Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

QURAN 4:82
"Je hawaizingatii hii Quran? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu, basi bila shaka wangelikuta ndani yake hitilafu nyingi"
  1. Understanding Muhammad, a Psychobiography” by Ali Sina.
  2. “Why I am not a Muslim” by ibn Waraq.
  3. Psychology of Mohammed: Inside the Brain of a Prophet” by Dr. Masud Ansari.
 
Mkuu Robert,
Ingekufaa zaidi lau ungeleta hoja za kutaka wewe binafsi ujielimishe hasa katika maswala ambayo huna ujuzi nayo. Lakini ulichofanya ni kutoa hukumu kwa yale usio na elimu nayo kwa ku-conclude. Hii ni tofati sana na vile mwanzo nilivyokudhania kama msomi mzuri na mwerevu wa mambo kwa kuzisoma posts zako.
Basi hoja za madai yako haya yanaweza kujibiwa kwa uchache wa maneno kwenye kila hoja yako kama ifuatavyo:

1. Kwanza kabisa tambua kuwa Qur'ani sio hearsay. Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu (Hapa namkusudia Allah) yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad (Swala na Salaam ziwe juu yake) kupitia kwa Malaika Jibril.
Hivyo Qur'an sio maneno ya Muhammad. Na uzuri baadhi ya hoja ambazo hata enzi hizo zilikuwa zikitolewa dhidi ya Qur 'an kama utoavyo wewe zimejibiwa ndani ya Qur'an yenyewe. Kwakuwa wewe unaipitia Tarjama ya Qur'an yaani Tarjama ya lugha ya Kiswahili basi kasome Sura ya 53 Aya ya 3-5 yaani Suurat Najm. Hapo utatambua kuwa Qur'an sio maneno ya Muhammad na wala sio hearsay.

Baada sasa ya wewe kutambua kuwa Qur'an ni maneno ya Allah yaliyoshushwa kwa Mtume Muhammad, unapaswa pia kutambua kuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho aliyetumwa baada ya Mitume wengi waliopita kabla yake mfano wa Ibrahim, Ismail, Ishaqa, Yaakub, Zakaria, Yahya, Issa (Yesu), Mussa, Haarun, Daud, Suleiman (Amani ziwe juu yao).

Kwakuwa ni Mtume wa mwisho, na Qur'an ndio kitabu cha mwisho kama muongozo kwa viumbe, basi Qur'an imetoa habari za mambo yote yaliyopita na yatakayokuja mpaka siku ya Qiyama.
Aliyewatuma hao mitume wote waliopita kabla ya Muhammad yaani Allah ndiye anayetoa habari za mitume hao tena kwa usahihi.

Ni kweli kabisa katika habari za Mitume walwaliotangulia, Muhammad hakuwepo. Bali anayesimulia ni yule aliyewatuma Mitume hao. Sasa wewe Robert unadhani Mwenyezi Mungu aliyewatuma Mitume kufikisha ujumbe kwa waja wake atashindwa kumueleza Mtume wake habari za Mitume hao?
Na si yeye tu Muhammad, bali kila Mtume aliyetumwa alielezwa habari za Mitume wa kabla yake ili watu wake wapate mazingatio.

Soma Sura ya Tatu aya ya 44 yaani Suurat Imraan utambue kwamba habari zote za Mitume waliopita amefunuliwa na Mwenyezi Mungu.

Hii ni katika dalili za wazi pia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hakujua kusoma wala kuandika lakini alitoa habari zilizopita kabla yake. Na utambue kuwa sehemu ya habari hizo alizosimulia ni Mayahudi wasomi wa Taurat ya Mussa walitumia nafasi hiyo kumuuliza Mtume Muhammad baadhi ya mambo yaliyopita ambayo Mtume hakuwepo ilhali wao Mayahudi wanafahamu kupitia kitabu chao cha Taurat.

Walimuuliza ili kumpima kama yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu akamshushia Wahyi juu ya habari hizo ambazo wao Mayahudi wanazifahamu kwakuwa wanazisoma kwenye Taurat. Na majibu ya Muhammad yalisadifu vyema ukweli wa habari hizo.

