Ipo hivi miaka kama kumi nyuma, baada ya baba yangu kufariki, tuliitwa na shangazi zetu tukapelekwa huko Tukuyu Busokelo tukapewa mji na kuambiwa sisi ndio tutakaoutunza mji, sababu ni baba yetu alikuwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia Yao ya watoto watu, na mbaya zaidi shangazi zetu hawapo hapa Tanzania. Mmoja kaolewa Zambia na mwingine yupo zake Uingereza kwa miaka mingi sasa
Baada ya kupewa mji Tukuyu ilibidi tukae vikao na ndugu zetu na tukajaribu kuwaeleza kuwa, kwa hali ilivyo itakuwa ngumu sisi kurudi Tukuyu kwa sababu sie pia tumetawanyika na nyumbani Njombe hapana mtu zaidi ya mama na mimi, so management ya Tukuyu itakuwa technically tuff
Kwenye mazungumzo tukamuomba baba yetu mdogo kwenye ukoo (baba yake alikuwa ni babu yetu mdogo walifuatana na babu yetu mzaa baba) baba yetu alijaribu kukata kwa sababu na yeye anaishi Mbeya mjini na kajipata sana
Baada ya kumsihi sana akatupa option kuwa Mbeya kwake yupo na shemeji yake wa kike (mdogo wa mke wake kabisa) akatueleza huyo shemeji yake ndoa yake ilivunjika akiwa na watoto wawili, yupo tu mjini). Tukamuomba basi yeye ndiye akae pale, kweli akakubali
Akahamia pale nilichokifanya nikapeleka mifugo na kumpatia mtaji kidogo wa kuendesha maisha kule kijijini (lengo la kupeleka mifugo ni kufanya mji uwe active pasionakane pametupwa kabisa)
Shida ilianzia hapa mwaka 2022, kaka yetu mkubwa akatushauri December lazima twende kule kijijini, kweli tulienda tukaa tukaona mazingira sio rafiki sana so tukazimia tujenge nyumba inayoendana na miaka ya sasa. Tukachangishana then tukaanza ujenzi wa msingi, baada ya kuondoka tukawa tumeazimia nyumba iishe kabla ya December 2023
Tukawa tumechangishana na kaka yangu tuliyefuatana akajitolea ataifanyia nyumba finishing na atamaliza Kila kitu, basi ilipofika December akashuka kule Tukuyu na mafundi wake Toka dar, kweli alijenga nyumba na kuanza kufanya finishings. Kumbe akiwa kule akawa anajipigia yule mama yetu pale
What happen there ni mimba na yule mwanamke ana mimba, aliyekuja kusema ni mke wa kaka yangu baada ya kugundua simu za bros hazipo sawa, shemeji kaniambia ukweli, nimewashirikisha kaka zangu wengine wamefedheheka sana na tukio lilivyo na tunaona aibu sana japo mhusika haonni shida na atamfanya yule mwanamke mke mdogo
Atamuacha pale na anadai anataka amfungulie duka kule kule kwenye kamji kadogo kanaitwa lwangwa, hapa tupo njia panda tunafanyaje, vipi Ile jamii kule wakijua itakuwaje? Wale ndugu zetu kule Kijijini watakuwa wanatuonaje wakija kujua. Je, baba mdogo atakuwa ametuweka kwenye kundi gani na kwa mila za Kinyakyusa hilo lipoje au tujiandae tu kurogwa?