Nimekuelewa hapo kwenye ukali wa nyota. Hii inawatokea watu wengi pasipo wao kujua, unakuta bosi na mfanyakazi wake, mpenzi na mpenzi wake, ndg na ndg, rafiki na rafiki.
Sawa kabisa Bwana Mseven! yaani ukifanyiwa ivo futa kabisaaaa kinyongo Moyoni mwako!! Utaona maajabu mbele, Vimba kimoyomoyo, fanya yako!
kuwa Mwema tu, jifanye mjinga kiaina lkn! akilini jua Nyota yako iko juu ni hatare!!...itaendaa watakupigia salute! usilipe ni ndg zako!! Nakupa mifani kidogo tu ya watu maarufu walio dharauliwa na ndg/wazazi!
Mandela, huyu ndugu zake hawajulikana saaana! mbali na mkewe Winnie na wanae!..... ina maana mke wa kwanza na wane alimdharau akamuacha! ndg zake walijua yule mlevi hana Maisha!
Mbali na Butiku, joseph nyerere,...ndg zake Nyerere hawajulikani kiviile Tanzania hii. sababu walimdharau mno wkt anadai Uhuru!...pia waliamini atapinduliwa Mbaya!
Martin Ruther ana ndg kibao lkn hawajulikani USA, Marcom x, unawajua ndg zake??....Zaidi ya hayo Ndg zake Yesu nani anawajua?? hata wachungaji wengi hawa wajui, na sababu kubwa wale walijua Yesu alikuwa Chizi!
Hata alipo surubiwa na kufufuka Msalabani ni Mama yake tuuu! na watu baki ndo tunawasikia km kina Mariamu Magdalena, hkn ndugu yake aliye kuwapo pale walimpuuza kitambo!
wakaenda Mbali zaidi na kumsema kuwa ''alirukwa na akili'' wakatamani kumfunga kamaba, hii ni kwa mujibu wa Biblia,......popote watu Wenye maono na Bright future,
Hawa wanachukiwa na kudharauliwa mnoo! Nyumbani na Makazini humo, hata waweza kufukuzwa kazi au kusimamishiwa mshahara kwa sababu za kipuuzi sana,.....Lkn mafanikio ya mbele ni hatare!
kwa sababu hii ndo Yesu akasema kuwa namnukuu ''Mti wenye Matunda ndiyo hupigwa Mawe''.....ukitafakari huu msemo utabakia kuchekaa tu!......
fikiria tu Yusufu alivo pigika! na kuchukiwa tena na ndugu zake hasaaa, na kilicho watokea baada ya hapo!...Nikutie Moyo tu, km hivi
ukitaka hao ndg zako wenye chuki wakuinamie siku moja mbele huko! usiwalipizie kisasi! utaona Maajabu!....usifanye kosa la kuwachukia au kuwalipizia kisasi,
hii inatokea hata kwa Mama zetu wa kambo!.....jikinge tu, na Mabalaa yake yasikudhuru, ila tu usiwalipizie kisasi ! ni ngumu sana lkn jitahidi kwa usalama wa kizazi chako!.....utabarikiwa mpaka useme yatosha sasa! !