Mfano wa maswali aliyoulizwa na Mayahudi ili kumpima Muhammad atoe habari zake ilhali hakuwepo wakati huo ni pale alipoulizwa juu ya vijana watatu wa pangoni. Allah akamshushia Wahyi kuwajibu waliomuuliza maswali. Aidha aliulizwa juu ya Dhul-Qarnaini, juu ya Roho na kadhaalika kisha akateremshiwa Wahyi kutoka kwa Mwennyezi Mungu na akajibu kwa fasaha kama tunavyojifunza katika Surah ya 18 Aya ya 83 yaani Suurat Al-Kahf au Sura ya 17 Aya ya 85. Hebu Mr. Robert soma hizo aya upate kujifunza kwanini Muhammad amesimulia habari wakati hakuwa akizijua na wala hakuwepo. Jibu ni jepesi, Qur'an sio maneno yake. Ni maneno ya Allah yaliyopitia kwa Malaika Jibril.

Kwakuwa Muhammad ni Mtume wa mwisho, na wametangulia wengi kabla yake na Qur'an ni kitabu cha mwisho sio ajabu kukuta ndani ya Qur'an habari zote zilizopita za Mitume na watu wao kuelezwa. Zinaelezwa ili watu wajue na wapate mazingatio. Soma Surah ya 23 Aya ya 44 kujua sio tu Muhammad bali kila Mtume aliyetumwa alitoa habari kwa watu wake juu wale waliopita. Na hawakutoa kwa maneno yao bali walifunuliwa na Mwenyezi Mungu.

Sio ajabu Muhammad kupitia Qur'n ameeleza habari za kale ilhali hakuwepo. Iwe ni jibu kwako wewe kuwa huyo Muhammad ni Mtume wa kweli aliyetumwa, anasimulia asiyoyashuhudia kwa usahihi kwa sababu ni Mwenyezi Mungu ndio anamsimulia.

Jibu hilo hapo juu.

Sasa utakuwa unaanza kuelewa. Kama usemavyo kuwa Biblia (japo hili jina la Biblia hata ndani ya hicho kitabu hakuna hilo jina la kitabu kiitwacho Biblia ambacho kilishushwa kwa Yesu) imekusanya vitabu vilivyoshushwa kwa Manabii mbalimbali, Qur'an ni kitabu cha mwisho. Ndani ya Qur'an imeeleza habari za Mitume wote waliotangulia na vitabu vyao. Kisha ikaeleza habari zitakazokuja baadaye mpaka siku ya Qiyama.

Tambua Ewe Robert, Mwenyezi Mungu hakutuma Mtume mpya kwa waja wake mpaka pale waja wanapokengeuka na kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume. Kwenda kinyume ni pamoja na kuasi, kupuuza mafundisho au kubadili maandiko ya vitabu.

Kwa huruma yake Allah humtuma Mtume mwingine abainishe na kusahihisha yale yaliyopotoshwa.

Ndio maana hata Yesu alisema hajaja ili kuitengua Taurat bali kuitimiliza.
Qur'an imebainisha yote yaliyopita na kusahihisha yote yaliyopotoshwa ili kuwaokoa watu na upotevu. Ipo mifano mingi, kwakuwa wewe Robert ni Mkristo unayeamini katika utatu wa Mungu, Qur'an inakusahihisha kwamba usiseme Utatu bali Mwenyezi Mungu ni Mmoja wala hana Utatu. Huo ni upotevu wa wazi ambao ni kinyume na Mafundisho ya Yesu.

Tafadhali, soma Surah ya 5 aya ya 73 yaani Suurat Al Maida. Kwa faida zaidi Mr. Robert soma pia Surah ya 4 aya ya 163 na aya ya 171 yaani Suurat Nisaa. Soma Surah ya 5 aya ya 46 ili upate kubainikiwa.

Aidha, kujua ni kwa namna gani Mafundisho ya Yesu yamebadilishwa na hao unaowasifu ni waandishi wa habari zake akiwemo Paulo, tambua sababu ya kushushwa Qur'an ikiwemo ni kasahihisha yaliyopotoshwa. Kwa faida tu, Aya hii ndani ya Qur'an inawatahadharisha ninyi Wakristo juu ya imani yenu kuwa Yesu ni Mungu.

Nayo ni Surah ya 5 aya ya 116 hadi ya 118 Allah atakavyomuhoji Yesu siku ya Qiyama juu hii imani yenu iliyopotoshwa kwa kumfanua Yesu ni Mungu.
"Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryam! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu!? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifai mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mkubwa wa yaliyofichikana.
Sikuwaambia lolote ila uliyoniamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao. Na uliponifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na wewe ni shahidi juu ya kila kitu.
Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hekima. "

(Surah ya 5 aya ya 116 mpaka aya ya 118).

