Mkuu Robert,
Ingekufaa zaidi lau ungeleta hoja za kutaka wewe binafsi ujielimishe hasa katika maswala ambayo huna ujuzi nayo. Lakini ulichofanya ni kutoa hukumu kwa yale usio na elimu nayo kwa ku-conclude. Hii ni tofati sana na vile mwanzo nilivyokudhania kama msomi mzuri na mwerevu wa mambo kwa kuzisoma posts zako.
Basi hoja za madai yako haya yanaweza kujibiwa kwa uchache wa maneno kwenye kila hoja yako kama ifuatavyo:
1. Kwanza kabisa tambua kuwa Qur'ani sio hearsay. Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu (Hapa namkusudia Allah) yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (Swala na Salaam ziwe juu yake) kupitia kwa Malaika Jibril.
Hivyo Qur'an sio maneno ya Muhammad. Na uzuri baadhi ya hoja ambazo hata enzi hizo zilikuwa zikitolewa dhidi ya Qur 'an kama utoavyo wewe zimejibiwa ndani ya Qur'an yenyewe. Kwakuwa wewe unaipitia Tarjama ya Qur'an yaani Tarjama ya lugha ya Kiswahili basi kasome Sura ya 53 Aya ya 3-5 yaani Suurat Najm. Hapo utatambua kuwa Qur'an sio maneno ya Muhammad na wala sio hearsay.
Baada sasa ya wewe kutambua kuwa Qur'an ni maneno ya Allah yaliyoshushwa kwa Mtume Muhammad, unapaswa pia kutambua kuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho aliyetumwa baada ya Mitume wengi waliopita kabla yake mfano wa Ibrahim, Ismail, Ishaqa, Yaakub, Zakaria, Yahya, Issa (Yesu), Mussa, Haarun, Daud, Suleiman (Amani ziwe juu yao).
Kwakuwa ni Mtume wa mwisho, na Qur'an ndio kitabu cha mwisho kama muongozo kwa viumbe, basi Qur'an imetoa habari za mambo yote yaliyopita na yatakayokuja mpaka siku ya Qiyama.
Aliyewatuma hao mitume wote waliopita kabla ya Muhammad yaani Allah ndiye anayetoa habari za mitume hao tena kwa usahihi.
Ni kweli kabisa katika habari za Mitume walwaliotangulia, Muhammad hakuwepo. Bali anayesimulia ni yule aliyewatuma Mitume hao. Sasa wewe Robert unadhani Mwenyezi Mungu aliyewatuma Mitume kufikisha ujumbe kwa waja wake atashindwa kumueleza Mtume wake habari za Mitume hao?
Na si yeye tu Muhammad, bali kila Mtume aliyetumwa alielezwa habari za Mitume wa kabla yake ili watu wake wapate mazingatio.
Soma Sura ya Tatu aya ya 44 yaani Suurat Imraan utambue kwamba habari zote za Mitume waliopita amefunuliwa na Mwenyezi Mungu.
Hii ni katika dalili za wazi pia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hakujua kusoma wala kuandika lakini alitoa habari zilizopita kabla yake. Na utambue kuwa sehemu ya habari hizo alizosimulia ni Mayahudi wasomi wa Taurat ya Mussa walitumia nafasi hiyo kumuuliza Mtume Muhammad baadhi ya mambo yaliyopita ambayo Mtume hakuwepo ilhali wao Mayahudi wanafahamu kupitia kitabu chao cha Taurat.
Walimuuliza ili kumpima kama yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu akamshushia Wahyi juu ya habari hizo ambazo wao Mayahudi wanazifahamu kwakuwa wanazisoma kwenye Taurat. Na majibu ya Muhammad yalisadifu vyema ukweli wa habari hizo.
Mfano wa maswali aliyoulizwa na Mayahudi ili kumpima Muhammad atoe habari zake ilhali hakuwepo wakati huo ni pale alipoulizwa juu ya vijana watatu wa pangoni. Allah akamshushia Wahyi kuwajibu waliomuuliza maswali. Aidha aliulizwa juu ya Dhul-Qarnaini, juu ya Roho na kadhaalika kisha akateremshiwa Wahyi kutoka kwa Mwennyezi Mungu na akajibu kwa fasaha kama tunavyojifunza katika Surah ya 18 Aya ya 83 yaani Suurat Al-Kahf au Sura ya 17 Aya ya 85. Hebu Mr. Robert soma hizo aya upate kujifunza kwanini Muhammad amesimulia habari wakati hakuwa akizijua na wala hakuwepo. Jibu ni jepesi, Qur'an sio maneno yake. Ni maneno ya Allah yaliyopitia kwa Malaika Jibril.
Kwakuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho, na wametangulia wengi kabla yake na Qur'an ni kitabu cha mwisho sio ajabu kukuta ndani ya Qur'an habari zote zilizopita za Mitume na watu wao kuelezwa. Zinaelezwa ili watu wajue na wapate mazingatio. Soma Surah ya 23 Aya ya 44 kujua sio tu Muhammad bali kila Mtume aliyetumwa alitoa habari kwa watu wake juu wale waliopita. Na hawakutoa kwa maneno yao bali walifunuliwa na Mwenyezi Mungu.
Sio ajabu Muhammad kupitia Qur'n ameeleza habari za kale ilhali hakuwepo. Iwe ni jibu kwako wewe kuwa huyo Muhammad ni Mtume wa kweli aliyetumwa, anasimulia asiyoyashuhudia kwa usahihi kwa sababu ni Mwenyezi Mungu ndio anamsimulia.
Jibu hilo hapo juu.
Sasa utakuwa unaanza kuelewa. Kama usemavyo kuwa Biblia (japo hili jina la Biblia hata ndani ya hicho kitabu hakuna hilo jina la kitabu kiitwacho Biblia ambacho kilishushwa kwa Yesu) imekusanya vitabu vilivyoshushwa kwa Manabii mbalimbali, Qur'an ni kitabu cha mwisho. Ndani ya Qur'an imeeleza habari za Mitume wote waliotangulia na vitabu vyao. Kisha ikaeleza habari zitakazokuja baadaye mpaka siku ya Qiyama.
Tambua Ewe Robert, Mwenyezi Mungu hakutuma Mtume mpya kwa waja wake mpaka pale waja wanapokengeuka na kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume. Kwenda kinyume ni pamoja na kuasi, kupuuza mafundisho au kubadili maandiko ya vitabu.
Kwa huruma yake Allah humtuma Mtume mwingine abainishe na kusahihisha yale yaliyopotoshwa.
Ndio maana hata Yesu alisema hajaja ili kuitengua Taurat bali kuitimiliza.
Qur'an imebainisha yote yaliyopita na kusahihisha yote yaliyopotoshwa ili kuwaokoa watu na upotevu. Ipo mifano mingi, kwakuwa wewe Robert ni Mkristo unayeamini katika utatu wa Mungu, Qur'an inakusahihisha kwamba usiseme Utatu bali Mwenyezi Mungu ni Mmoja wala hana Utatu. Huo ni upotevu wa wazi ambao ni kinyume na Mafundisho ya Yesu.
Tafadhali, soma Surah ya 5 aya ya 73 yaani Suurat Al Maida. Kwa faida zaidi Mr. Robert soma pia Surah ya 4 aya ya 163 na aya ya 171 yaani Suurat Nisaa. Soma Surah ya 5 aya ya 46 ili upate kubainikiwa.
Aidha, kujua ni kwa namna gani Mafundisho ya Yesu yamebadilishwa na hao unaowasifu ni waandishi wa habari zake akiwemo Paulo, tambua sababu ya kushushwa Qur'an ikiwemo ni kasahihisha yaliyopotoshwa. Kwa faida tu, Aya hii ndani ya Qur'an inawatahadharisha ninyi Wakristo juu ya imani yenu kuwa Yesu ni Mungu.
Nayo ni Surah ya 5 aya ya 116 hadi ya 118 Allah atakavyomuhoji Yesu siku ya Qiyama juu hii imani yenu iliyopotoshwa kwa kumfanua Yesu ni Mungu.
"Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryam! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu!? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifai mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mkubwa wa yaliyofichikana.
Sikuwaambia lolote ila uliyoniamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao. Na uliponifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na wewe ni shahidi juu ya kila kitu.
Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hekima. "
(Surah ya 5 aya ya 116 mpaka aya ya 118).
