Sijajua sababu ya kuleta uzi wako huu jukwaa la Sheria. Ila acha niseme umekosea. Hukukusudia. Kisheria, hakuna sheria inayolazimisha ndugu kupendana.
Lakini, huna haja ya kujilazimisha kwa mtu asiyekupenda. Kama anaona huna umuhimu, basi achana naye. Kuwa karibu na nduguzo wengine.
Kinachokutesa wewe ni kunyimwa msaada wa nduguyo. Wala si chuki. Maana sijaona popote alipokutenda ubaya. Ila kwa kuwa kila ukimuomba hakupatii, basi umeitafsiri kuwa ni chuki.
Pia, wapo watu wanapbaki na visasi sana. Huenda ulikuwa unapendwa sana na wazazi kuliko yeye. Wengine husahau, lakini wengine hulibeba moyoni. Anakua akiishi nalo, na hivyo kutengeneza nafasi ya kulipiza. Anashindwa hata kukusaidia, kwa sababu tu wazazi walikuthamini kuliko yeye.
Wazazi tujiangalie katika makuzi. Tusioneshe kumpenda mtoto mmoja zaidi ya wengine.
Kama unahisi ni chuki, kaa zungumza na wazazi wako. Waeleze, ila kigezo kisiwe kukusaidia. Ila viashiria vingine. Wazazi watazungumza naye na kujua undani.
Pole Mkuu.