Kaka yangu ananichukia

Dada ako atakua mchawi
 
Unalazimisha undugu kiruuuuh..... Me ndugu wa hvo nawapenda sana nawatesa kimaendeleo sio kimaneno
 
Mkuu ni heri uyo anayekuchukia live live kuliko yule anaekuchukia kimoyoni alafu usoni anakuchekea, ila uyo kaka yako yawezekana ni mchawi so kuna kitu labda alitaka kufanya kwako lkn anajikuta anashindwa kikubwa kaa nae mbali tu
 


Rahisi sana. Kazana na maisha yako. Tafuta sana hela ufanikiwe... Imetokea tu nyota zenu haziivi so usilazimishe, fanya mishe zako nyingine tu...
 
hakuna tatizo hapo wew tu ndo unahisi kuna tatizo hustle kivyako fanya maisha yako ndugu acha akusaidie akijisikia ila kama hakusaidii komaa tu mkuu.. mimi kulazimisha mzoea na ndugu ni jambo nisilowezaa undugu wa kumtafuta yeye tu wew anahisi unajikomba piga kimyaa..
 
Ni ndugu yako Lkn kuna siku hata moja umewahi kumuuliza shida ni nini maana, kiume ni kuangaliana usoni na kuuliza shida bila kuogopa kama ni Mwanaume kweli atanyoosha maelezo mtayamaliza lakini kama Hatonyoosha maelezo nakushauri achana naye tena usiendelee kumtatilia wala kutaka misaada kutoka kwake. Huenda akikuona unamfatilia sana na hayuko tayari kuyamaliza Ukaongeza tatizo baada ya kupunguza
 

Kwenye ukoo hawajosekanagi aisee mtu hujui umemkosea nin ila anakuchukia vibaya
 
Reactions: THT
Achana nae, nina huyo ndugu tena wa tumbo moja nae ana pigo hizo hizo nimetemana nae mwaka wa nne huu na tukikutana kila mtu na lake. Mtu kama hakutaki usilazimishe endelea na maisha yako.
 
Ila Kama huna nmb zake bas mkeo anazo na pengine wanawasiliana Sana

Mm shemeji angu Sina nmb zake na Wala Hana zangu amemuoa dada angu sijui wanako ishi uko arusha
 
Reactions: THT
Kwa sauti kubwa nasema,"ACHANA NAE" asilimia 90 ya wadau wamesema hivyo.
Angalia maisha yako ufanyaje yawe Bora. That's it
 
Kuna watu huwa tunatunza kumbukumbu hata za zaman,yawezakuwa zaman mkiwa wadogo uliwah mfanyia kitu kilichomkaa mpaka leo
Kweli kabisa, au kujibizana nae, kubisha kila akikutuma kitu, vitu hivi tulifanya kwa wakubwa zetu wakati wa utoto, japo si vizuri, wengine wanaweka kinyongo.
 
Mkuu mi sijaona tatizo lolote hapo acha kujiumiza akili kwasababu et kaka yako akusaidii kila mtu duniani anamaisha yake wewe kakayako kukusaidia au kutokusaidia hilo ni swala la hiari yake na kwenye haya maisha ishi kivyako.
Mimi ni wa mwisho kwetu tupo wa3 na wa2 ni kaka zangu wote mzee wao ni wanamaisha ya hatari bata South Africa bata Dubai kwao ni kawaida Sana kwenda kula bata mimi ndo nilimaliza chuo nina mwaka wa 3 saivi nipo napambana na maisha yangu sina time na mtu yoyote na hawajawah kuskia SIM zao zinaita namba yangu kwa shida yoyote mbaka kuna time wakajua kuwa nina weza kuishi bila wao na ndo wakaanzaga kunitafutaga wakinisalimia na kuniuliza kama nina shida yoyote nawajibu sina shida yoyote niko powa tu mambo yanaenda.
Sasa wewe unaanza kulalamika kuwa kakayako akusaidii heheheh utateseka Sana usipo badilika mkuu wewe kaza pambana mwenyew muonyeshe kuwa unauwezo wakushi bila yeye na ukaenjoy life Mungu ndo kila kitu kwenye haya maisha badilika kiongoz am telling you
 
Achna nae huyo, mchukulie kama sio ndugu yako... We unaona kabisa mtu anakuchukia bado unaendelea kujikomba komba mpaka kufungua thread? Jitambue kumbavu ww
Ukiwa kwenye situation hiyo huwezi kuignore, kwasababu ya maswali mengi, mtu a najiuliza kwani kuna nini ama amefanya nini hata ndugu yake hataki mazoea nae kabisa kabisa
 
huenda kuna jambo lilitokea huko nyuma mwenzako kabaki nalo mpaka sasa!

kaa naye chini, weka tofauti, umri na uwezo pembeni mtete!

ila jitayarishe kwa lolote! huenda kashuhudia kitu ama kaambiwa jambo na likawa la ukweli!

malizeni tofauti zenu! najua ni rahisi kusema kuliko kuyatenda, jaribu tu!
 
Ndo wapo hivyo ndugu zetu.Mimi ni miaka 6 sasa brother hatuwasiliani wala kuonana.Hata namba za simu sina za yule jamaa.Kila mtu afe kivyake ndo nimeamua hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…