Upotevu huo ndiyo sababu Muhammad ametumwa kama alivyotumwa Yesu, Mussa, na Mitume wengine kabla yake kuja kusahihisha makosa na upotevu uliosababishwa na watu kubadili maandiko kwa manufaa yao ya kidunia.
Nakusahihisha Robert,
Hao mitume uliowataja hawakiandika vitabu. Mitume wanashushiwa Wahyi yaani Ufunuo ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu.
Tunazungumzia mfano Injili ya Yesu haya sio uandishi wa Yesu. Ni maneno ya Mwenyezi Mungu aliyoshushiwa Yesu na msneno hayo ndio Kitabu cha Injili. Kadhaalika Taurat ya Mussa na Zaburi ya Daud. Ni vitabu ambavyo waandishi sio hao Mitume bali ni mane i ya Mwenyezi Mungu kupitia hao Mitume.
Hakuna aliyesimulia hadith zake mwenyewe wala kujiandikia kitabu chake mwenyewe. Mitume walipewa ufunuo, na mfano wake ndio vitabu kama Zabur, Taurat, Injili na Qur'an.
Muhammad hajashushiwa 'vitabu' bali ameshushiwa 'kitabu' nacho ni Qur'an. Ndani ya Qur'an hakuna kitabu cha Injili, Taurat wala Zabur bali kuna habari zote za Mitume wote waliotumwa kabla yake. Alichokifanya Muhammad hakimo kwenye Qur'an kwa sababu Qur'an si maneno ya Muhammad bali Muhammad ameishi kwa kuifuata na kuifundisha Qur'an kama muongozo kwa watu. Hilo litambue Robert.
Robert,
Elewa pia Mitume wote waliopita kabla ya Muhammad yaani Yesu, Mussa, Zakaria, Yahya, Ibrahim, Ismail, Ishaqa, Yaakub, Lut, Yunus, Nuh na wengineo walitumwa kwa watu maalum. Kama ilivyo Mussa na Yesu wao walitunwa kwa Wana wa Israil pekee.
Muhammad ametumwa kwa watu wote wakiwemo watu wa kitabu (Ahlul Kitabu) yaani hao Mayahudi na Manasara (Wakristo) ambao sehemu kubwa ya mafundisho ya Yesu yamepotoshwa.
Ndio maana ndani ya Qur'an zipo habari za Mayahudi na Manasara na kubainisha upotevu wao. Muhammad anatokana na Waarabu na lugha yake ni kiarabu. Na Qur'an maneno ya Mwenyezi Mungu yameshushwa kwa lugha ya Mtume aliyetumwa ambaye ni Mwarabu.
Shida iko wapi ndugu Robert kama Qur'an imetoa habari za wayahudi kwa kiarabu!? Ama ulitaka Mtume awe Mwarabu halafu azungume kizungu kisha useme "iweje Mtume mwarabu halafu anasema kizungu?
Ah! Taikun wa Fasihi umepatwa na nini?
Ni fasihi gani hiyo unayojivunia nayo kiasi cha kutokujua kuwa suala la kutoa habari fulani ya watu fulani halifungamani na lugha ya mtu?
Mwenyezi Mungu aliyemtuma Mussa au Isa na kuwapa Tuarat na Injil kwa fikra zako atashindwa kumueleza Muhammad juu ya yale waliyopewa mitume wenzie waliopita kabla yake? Masimulizi ya habari za hao mitume waliomtangulia Muhammad sio utunzi wa Muhammad bali ni maneno ya Mwenyezi Mungu akimuhabarisha Muhammad.
Sasa lugha inakuwaje kikwazo hapo?
Kuwa Myahudi na rafiki wa Yesu hakuashirii kuwa ndio ukweli wa anachosema. Kwani Yuda alikuwa nani kwa Yesu?
Anayesema katika Qur'an juu ya namna Maryam mama wa Yesu alivyobashiriwa kumzaa Yesu na mahala alipomzalia sio Muhammad bali anayesema ni Mwenyezi Mungu.
Qur'an si maneno ya Muhammad.
Rafiki wa Yesu hawezi kuwa na maarifa zaidi kumzidi Mwenyezi Mungu, neno la Mwenyezi Mungu ndilo sahihi kuliko neno la Yohana.
