#COVID19 Kaka yangu amefariki kwa ugonjwa wa CORONA

Poleni sana, leo mimi najisikia ovyo kweli nimetapika angalau najisikia nafuu sijui ndiyo yenyewe dah
Unaona sasa[emoji849]hizi ndio hofu tunazozizungumzia kama kila mtanzania atakuwa akihusisha kila uchovu na kujiskia vibaya ni corona tutapoteza watu wengi mno nachukia sana ninapoona watu tunapeana hofu na kukuza hizi habari.
 
Kati ya kosa alilofanya n kwenda hospitali, ukiukwaa kaa home, jidisconnect na ulimwengu halafu assume ni tatizo la kawaida! Mm kama mm nimeupata nisave kwa namna hiyo lkn n maumivu yasiyoelezeka! Poleni sana
Naunga mkono hoja kama taifa tungeendelea kuwa na msimamo ule ule coz wagonjwa walikuwepo na tulikuwa tukijiuguza nyumbani na tunarudi uraiani sasa angalia tulivyoanza kuishi kwa mihemko madhara yake ndio haya
 
Poleni sana ndugu yangu. Hakika machungu ya ndugu hayasimuliki ila Mwenyezi Mungu anafahamu yaliyoko mbele yenu, inshaalah atakuvusheni kila penye hofu na vikwazo maana yeye ni mwingi wa rehema
 
Pole sana
Lakini hatutaacha kusema hii ndio legacy iliyoachwa na yule mfu mwendazake, kwa kuwajaza ujinga watanzania wakadhani wao corona haiwahusu, na wanaonekana hata humu kwenye posti na majibu ya kipuuzi
Ni hatari sana ukiwashika akili wajinga na masikini......ni tishio kwa usalama wa nchi
 
Poleni sana
 
Huyo alikua na magonjwa mengine either kisukari au HIV,
 
wakuu ikiwa uviko 19 ipo katika dalili za awali unatibu vipi kisayansi na kiasili?
 
Pole sana. Tatizo huu ugonjwa unaondoa watu kimzaha mzaha matokeo yake watu wanaupuuza. Mtu anaanza kuumwa kama utani vile unasikia kesho yake kaondoka. Nimepoteza mjomba wangu mpendwa wiki hii kimchezo mchezo tu

Tukachanjeni wandugu. Bora kuchanja mapema jamani before it's too late

Majuto mjukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…