Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari

Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari

Hawa ndugu wangekuwa wana uwezo wa kuzalisha chakula wasingeleta bara, viroho vibaya vipo juu sana, japo si wote.
Kuliko nyie watanganyika, mna chuki na roho mbaya.
 
Wazanzibari kina Jagina nawaunga mkono kwenye jambo moja tu ili wanalo semaga misikitini kuwa 👉 kichaa wa Zanzibar ni zaidi ya Shekh wa bara na nguruwe wa Zanzibar ni zaidi ya muhumini wa bara😁😁😁😁😁
Wacha kunipakazia , Nilisema wapi maneno hayo?
 
Wazianzibari walioko Bara warudi makwao, wanakula hela yetu!
Una hela ukiitoa wapi , Nyerere aliichukuwa pesa yote ya Zanzibar Narodjni Bank , London , 500 milioni Pounds wakati pesa yake iliisha kwenye vita na Uganda. Akaawaambia Watanganyika wakaze mikanda , .Dollar moja ilikuwa shilingi 7 tu . Leo iko ngapi utajua mwenyewe
 
Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kugharamia matibabu kwa Watu wasio Wazanzibar.

Saada ametoa kauli hiyo leo Juni 9, 2026 wakati akijibu hoja kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia vikao vinavyoendelea vya kujadili bajeti mbalimbali.

“Mtu ambaye sio Mzanzibar anakwenda katika hospitali zetu anaonesha matibabu kadi, pili Watu kuzuiwa nadhani nilitoa maelezo sana, sio ZHF inaanza bali inaendelea kuwasajili wengine ambao sio wa sekta ya umma”

“Wakati Wanachama wa ZHF wakiendelea kusajiliwa kulikuwa na Matibabu Kadi zikitolewa unakwenda kwa Sheha unachukuliwa taarifa zako unakwenda hospitali hakuna anayekurudisha ilo moja, la pili kilichokuwa kikibainika kwa wenzetu wa hususan kwa ngazi ya Masheha si waaminifu, Mtu si Mzanzibar anakwenda kwenye hospitali zetu anaonesha matibabu kadi na wale waliokuwa wanakaa pale wanamwambia atoe kitambulisho cha Mtanzania”

“Bajeti yetu ya trilioni 8 tutaweza kuwatibu Watu milioni 60 ? Tumeona wengine sio Wazanzibar wanatibiwa kwa kutumia matibabu kadi,”amesema Kaimu Waziri wa Afya.

Hata hivyo, Serikali ya Zanzibar inaendeleza sera ya matibabu bure ambapo kila Mzanzibar halipishwi fedha yeyote kwenye matibabu mbali mbali ikiwemo dialysis, upasuaji, kulazwa, huduma za dharura, upasuaji au homa.

Msijiendee tu zanzibar mkaugua hayaa
 
MUUNGANO ULIKUFA 2010 PALE KIKWETE ALIWARUHUSU ZANZIBAR KUWA NA KATIBA YAO
 
Hao ni wajinga sana, wangejua bila Tanganyika wangekuwa hohehae, ni bora huu muungano haramu uvunjwe tu kila mtu apambane na hali yake
 
Honestly Mimi saada nimemwelewa.
Huko Zanzibar matibabu kwao ni bure, kama sisi huku bara ilivyo Elimu bure.
Na nasikia Zanzibar wapo kwenye final stages kutoa pensions kwa wazee wote regardless aliwahi kuwa serikalini au uraiani...
Hajasema Sio kwamba wasio Wazanzibar hawatibiwi, HAPANA
Isipokuwa watatibiwa kwa hela.

Sasa hiyo BIMA ni ya WaZanzibar tu,
Na inagharamiwa na SMZ. kwasabu wasipoweka restrictions watu baki watakwenda huko kama medical tourists na BiMA kuelemewa.
BIMA BURE YA AFYA HATA BARA TUNAWEZA TUKIAMUA
Badala ya nyie Wabara kuwalalamikia Wazanzibar kuwanyima matibabu kadi ilitakiwa tushirikiane tupaze sauti zetu ili kuishinikiza serikali ifanye kama yanayofanyika huko Zanzibar.
Kumbuka hata hicho mnachokililia hakikuja hivihivi..Wapo watu wali-struggle..
Hamuwezi kulalamika kutotibiwa bure ugenini wakati huku kwenu Morogoro, Mbeya, Simiyu, au Tanga mnatibiwa kwa cash, na hamlalamiki.....

Badala ya kushinda kutwa, kujadili umbea wa akina Juma Lokole, sasa tubadilike tuanze kujadili mijadala yenye tija kwa Taifa.
1. Mfumuko wa bei
2. Huduma za jamii
3. Ajira
4. Chaguzi zetu
5. Rushwa kwenye jamii
6. Nk
 
Tatizo liko wapi?znz wameweza tunapaswa kuwapongeza.wamesema bajeti yao ni tr 8 hawawez kuwatibu watu milion 60 wako sahih bima yao hairuhusu.tuwapongeze wamefanya vyema.kwann wao wanaweza na sisi hatuwezi? tatizo ni uongozi mbovu tulianzisha bima ya afya tukashndwa.kwnn tuwalaamu wazanzbar walioweza?ww unayoweka serikali dhaifu kila chaguz umetokea tanga dodoma songea tabora unataka utibiwe bure znz una akili kweli?
 
Back
Top Bottom