Kalynda imeondoka na kijiji, Viongozi hawajulikani walipo

Mimi nasema wazi, sensa ya watu na makazi inaweza kuonyesha labda tuko 70mil lakini kwa hakika pengine nusu ya hawa 70mil ni "misukule". Yaani watu wapo wanaishi lakini akili zao zinaongozwa na wengine.

Hii nchi hata maendeleo tuliyo nayo leo hayaakisi rasilimali tulizonazo sababu ya hawa "misukule". Hawana uwezo wa kufikiri, kuchanganua wala kuhoji kitu zaidi ya kuamini kila wanaloambiwa.

Mtaji wa Wanasiasa na matapeli ni uwepo wa watu kama hawa. Mbaya zaidi wapo kwa idadi kubwa sana kiasi cha kuathiri mambo mbalimbali muhimu ya kijamii. Leo watatapeliwa na hao Kalyinda sijui, next time wakija wengine still watajiunga.

Yaani wakiambiwa tu kua sisi sio kama wale wakaonyeshwa vyeti vya ku download Brela basi washaingia mkenge. Wao ni wale wakiumwa na nyoka hata wakimuona nyoka mwengine (sio jani hata) hawashtuki kabisa.
 
Ila master mind wa kalynda kama si mnigeria basi mghana au mkenya, kasi waliokuja nayo mzembe mzembe hutoboi , ila watu walionywa hawakusikia
Mimi Green card tu naona ni Utapeli wa Wamarekani ndio sembuse hizi kekundu keupe unanipataje?

Kuna tapeli juzi nimemkimbiza humu ati anajifanya wakala wa ajira Qatar, anajuwa wabongo walivyo na shida ya ajira atawajaza, akajifanya eti kuna kiingilio cha ofisini, kudadeki.

Nawapa hesabu rahisi 20,000 Γ— 20,000/= ni schilling ngapi? Ni million 400 cash hiyo unasema nayo unawaacha walio register kusubiri ajira, ukitowa kodi ya ofisi miezi 6 na vidampa kama wanne uliowapa ajira za muda na pocket money za viherehere wa serikali wanaokuja kuhojihoji yani toptop hukosi million 300 kwa muda mfupi tu huyo unasepa na kijiji unachaguwa ukaishi wapi na pesa za mazezeta.
 
Tanzania Ni Tajiri Pesa Chekwa
Yaani Mtu Anakuletea Cash Yake Mwenyewe Huwezi Kuiacha Kamwe
nasema Wapigwe Tu Tumechoka

Bwana Bure Hayupo Ndugu Zangu
 
Eeehhhh poleni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…