Kala Pina alitaka kuwatolea posa wasanii wenzake ambao ni Voice Wonder pamoja na Mr Blue nyakati hizo!!

Kala Pina alitaka kuwatolea posa wasanii wenzake ambao ni Voice Wonder pamoja na Mr Blue nyakati hizo!!

Meja Jenerali Isamuhyo

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
3,709
Reaction score
10,896
Ukizungumzia msanii wa Hip Hop waliokuwa wana matukio ya kushangaza na ukorofi basi huwezi kumuacha Kala Pina mzee wa Kikosi cha Mizinga kutokea pale Kinondoni Block 41.

Pina aliwahi kutishia kumtolea posa msanii mwenzake aitwaye Voice Wonder kisa tu anadai alikuwa anabana sauti wakati wa kuimba.
Msiomjua Voice Wonder tafuteni wimbo wake unaitwa “Nimpende nani?”

Kala Pina pia alitaka kumtolea posa Mr Blue kwa kubana sauti wakati wa kuongea na kung’ata lips alipokuwa anaongea/kuhojiwa. Pina hakuwa anafurahishwa pia na style ya Mr Blur kupaka rangi kwenye nywele.

Kala Pina aliwahi kugombana na machalii wa Chugga, baada ya kumpiga na chuma kwenye mdomo msanii wa kundi la Nako2 Nako aliyefahamika kama Bou Nako. Jamaa ilibidi afanyiwe operesheni kubwa ya kurekebisha meno yake.

Kala Pina kwenye 1&2 aliwahi kumteka Salama Jabir kwasababu ya Salama kupenda kumnanga jamaa kuwa huwa anatoa video mbaya.

Leo nimejikuta nimenkumbuka Mzee wangu Kala Pina na kundi lake la Kikosi cha Mizinga pale maskani kwao Block 41.

Kama uhuni ulifanywa sana zamani, BASATA hawakuwa na meno kama ilivyosasa!!
 
Mara ya mwisho nilikutana nae stendi mwenge,ni kiongozi wa shughuli za kila siku pale, kuhusu kumtolea posa blue alikana,tena akiwa pamoja na blue
Kuna tukio moja kikosi wanapafom,shabiki akanogewa akapanda jukwaani,alimrudisha chini kwa bonge la teke
😂😂😂😂😂
 
Mara ya mwisho nilikutana nae stendi mwenge,ni kiongozi wa shughuli za kila siku pale, kuhusu kumtolea posa blue alikana,tena akiwa pamoja na blue
Kuna tukio moja kikosi wanapafom,shabiki akanogewa akapanda jukwaani,alimrudisha chini kwa bonge la teke
Ata chid benzi,alitolewa jukwaani na bonge la ngumu na kalapina
 
Yuko wapi sasa huyo kala pina? Picha yake je?
Hii ndiyo ilikuwa picha yake wakati akifanya hayo matukio
Screenshot_2025-05-20-22-19-19-928_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg


Kwa sasa umri umesogea ameingia utu uzima kiasi.
 
Nakumbuka zamani wakati Kiss FM ikiwa ya moto ilikuwa inawapa sana airtime hawa jamaa,kwao freestyle ililala pale walikuwa hawashikiki.
Kwa freestyle hakuna artist aliyekuwa anafikia level za Ngwea"the Late himself", he was the surname of freestyle.

Mwana fa alikiri wazi Ngwea ni hatari
Fid q alifutishwa verse mara kadhaa kwenye ngoma ya CNN. The man was ahead of time!
 
Back
Top Bottom