Upotevu huo ndiyo sababu Muhammad ametumwa kama alivyotumwa Yesu, Mussa, na Mitume wengine kabla yake kuja kusahihisha makosa na upotevu uliosababishwa na watu kubadili maandiko kwa manufaa yao ya kidunia.

Nakusahihisha Robert,
Hao mitume uliowataja hawakiandika vitabu. Mitume wanashushiwa Wahyi yaani Ufunuo ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu.

Tunazungumzia mfano Injili ya Yesu haya sio uandishi wa Yesu. Ni maneno ya Mwenyezi Mungu aliyoshushiwa Yesu na msneno hayo ndio Kitabu cha Injili. Kadhaalika Taurat ya Mussa na Zaburi ya Daud. Ni vitabu ambavyo waandishi sio hao Mitume bali ni mane i ya Mwenyezi Mungu kupitia hao Mitume.

Hakuna aliyesimulia hadith zake mwenyewe wala kujiandikia kitabu chake mwenyewe. Mitume walipewa ufunuo, na mfano wake ndio vitabu kama Zabur, Taurat, Injili na Qur'an.

Muhammad hajashushiwa 'vitabu' bali ameshushiwa 'kitabu' nacho ni Qur'an. Ndani ya Qur'an hakuna kitabu cha Injili, Taurat wala Zabur bali kuna habari zote za Mitume wote waliotumwa kabla yake. Alichokifanya Muhammad hakimo kwenye Qur'an kwa sababu Qur'an si maneno ya Muhammad bali Muhammad ameishi kwa kuifuata na kuifundisha Qur'an kama muongozo kwa watu. Hilo litambue Robert.

Robert,
Elewa pia Mitume wote waliopita kabla ya Muhammad yaani Yesu, Mussa, Zakaria, Yahya, Ibrahim, Ismail, Ishaqa, Yaakub, Lut, Yunus, Nuh na wengineo walitumwa kwa watu maalum. Kama ilivyo Mussa na Yesu wao walitunwa kwa Wana wa Israil pekee.

Muhammad ametumwa kwa watu wote wakiwemo watu wa kitabu (Ahlul Kitabu) yaani hao Mayahudi na Manasara (Wakristo) ambao sehemu kubwa ya mafundisho ya Yesu yamepotoshwa.

Ndio maana ndani ya Qur'an zipo habari za Mayahudi na Manasara na kubainisha upotevu wao. Muhammad anatokana na Waarabu na lugha yake ni kiarabu. Na Qur'an maneno ya Mwenyezi Mungu yameshushwa kwa lugha ya Mtume aliyetumwa ambaye ni Mwarabu.

Shida iko wapi ndugu Robert kama Qur'an imetoa habari za wayahudi kwa kiarabu!? Ama ulitaka Mtume awe Mwarabu halafu azungume kizungu kisha useme "iweje Mtume mwarabu halafu anasema kizungu?

Ah! Taikun wa Fasihi umepatwa na nini?
Ni fasihi gani hiyo unayojivunia nayo kiasi cha kutokujua kuwa suala la kutoa habari fulani ya watu fulani halifungamani na lugha ya mtu?

Mwenyezi Mungu aliyemtuma Mussa au Isa na kuwapa Tuarat na Injil kwa fikra zako atashindwa kumueleza Muhammad juu ya yale waliyopewa mitume wenzie waliopita kabla yake? Masimulizi ya habari za hao mitume waliomtangulia Muhammad sio utunzi wa Muhammad bali ni maneno ya Mwenyezi Mungu akimuhabarisha Muhammad.
Sasa lugha inakuwaje kikwazo hapo?

Kuwa Myahudi na rafiki wa Yesu hakuashirii kuwa ndio ukweli wa anachosema. Kwani Yuda alikuwa nani kwa Yesu?
Anayesema katika Qur'an juu ya namna Maryam mama wa Yesu alivyobashiriwa kumzaa Yesu na mahala alipomzalia sio Muhammad bali anayesema ni Mwenyezi Mungu.
Qur'an si maneno ya Muhammad.

