Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari

Hii ndoa ilishakua ngumu wanaoi ng'ang'ania hatujui ina maslahi gani maana hata kiusalama haijalishi tuna Zanzibar hatuna Alishabab wakiamua kutukalisha wanatukalisha tu..
Ni ujinga tu.. na ni bomu baya siku likilipuka
 
Kwani kumetokea nini kwenye hii Nchi matamko yanakuwa mengi? hapo zamani tulikuwa tunaishije? Nafikiri kuna mahala hapako sawa pana hitaji kutazamwa kwa kina ili pasije kupasuka zaidi.
Kuna ombwe la uongozi...
Na laana za utekaji, mauaji na dhuluma za kisiasa.
 
Ndio maana Wachina wanawanyoosha tu wanadini shupavu kupitia internment camps, kulea ujinga wa aina hii huwezi kuwa na nchi bora.

Yani unaona ni bora tu nchi yako Tanganyika iharibikiwe kisa unahisi Zanzibar wanapingwa kwa sababu ya Uislamu wao!
Wapi nimesema bora iharibiwe kisa hivyo ?

Nimesema siwezi kuwaunga mkono na kuwa pamoja na wanajiita wanaharakati halafu wanachanganya na ajenda pamoja na chuki za kidini na kuacha hoja za msingi ni hivyo simple .

Kwani kupigana nchi Kuna njia Moja tu ya kuungana na watu Fulani na mimi siwezi kupigania kwa njia nyingine ?

Nisipokuwa pamoja na Chadema , Mange Kimambi au wana Jf katika njia zao na Mimi nikawa na njia zangu au nikawa na watu wengine katika kupigania nchi haifai na ni lazima niwe na watu walio changanya ajenda ?

Elewa wewe Mzee , mimi sijasema wala sifurahi nchi kuchezewa kwa namna yeyote bali point yangu kuu ni kuwa watu wanachanganya ajenda na kuwa na udini hawana moral justification ya kutaka hao wanawasema wawe pamoja nao
 
Sada mku
Sada mkuya yuko sahihi kabisa bajeti ya Afya ya Zanzibar ni kwa ajili ya wanzanzibari
 
Kabisa, tunalazimisha ndoa wakati mke hataki

Yes kabisa, sisi ndio kwenye kila mambo yetu lazima tuwaweke na Zanzibar, mgeni mashuhuri akija kwetu lazima tumpeleke na Zanzibar, hata Rais wa Singapore leo ameenda Zanzibar ila ni mgeni wetu

Ila hakuna mtu mashuhuri ambae kaalikwa Zanzibar then wakasema aje na bara

So shida iko kwetu

Yale maneno ya waziri wa vijana na maneno ya waziri wa afya hakuna mtu hapa kwetu anaweza kuyasema bungeni
 
Niliwahi andika kwamba "Rais samiah ndio Abood jumbe wa kizazi hiki"!?

yaani mama ndio atatusaidia kupata serikali tatu!!?je Msaada wa kijeshi wa Russia uta rush process ya serikali tatu!!?
 
Huyu amewahi kua waziri wa fedha Tanganyika stupid huu muungano kuna nini kilichojificha nyuma ya muungano
 
Tatizo Tanganyika ni nchi ya kufikirika tu
ila nchi ya zanzibar ipo

Muungano wa kidwazi sana Nyerere na wazee wenzake walikosea sana kuiuwa Tanganyika..

Lakini bado mpaka leo hii bado kuna mapimbi ya kijani yanaulinda huu muungano kwa nguvu zote sijui una maslahi gani kwao!
 
Na hapo ndipo penye ugumu. Nahisi kuna siri kuhusu muungano zaidi ya tu kuungana ila kwa investment na sheria zinavyoendeshwa kwa upande wa Zanzibar. Nina uhakika kuvunjika hakuko mbali maana Zanzibar ilitakiwa kupata goli moja tu ili kunyoosha kila kitu.

Na wanalifanya hilo kwa ustadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…