokuwa kikibainika kwa wenzetu wa hususan kwa ngazi ya Masheha si waaminifu, Mtu si Mzanzibar anakwenda kwenye hospitali zetu anaonesha matibabu kadi na wale waliokuwa wanakaa pale wanamwambia atoe kitambulisho cha Mtanzania”

Soma Pia: Zanzibar: Naibu Waziri wa Vijana, Hassan Khamis: Wanaofanya kazi kwenye Mahotel Zanzibar siyo wazawa inabidi tufanye Mapinduzi

“Bajeti yetu ya trilioni 8 tutaweza kuwatibu Watu milioni 60 ? Tumeona wengine sio Wazanzibar wanatibiwa kwa kutumia matibabu kadi,”amesema Kaimu Waziri wa Afya.

N.B: Huyu mama tukumbuke alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya Muungano

Wazianzibari walioko Bara warudi makwao, wanakula hela yetu!
 
Mimi siamini kama wangefika mbali sana.

Znz haibanwi na Tanganyika kwenye mapato na huchangiwa mpaka bajeti.

Wangeweza kua mbali sana hata sasa
Sijui sana mambo ya vipengele vya Muungano,lakini lau wangekuwa nje ya muungano wangeweza kuvutia wawekezaji wengi na hasa ukichukulia kile ni kisiwa,uwekezaji ungekuwa wa kuvutia watalii zaidi ,naamini kabisa huu muungano lazima umeweka limit kwa baadhi ya mambo
 
Wameamua kuweka mambo hadharani mpaka sasa.

Tuwape taraka yao tu wawe single Mother.
 
My point exactly, huu muungano uvunjike tu kwani hata kwa Tanzania Bara(Tanganyika) unaielemea na ni hasara tupu. Mbona wenzao Ngazija wana-survive kivyaovyao.
Hata wao bara waache kutibiwa kwenye hospitals za serikali na huduma zote za kijamii iwe wanapewa kipaumbele wa Bara hao Wazenji wawe wanahesabika kuwa ni wageni.
Lau nasi tutaanzisha tiba Bure kwa watanganyika na tukawa na vibali maalumu nao wanatakiwa wasitie pua zao hapa.

Tatizo utanganyika wetu tulishauua,tupambane na hali zetu tu
 
Sijui sana mambo ya vipengele vya Muungano,lakini lau wangekuwa nje ya muungano wangeweza kuvutia wawekezaji wengi na hasa ukichukulia kile ni kisiwa,uwekezaji ungekuwa wa kuvutia watalii zaidi ,naamini kabisa huu muungano lazima umeweka limit kwa baadhi ya mambo
Kwa huu mtazamo wako wa upande wa uwekezaji na limits inawezekana upo sahihi.
 
Back
Top Bottom