Rafiki wa Yesu hawezi kuwa na maarifa zaidi kumzidi Mwenyezi Mungu, neno la Mwenyezi Mungu ndilo sahihi kuliko neno la Yohana.

Nakusahihisha ndugu Robert,
Suleiman hajafuga majini bali Mwenyezi Mungu alimpa uwezo wa kuwatumikisha atakavyo. Kuku, mbuzi na mbwa ndio unaweza kuwafuga.
Na hii ni kwa kuwa kila Mtume Mwenyezi Mungu alimpa miujiza na karama zake ili kuwa hoja kwa watu wake.

Kama ambavyo Mwenyezi Mungu alivyomfanya Daud na Suleiman kutambua lugha za wadudu, wanyama, ndege. Bali hata upepo pia Suleiman alipewa uwezo wa kuuamrisha. Yesu naye alipewa miujiza ya kuwafufua wafu, kuwaponya viwete na kuzungumza angali mdogo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Habari za Mitume wote waliomtangulia Muhammad hakuzitunga yeye, amefunuliwa na yule aliyewafunulia waliopita kabla yake, yaani Mwenyezi Mungu.

Huo ni upungufu uliomo katika kitabu chako unachokiamini. Pia hakuna Mtume aliyejiandikia hadith zake. Yesu alijiandikia hadith gani? Yesu alipewa Injili ikiwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Injili sio hadith za Yesu alizojiandikia, Iweje useme Suleiman na mwanawe wamejiandikia hadith? Kama kitabu chako ndio kimeandika hivyo basi huo ni upotevu na upungufu mkubwa.

Mwenyezi Mungu aliyewatuma Mussa, Yesu, Ibrahim na mitume wote akiwemo Muhammad ni Mungu mmoja tu. Mungu wa Musa ndio Mungu wa Yesu, Ibrahim, Yaakub na mitume wote na viumbe wote ambaye ndio Mola wa viumbe wote ukiwemo na wewe.

Bali ni ukweli ambao ninyi Wakristo hampendi kuusikia kuwa Yesu sio Mungu, Yesu ni Mtume tu aliyetumwa na wamepita mitume wengi kabla yake. Mitume wote hao kuanzia Nuhu, Ibrahim, Lut, Mussa, Isa mpaka Muhammad wote wametumwa na Nwenyezi Mungu mmoja. Unastaajabu kusikia neno "Allah"?

Wewe Taikun wa Fasihi kwa fasihi yako ya kiswahili huyo Yehova wewe unaita Mungu. Ukienda kwa Mataikun wenzio wa fasihi ya Kiingereza huyo Mungu wanamuita God. Sasa Taikun, Yehova, God na Mungu ni kitu kimoja au ni tofauti!?

Ukinijibu hapo basi hutapata shida kwanini "Allah" ndio Mungu muumba mbigu, ardhi na vilivyomo na ndiye anayepaswa kuab udiwa yeye pekee.

Jibu la hoja hii limejibiwa hapo juu.

Qur'an iko sawa, haijapuyanga kama usemavyo Robert.
Kuanzia Mtume wa Mwanzo Nuhu mpaka wa Mwisho Muhammad, katikati yao wakiwemo Mussa, Yesu, Ibrahim na wengineo wote hawakuwa dini ya Uyahudi. Wote walikuwa ni Waislam.

Pengine Taikun hujui nini maana ya Uislam. Nitakurudisha darasani mahususi ujue maana ya Islam kama dini. Hapa si mahala pake.

Kama unavyidai wewe pamoja na wengine wengi kuwa Qur'an imenakili visa vya biblia, inawezekanaje Mtu (Muhammad) anakili visa wakati Muhammad hakujua kusoma wala kuandika?
Na kitendo cha Mwenyezi Mungu kumleta Mtume Muhammad asiyejua kusoma wala kuandika kina hekima kubwa sana.

Hapana shaka wangesema na hata wewe ungesema Muhammad ameandika mwenyewe maneno haya yaani Qur'an. Sasa angenakili vipi visa viliyoandikwa kwenye vitabu vya mitume waliopita kabla yake ilhali yeye hajui kusoma wala kuandika?

Qur'an haijanakili chochote kutoka kokote. Visa vinavyofanana katika Qur'an na Taurat na Injil sio ajabu kwakuwa vitabu vyote vimetoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mitume wake.