Nakusahihisha ndugu Robert,
Suleiman hajafuga majini bali Mwenyezi Mungu alimpa uwezo wa kuwatumikisha atakavyo. Kuku, mbuzi na mbwa ndio unaweza kuwafuga.
Na hii ni kwa kuwa kila Mtume Mwenyezi Mungu alimpa miujiza na karama zake ili kuwa hoja kwa watu wake.
Kama ambavyo Mwenyezi Mungu alivyomfanya Daud na Suleiman kutambua lugha za wadudu, wanyama, ndege. Bali hata upepo pia Suleiman alipewa uwezo wa kuuamrisha. Yesu naye alipewa miujiza ya kuwafufua wafu, kuwaponya viwete na kuzungumza angali mdogo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Habari za Mitume wote waliomtangulia Muhammad hakuzitunga yeye, amefunuliwa na yule aliyewafunulia waliopita kabla yake, yaani Mwenyezi Mungu.
Huo ni upungufu uliomo katika kitabu chako unachokiamini. Pia hakuna Mtume aliyejiandikia hadith zake. Yesu alijiandikia hadith gani? Yesu alipewa Injili ikiwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Injili sio hadith za Yesu alizojiandikia, Iweje useme Suleiman na mwanawe wamejiandikia hadith? Kama kitabu chako ndio kimeandika hivyo basi huo ni upotevu na upungufu mkubwa.
Mwenyezi Mungu aliyewatuma Mussa, Yesu, Ibrahim na mitume wote akiwemo Muhammad ni Mungu mmoja tu. Mungu wa Musa ndio Mungu wa Yesu, Ibrahim, Yaakub na mitume wote na viumbe wote ambaye ndio Mola wa viumbe wote ukiwemo na wewe.
Bali ni ukweli ambao ninyi Wakristo hampendi kuusikia kuwa Yesu sio Mungu, Yesu ni Mtume tu aliyetumwa na wamepita mitume wengi kabla yake. Mitume wote hao kuanzia Nuhu, Ibrahim, Lut, Mussa, Isa mpaka Muhammad wote wametumwa na Nwenyezi Mungu mmoja. Unastaajabu kusikia neno "Allah"?
Wewe Taikun wa Fasihi kwa fasihi yako ya kiswahili huyo Yehova wewe unaita Mungu. Ukienda kwa Mataikun wenzio wa fasihi ya Kiingereza huyo Mungu wanamuita God. Sasa Taikun, Yehova, God na Mungu ni kitu kimoja au ni tofauti!?
Ukinijibu hapo basi hutapata shida kwanini "Allah" ndio Mungu muumba mbigu, ardhi na vilivyomo na ndiye anayepaswa kuab udiwa yeye pekee.
Jibu la hoja hii limejibiwa hapo juu.
Qur'an iko sawa, haijapuyanga kama usemavyo Robert.
Kuanzia Mtume wa Mwanzo Nuhu mpaka wa Mwisho Muhammad, katikati yao wakiwemo Mussa, Yesu, Ibrahim na wengineo wote hawakuwa dini ya Uyahudi. Wote walikuwa ni Waislam.
Pengine Taikun hujui nini maana ya Uislam. Nitakurudisha darasani mahususi ujue maana ya Islam kama dini. Hapa si mahala pake.
Kama unavyidai wewe pamoja na wengine wengi kuwa Qur'an imenakili visa vya biblia, inawezekanaje Mtu (Muhammad) anakili visa wakati Muhammad hakujua kusoma wala kuandika?
Na kitendo cha Mwenyezi Mungu kumleta Mtume Muhammad asiyejua kusoma wala kuandika kina hekima kubwa sana.
Hapana shaka wangesema na hata wewe ungesema Muhammad ameandika mwenyewe maneno haya yaani Qur'an. Sasa angenakili vipi visa viliyoandikwa kwenye vitabu vya mitume waliopita kabla yake ilhali yeye hajui kusoma wala kuandika?
Qur'an haijanakili chochote kutoka kokote. Visa vinavyofanana katika Qur'an na Taurat na Injil sio ajabu kwakuwa vitabu vyote vimetoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume wake.
Ndio maana Mayahud walijaribu kumchallenge Muhammad kwa kumuuliza habari za zamani kabisa ambazo Muhammad hakuwepo na habari hizo zimo kwenye Taurat zao Mayahud na Mtume Muhammad hajui kusoma lakini walijibiwa kisawasawa visa hivyo.
