Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Leo asubuhi kwenye mwendokasi ya Kimara-kivukoni kuna mzee alikuwa anaongea kwenye simu kwa sauti kubwa nafikiri intention yake ni watu wamsikie namnukuu "Huyo dogo ni fala anaoaje mwanamke mwenye mtoto huko ni sawa na kununua gari bovu wakati kuna wanawake wengi hawana watoto ona sasa kauza mpaka simu kuhudumia watoto wa mwenzie mi nilimwambia afukuze hao watoto waende kwa baba zao" Mwisho wa kunukuu..

Wanaoponda single maza wana hoja wasikilizwe.
Hatuwapondi ila hatuwataki kabisa kwenye kuwaoa, ila utelezi watupe tu
 
Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.
Huyo mwanaume ni wa mfano. Yaani nampongeza sana. Anajua anachokitafuta ktk maisha yake na anajua hawezi kipata kwa mwanamke mwenye mtoto. Mwacheni kijana wa watu aende kwa amani. Alilelew vyema na akafuata malezi mazuri, safi kabisa.

Mimi sitaoa kabisa single mother, ni never kabisa. Nolikua na sababu zangu ila jamaa kaniongea sababu zingine kiwa hata kwenye malezi ni ngumu kuwakanya watoto wako.

Good maen with brain. Mwanaume anaejielewa hawezi kuoa single mother. Wewe mwenyewe umesema kabisa kuwa ulimwelekeza mdogo wako jinsi ya kumwambia. Hayo uliyomwambia inawezekana hayana ukweli ni kumpanga tu kijana wa watu.

Huyo kijana ni mtu na nusu. Safi kabisa.
 
Back
Top Bottom