Ndio maana Mayahud walijaribu kumchallenge Muhammad kwa kumuuliza habari za zamani kabisa ambazo Muhammad hakuwepo na habari hizo zimo kwenye Taurat zao Mayahud na Mtume Muhammad hajui kusoma lakini walijibiwa kisawasawa visa hivyo.
Kwakuwa aliyesimulia visa ndani ya Taurat na Injili ndio huyo huyo Mwenyezi Mungu aliyemfunulia Mtume wake Muhammad.

Qur'an chanzo chake sio Biblia Robert.
Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoshushwa kwa Muhammad kupitia Malaika Jubril.

Qur'an imeeleza yote yaliyopita kwa Mitume na watu wao, inaeleza habari ya yatakayokuja baadaye, inabainisha haki na baatili, inatoa mwongozo wa maisha ya bunadamu. Inatoa habari njema kwa wenye kuamini na kutenda mema na inatahadharisha mafikio mabaya kwa watakao kwenda kinyume na muongozo huo.

Qur'an ndio kitabu cha mwisho na muongozo kwa watu wote, kimebainisha wazi habari zote zilizopita za mitume wote. Unataka ziondolewe habari hizo ili ummu huu usipate kutambua yaliyopita kabla yao?

Qur'an imeeleza mpaka yale ambayo yamepotoshwa na watu yaliyoletwa kwenye Injili ya Yesu na Taurat ya Mussa.

Qur'an imetakasika na upotevu, na ndio njia ya sawasawa baada ya Mwenyezi Mungu kumtuma Yesu kwa Mayahudi kisha Mayahudi wakambadilisha Yesu badala Mtume wakamfanya Yesu ndio Mungu! Huu ni upotevu ambao Qur'an imekuja kubainisha ili kuwa katika uongofu.

Qur'an haijaja kukueleza eti tawala za watu zilifuatana vipi. Qur'an ni muongozo kamili wa maisha ya mwanadamu.
Vipi, kwenye Biblia wamezungumzia pia Utawala na Uongozi wa Rais wa Tanzania wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan?
Kwako wewe ungeyakuta haya kwenye Qur'an ndio ungeamini kuwa Qur'an ni kitabu cha Mwenyezi Mungu?

Qur'an hakuna ilichoacha katika kutoa muongozo wa maisha ya mwanadamu. Na nyingi katika hoja zenu zimejibiwa ndani ya Qur'an yenyewe.
Hayo maswali yako mwisho utaishia kuiuliza Qur'an "nyumbani kwangu kuna viti vingapi?" Kisha useme Qur'an imeshindwa kukujibu.

Kwahiyo Taikun wewe kwa Mtazamo wako unaona alipozaliwa Yesu kwenye Mtende huo Mtende ni wa pale Tandale kwa Tumbo? Acha masihara kwenye mambo ya msingi Taikun.

Kwani Yakobo alikuwepo wakati wa Yesu!? Habari za Yakobo Yesu alizitoa wapi? Kama Qur'an imeielezea Taurat na Injil ndani yeke itaacheje kumtaja Yakobo na watoto wake? Soma Surah ya Al Imraan Aya ya 84, Al Baqarah aya 136, An Nisaa aya ya 163 kisha malizia na Al Baqarah aya ya 140 uone sio watoto tu wa Yakobo bali mpaka wajukuu zake wametajwa humo.

Hebu Taikun unapoamua kutoa bandiko la namna kama hii uwe kweli umesoma na umetafiti vya kutosha basi. Vinginevyo unajidhalilisha mbele za watu.

Utaikun wako wa fasihi uko wapi sasa?

Qur'an ina nondo zote, zilizopita na zijazo. Hata zile zilizopita ambazo zimepotoshwa au kufichwa Qur'an imezibanisha. Na imepambanua haki na baatil. Na imekuja kusafisha yote yaliyopotoshwa ambayo Yesu aliyafundisha kisha baadaye yakapotoshwa kwa makusudi. Mojawapo kubwa na baya zaidi ni kumfanya Yesu kuwa ni Mungu wakati yeye ni Mtume tu na mitume wengi wamepita kabla yake.

