Hiyo taarifa ukiangalia ni yauongo Kwa sababu,
Haionyeshi Yesu alizaliwa Sehemu gani, hivyo unaweza sema Yesu alizaliwa hapa DAR es salaam,
Haionyeshi Kwa nini Yesu alizaliwa nje chini ya mtende?
Haya embu soma Biblia uone inavyoweza kutumika Mahakamani kwasababu inajibu in full details
1. Yesu alizaliwa wapi? Eneo
Jibu: Bethlehem ya uyahudi.
2. Alizaliwa wapi( labour yake)?
Jibu; kwenye Hori la ng'ombe
3. Alizaliwa muda gani?
Jibu; alizaliwa usiku
4. Kwa nini alizaliwa kwenye hori la ng'ombe kwani hakuna nyumba?
Jibu; Ilikuwa ni kipindi cha Sensa ya uyahudi hivyo wayahudi wengi walirudi kuhesabiwa mpaka wengine wakakosa nyumba za wageni. Mariam na Yusufu walikuwa sehemu ya waliokosa sehemu ya kukaa. Ndio maana Uchungu ulipomshika akazaliwa kwenye hori la ng'ombe.
5. Yesu alizaliwa wakati WA utawala wa Nani na Dola gani?
Jibu; Yesu alizaliwa nyakati za Dola la Tumi, n Mfalme wa eneo lile aliitwa Herode.
Hiyo ni Biblia ambayo mahakamani inaweza kusikilizwa, lakini Quran haina data hizo na sio kosa Kwa sababu mwandishi wake hakuwepo wakati huo na hapajui hata anapopasimulia.
Soma;
Luka 2:6
Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,
Luka 2:7
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Luka 2:11
maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.
Luka 2:12
Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.
Mathayo 2:1
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Mathayo 2:2
Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Mathayo 2:3
Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
Mathayo 2:4
Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
Mathayo 2:5
Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;
Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Mathayo 2:7
Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
Mathayo 2:8
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.