Kwakuwa aliyesimulia visa ndani ya Taurat na Injili ndio huyo huyo Mwenyezi Mungu aliyemfunulia Mtume wake Muhammad.
Qur'an chanzo chake sio Biblia Robert.
Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoshushwa kwa Muhammad kupitia Malaika Jubril.
Qur'an imeeleza yote yaliyopita kwa Mitume na watu wao, inaeleza habari ya yatakayokuja baadaye, inabainisha haki na baatili, inatoa mwongozo wa maisha ya bunadamu. Inatoa habari njema kwa wenye kuamini na kutenda mema na inatahadharisha mafikio mabaya kwa watakao kwenda kinyume na muongozo huo.
Qur'an ndio kitabu cha mwisho na muongozo kwa watu wote, kimebainisha wazi habari zote zilizopita za mitume wote. Unataka ziondolewe habari hizo ili ummu huu usipate kutambua yaliyopita kabla yao?
Qur'an imeeleza mpaka yale ambayo yamepotoshwa na watu yaliyoletwa kwenye Injili ya Yesu na Taurat ya Mussa.
Qur'an imetakasika na upotevu, na ndio njia ya sawasawa baada ya Mwenyezi Mungu kumtuma Yesu kwa Mayahudi kisha Mayahudi wakambadilisha Yesu badala Mtume wakamfanya Yesu ndio Mungu! Huu ni upotevu ambao Qur'an imekuja kubainisha ili kuwa katika uongofu.
Qur'an haijaja kukueleza eti tawala za watu zilifuatana vipi. Qur'an ni muongozo kamili wa maisha ya mwanadamu.
Vipi, kwenye Biblia wamezungumzia pia Utawala na Uongozi wa Rais wa Tanzania wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan?
Kwako wewe ungeyakuta haya kwenye Qur'an ndio ungeamini kuwa Qur'an ni kitabu cha Mwenyezi Mungu?
Qur'an hakuna ilichoacha katika kutoa muongozo wa maisha ya mwanadamu. Na nyingi katika hoja zenu zimejibiwa ndani ya Qur'an yenyewe.
Hayo maswali yako mwisho utaishia kuiuliza Qur'an "nyumbani kwangu kuna viti vingapi?" Kisha useme Qur'an imeshindwa kukujibu.
Kwahiyo Taikun wewe kwa Mtazamo wako unaona alipozaliwa Yesu kwenye Mtende huo Mtende ni wa pale Tandale kwa Tumbo? Acha masihara kwenye mambo ya msingi Taikun.
Kwani Yakobo alikuwepo wakati wa Yesu!? Habari za Yakobo Yesu alizitoa wapi? Kama Qur'an imeielezea Taurat na Injil ndani yeke itaacheje kumtaja Yakobo na watoto wake? Soma Surah ya Al Imraan Aya ya 84, Al Baqarah aya 136, An Nisaa aya ya 163 kisha malizia na Al Baqarah aya ya 140 uone sio watoto tu wa Yakobo bali mpaka wajukuu zake wametajwa humo.
Hebu Taikun unapoamua kutoa bandiko la namna kama hii uwe kweli umesoma na umetafiti vya kutosha basi. Vinginevyo unajidhalilisha mbele za watu.
Utaikun wako wa fasihi uko wapi sasa?
Qur'an ina nondo zote, zilizopita na zijazo. Hata zile zilizopita ambazo zimepotoshwa au kufichwa Qur'an imezibanisha. Na imepambanua haki na baatil. Na imekuja kusafisha yote yaliyopotoshwa ambayo Yesu aliyafundisha kisha baadaye yakapotoshwa kwa makusudi. Mojawapo kubwa na baya zaidi ni kumfanya Yesu kuwa ni Mungu wakati yeye ni Mtume tu na mitume wengi wamepita kabla yake.
Utaikon wako ungejikita zaidi kudadavua pale ambapo Yesu mwenyewe anasema kwenye hiyo ambayo ninyi mnaiita Biblia kuwa yeye ametumwa tu, na aliyemtuma ni Mungu. Kisha mkamfanya tena yeye ndio Mungu muabudiwa badala ya kumuabudu yule ambaye amemtuma Yesu kama alivyomtuma Mussa na mitume wengineo.