Utaikon wako ungejikita zaidi kudadavua pale ambapo Yesu mwenyewe anasema kwenye hiyo ambayo ninyi mnaiita Biblia kuwa yeye ametumwa tu, na aliyemtuma ni Mungu. Kisha mkamfanya tena yeye ndio Mungu muabudiwa badala ya kumuabudu yule ambaye amemtuma Yesu kama alivyomtuma Mussa na mitume wengineo.
unaongelea hii Quran iliyokusanywa na kuchapishwa mwaka 1924 nchini misri kwa amri ya mfalme chini ya Al Azhar university? Before 1924 waislam hamkua a standardized book,Saud Arabia wameipitisha mwaka 1986.
 
  • Nzuri
Reactions: 511
  1. Understanding Muhammad, a Psychobiography” by Ali Sina.
  2. “Why I am not a Muslim” by ibn Waraq.
  3. Psychology of Mohammed: Inside the Brain of a Prophet” by Dr. Masud Ansari.
Binadamu hawaishi ujinga mpka unakufa, sasa uchukue kitabu kitukufu upeleke kwa watu wanahukumiana kutokana na haki za ushoga,
Acheni kutafuta kutrend kwa kuusema uslam vibaya (ushirikina tu umewajaa )
Wengine mnatumwa na waganga wenu so angalia kesho yako basi kaa kimya acheni chuki za ajabu
 
Biblia imeshinda kesi.
kwa kuandika kile kilicho shuhudiwa wakati huo.

hoja zote qurani imeshindwa.
mfano.
iliposema Yesu alizaliwa chini ya mtende.
haijaeleza alizaliwa lini
katika nchi gani
mkoa, wilaya, na kijiji gani
wakati huo kulikuwa na mtawala gani
ndugu wa damu walikuwa akina nani nk.
ambayo yote yameandikwa katika Biblia.
Koooort
Chukua Muhamadi peleka jera kwa kueleza mambo ya uwongo.
 
Ni mjinga pekee atamkana Yesu sababu ya hiyo Quran ni Kitabu kimejaa uongo sana

Biblia imeandika kwa kina matukio yanayohusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa vipengele vifuatavyo:

Mahali: Yesu alizaliwa Bethlehemu (Mji mdogo katika Yudea).

Wakati: Kipindi cha utawala wa Mfalme Herode Mkuu (Mathayo 2:1).

Familia: Mama yake ni Maria, na alichumbiwa na Yosefu, mjukuu wa Daudi, mfalme wa zamani.

Shahidi wa Matukio: Wachungaji walishuhudia kuzaliwa kwake na baadaye Mamajusi kutoka Mashariki walithibitisha kwa kumletea zawadi.

Utimilifu wa Unabii: Matukio haya yalitabiriwa miaka mingi kabla katika Agano la Kale (Mika 5:2).

Biblia inaungwa mkono na maandiko ya kihistoria na uthibitisho wa kisayansi:

Nyaraka za Warumi znathibitisha uwepo wa Yesu katika kipindi cha Herode na Pontio Pilato.

Archaeologist wamegundua Bethlehemu na maeneo mengine yaliyotajwa kwenye Biblia.

Qur'an Haina ushahidi wowote wa kihistoria ,archeolojia ,Ni kitabu cha kipropaganda tu

Hoja hii inaimarisha Biblia kwa kusema:

"Biblia ni maandiko yanayoeleza matukio kwa undani wa mahali, wakati, na watu waliokuwepo. Maelezo haya ni ushuhuda wenye nguvu wa kihistoria."
 
Kumbukumbu la Torati 6:14
Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;

Ukitaka kujua majina(proper name/personal name) ya miungu ya mataifa kama Misri, Kanaani, Yordan, Moabu, Waajemi, Wamedi, warumi yote ipo Kwa Majina ninaweza kukutajia with Reference.
Na pia ukitaka kujua mungu wa waarabu nitakutajia achilia mbali huyo Yehova Mungu wa Wayahudi.

Ndio maana watu wote wenye maarifa, ufahamu, elimu na Ujuzi watashangaa wakisikia wakisema Allah akamuambia Musa au Daudi au Yesu ilhali Allah sio Mungu wa Wayahudi. Huo utakuwa ni uongo mkubwa ambao hautavumiliwa.

Au mtu aseme Torati, injili, Zaburi na maandiko yote ya kiyahudi ati yawe yametoka Kwa Allah, huo ni upotoshaji na wanaopotoshwa na watu wasioelimika au walioamua kupotoka.

Au Yehova amuagize Muhammad muarabu yaani huo utakuwa uongo mkubwa
Una elimu kubwa sana

Najifunza mengi kupitia kwako
 
Kwema Wakuu!

Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.

Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?

Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.

Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.

Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.

Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;

1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.

a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.

Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.

Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.

Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.

2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.

Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.

Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.

3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.

Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.

Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.

Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.

4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.

Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?

Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.

Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?

Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.

Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.

5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.

Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.

Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.

6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.

Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.

7. Mtiririko na visa na matukio ya Kihistoria.
Biblia ni kitabu ambacho kimeandikwa Kwa kufuata mtiririko wa visa na matukio unaoleweka. Kuanzia kisa cha Adamu mpaka Yusufu anachosimulia Musa, Kisha tawala za dunia kama Tawala la Nimrodi, kisha tawala la mafarao, kisha tawala la Waashuru na Wakaldayo, kisha wakafuata Waajemi na Wamedi, kisha wakafuata Wayunani/wagiriki, kisha wakafuata Warumi ndipo alipozaliwa Yesu.
Lakini Quran haina mtiririko wa visa na matukio, kumaanisha haiwezi kutumika hata shuleni Kama rejea za kihistoria kuhusu tawala, au mambo ya kuitawala au Kisiasa kwani Quran haijui wapi dunia imetoka ilipo na wapi inapoenda. Wakati Biblia inaeleza wapi Dunia ilipotoka na wapi ilipo na inapokwenda.

Quran inaweza kuulizwa swali, Yesu alizaliwa wakati WA utawala gani na wanani na ukashindwa kujibu?
Kimahakama Quran kama haijui baadhi ya taarifa muhimu kama Zama na Maeneo husika ya tukio lilipotukia haiwezi kutumika kama Rejea au ushahidi muhimu katika mambo ya Kidini.

Kwa mfano; Issa kazaliwa kwenye mtende Kwa mujibu wa Quran lakini haielezi ni eneo gani au nchi gani Issa alizaliwa, hata Hapa Tanzania ipo mitende, hii ni tofauti na Biblia inataja na kuelezea visa katika mtiririko uliokamilika.

8. KUjitosheleza, kujitegemea na kutoa taarifa zote muhimu.
Biblia inajitosheleza na kujitegemea Biblia kuhusisha kitabu kingine. Msomaji yeyote wa Biblia akimaliza kuisoma hatahitaji rejea za kitabu kingine.
Mfano msomaji akisoma kisa cha Yakobo, atajua Yakobo alizaliwa wapi, ndugu yake ni Nani, Routes zake zote, wake zake, watoto wake na umri wake mpaka anakufa. Kwa nini aliitwa Yakobo, ikawaje akabadilishwa jina n.k
Lakini Quran haijitoshelezi haina hizo taarifa muhimu. Hivyo kuifanya Quran kuwa tegemezi Kwa vitabu vingine.

Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Majaji mjadili kwa hoja.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Mwenye Qur'an yake (shetani) anakuangalia tu kwa hasira, anakusubiri kwa hamu akuvalishe mabomu mwilini.
 
Naongezea
9. Muasisi wa Quran yaani Muhamad alikuwa hajui kusoma na kuandika kwahiyo kama msomi ni ngumu kuifanya kama rejea. Mtu ambaye hajui kusoma na kuandika bado tunamchukulia kwenye kundi la wajinga kwasababu maarifa yapo pia kwenye maandishi.
10. Dhana ya kuwa Muhamad alishushiwa Quran halafu akapewa mtu asiyejua kusoma na kuandika bado haileti maana. Kumbuka Mussa alikuwa karibu na Mungu lakini alikuwa anaambiwa aandike mwenyewe amri kuu za Mungu
11. Mungu siyo binadamu anauwezo wa kusikia lugha zote dunia ndiyo maana Biblia inatafsiri za lugha mbalimbali duniani ndiyo maana unaweza kumuomba Yesu kwa kutumia lugha yoyote hata kwa kisukuma, kiarabu, kiajemi, kihindi n.k yaani unaweza kusoma Biblia ya kiingereza lakini ukasali kwa lugha ya kihaya na Mungu akakusikia ila tunapokuja kwa waislamu lugha ni moja tu ambayo ni kiarabu ambapo muarabu yeye hiyo lugha anaielewa vizuri hapati shida ila wengine mpaka wapate watafsiri na lazima usali kwa lugha ya kiarabu. Bila kuswali kwa kutumia lugha ya kiarabu bado hujawasiliana na Allah.
 
Back
Top Bottom