Kaka yangu ananichukia

Sijajua sababu ya kuleta uzi wako huu jukwaa la Sheria. Ila acha niseme umekosea. Hukukusudia. Kisheria, hakuna sheria inayolazimisha ndugu kupendana.

Lakini, huna haja ya kujilazimisha kwa mtu asiyekupenda. Kama anaona huna umuhimu, basi achana naye. Kuwa karibu na nduguzo wengine.

Kinachokutesa wewe ni kunyimwa msaada wa nduguyo. Wala si chuki. Maana sijaona popote alipokutenda ubaya. Ila kwa kuwa kila ukimuomba hakupatii, basi umeitafsiri kuwa ni chuki.

Pia, wapo watu wanapbaki na visasi sana. Huenda ulikuwa unapendwa sana na wazazi kuliko yeye. Wengine husahau, lakini wengine hulibeba moyoni. Anakua akiishi nalo, na hivyo kutengeneza nafasi ya kulipiza. Anashindwa hata kukusaidia, kwa sababu tu wazazi walikuthamini kuliko yeye.
Wazazi tujiangalie katika makuzi. Tusioneshe kumpenda mtoto mmoja zaidi ya wengine.

Kama unahisi ni chuki, kaa zungumza na wazazi wako. Waeleze, ila kigezo kisiwe kukusaidia. Ila viashiria vingine. Wazazi watazungumza naye na kujua undani.

Pole Mkuu.
 
Kuna watu huwa tunatunza kumbukumbu hata za zaman,yawezakuwa zaman mkiwa wadogo uliwah mfanyia kitu kilichomkaa mpaka leo

Kuna watu huwa tunatunza kumbukumbu hata za zaman,yawezakuwa zaman mkiwa wadogo uliwah mfanyia kitu kilichomkaa mpaka leo
labda mkuu ila mi ni mdogo kwake yeye wa kwanza mimi wa nne
 
Nashukuru sana kwa mchango wako
 
Una umri gani na umemaliza lini chuo? Wewe unataka kaka yako akusaidie nini?
Mi sitaki anisaidie kitu ndiyo maana sijalalamika. The info I provided do with it what you will
 
mpotezee fanya yako utazoea kumuona wa kawaida
 
Mi sitaki anisaidie kitu ndiyo maana sijalalamika. The info I provided do with it what you will
Punguza hasira na jazba ulipofikia pambana mwenyewe ila usiibe fanya kazi yoyote iliyo mbele yako na usimtangazie yeyote elimu uliyo nayo kama hajakuuliza.sasa ni mwendo wa elimu ya mtaa chagama au vipi unaweza ukao..
 
Hajuwahi kukusaidia chochote !kwani lazima,nani kasema?imeandikwa wapi!kuzaliwa tumbo moja sio lazima msaidiane,
Tafuta maisha yako,binadamu wengi tu wanaweza kuwa ndugu zako,kuliko uliotoka nao tumbo moja,tafuta pesa,pesa,pesa,utapata heshima
 
Hajuwahi kukusaidia chochote !kwani lazima,nani kasema?imeandikwa wapi!kuzaliwa tumbo moja sio lazima msaidiane,
Tafuta maisha yako,binadamu wengi tu wanaweza kuwa ndugu zako,kuliko uliotoka nao tumbo moja,tafuta pesa,pesa,pesa,utapata heshima
Ndo hivyo
 
Hana mipango na wewe cha muhimu tafuta pesa mwenyewe atakuja kukusalimia kila asubuhi akiamuka ,Sisi kuna broo wetu wa Baba mmoja alikuwa anatubagua sana Tumesoma kwa shida alikuwa anawapa misaada ndgu wa nje Sio sisi ndgu zake muda huo ana magari 10 na maduka makubw ya pembe jeo. Hakuwai kukanyaga kwa Mama etu ata mara moja lakini saiz mzee amefariki na mama ake amefariki amebaki mama etu na saizi bro ameshafirisika hana kitu amebadilika sana adi leo Anakuja kukusalimia kila siku. na pale home anaendaga kusalimia kila akienda kijjn lazima pale akasamilie. SAKA PESA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…