Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Musa aliandika hadi kifo chake hilo linawezekana vp kinyume na kwamba kuna mwaandishi aliyeandika kifo cha Musa?

Ukiambiwa shule muhimu unafikiri wanaosema hivyo ni wajinga?

Musa kabla hajafa soma kwenye kitabu cha Hesabu kinaeleza wazi Mungu alimuambia Amuandae Joshua kuwa mrithi wa kiti chake/kuongoza Israel.
Hivyo alizidisha kumuweka Yoshua Karibu ili amfundishe kazi.

Jibu la swali lako limetokea hapo.

Biblia imeandikwa na watu wenye akili, Wanafalsafa wenye upeo WA juu.
Ndio maana data muhimu karibu zote waliziingiza.

Vipi Quran iliandikwa na watu wa Aina gani?
Kwa maana data muhimu kama asili ya watu, mahali walipozaliwa, routes walizopita, miaka yote walioishi, mahali walipozikwa zote Quran haina hizo data.

Hivyo moja Kwa moja kitabu cha Quran hakiwezi kutumika Kama rejea kuu mahakamani au mahali popote PA maana walipo watu wenye akili za juu
 
Usilamishe tu iwe hivyo ndio maana mwanzo kabisa nilikwambia kuwa hivi ni vitabu vya imani uliyoyaeleza kuhusu biblia ni vitu ambavyo wewe unaamini.

Biblia ni kitabu cha Imani Kwa wenye Imani.
Biblia ni kitabu cha kihistoria Kwa wasomi na wanahistoria.
Biblia ni kitabu cha watawala kwa wanaotaka kutawala kwani watafuatilia Tawala zilizopita humo.

Lakini Quran ni kitabu cha Imani tuu. Kipo limited.
Hamuwezi tumiwa kihistoria, au kiutawala Kwa sababu hakuna Data za maana katika Nyanja hizo.
Sio ajabu watawala wote Duniani hutumia Biblia katika kutoa nukuu zao kurejelea historia Fulani ya Dunia.

Sijui Kama unaelewa logic yangu au unafikiri tunabishania dini hapa.
 
Quran imeangukia pua.

Imepigwa vibaya sana.

Uislmu ni hovyo sanna

Quran ni kweli imepigwa vibaya na kuangukia pua.

Ila sio kweli kuwa uislam ni hovyo.

Uislam ni Dini nzuri Sana lakini kuna mambo madogo madogo ndio umepuyanga.

Ninachowapendea Waislam ni watu wakufuata kile kilichoaandikwa. Hiyo kwangu ni Jambo linalonifanya niwapende na kuwapa heshima.

Ila tatizo walilonalo ni uduni wa elimu kuhusu asili ya kile nilichoandika humo ndani ya Quran ambacho hawajui asili yake kuu imetoka kwenye Maandiko ya kiyahudi.

Waislam Huo ndilo ukweli hawataki kuusikia.
Hapo ndio unawaona Kama akili zao zimefyatuka
 
Hata muundo wa Katiba za Duniani wametoa kwenye. ..BIBLIA

HUMU UTAKUTANA NA AMRI KUMI Kama KATIBA MAMA

Halafu Kuna BY LAWS zipo nyingi

Kuna SHERIA ZA MAADILI

KUNA SHERIA ZA VYAKULA

KUNA SHERIA ZA MAVAZI


KUNA SHERIA ZA KIJAMII


N.k
 


DHAMBI YA ASILI​

Katika Agano la Kale kitabu cha kwanza, kinachoitwa Mwanzo, imo hadithi ya kuumbwa mtu na kuanguka kwake. Hivyo ndivyo inavyosimuliwa alivyoanguka Adam kutokana na kukosa neema:

Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mwanzo 2.15-17

Juu ya hivyo lakini Adam kwa kushawishiwa na mkewe, Hawa, aliasi amri ya Mungu na akala matunda ya mti wa ujuzi aliyokatazwa. Mungu akawalaani wote wawili:

Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, na mavumbini utarudi.

Mwanzo 3.16-19

Kwa ajili ya dhambi yao hiyo, Kanisa linasema, Adamu na Hawa wakakosa neema ya kutakaswa, haki ya kuwapo Mbinguni na vile vipawa vyao mahsusi; ndio ikawa waweza kufa, kuteseka, na kuwa na matamanio makubwa kutenda maovu na wakafukuzwa kutoka bustani ya Paradisio (Firdausi). Kwa sababu ya dhambi ya Adamu wanaadamu wote wakizaliwa wanakosa neema ya utakaso na wanarithi adhabu yake. Hii ndiyo inayoitwa dhambi ya asili.

Thiologia, yaani ilimu ya Ungu, ya Mtakatifu Paulo iliikuza hiyo imani ya Dhambi ya Asili kuthibitisha imani nyengine, yaani imani ya kuokoka kwa kifo cha Yesu msalabani. Katika barua yake aliyowapelekea Warumi Paulo aliandika hivi:
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.

Warumi 5.12-15

Pia vile vile Paulo aliwaandikia Wakorintho:

Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhaalika na katika Kristo wote watahuishwa.

1 Wakorintho 15.22

Paulo anakusudia kusema kuwa wanaadamu wote, wameingia makosani kwa vile Adam alivyovunja amri ya Mwenyezi Mungu, ndio maana ya kufa kwao; mpaka kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo ndiko kumeleta uhai kwa wenye kumuamini kuwa yeye ni Mwana wa Mungu aliyekuja duniani kwa ajili ya kuwaokoa walimwengu kwa kuteswa na kutundikwa msalabani na kufa na kuingia Jahannam na kisha kufufuka na kupaa mbinguni.

Haya ni mafunzo ambayo Paulo amejaribu kufunza katika barua zake. Lakini imani aliyofunza Paulo ya Dhambi ya Asili ya kurithiwa inapingwa na vifungu vingine kutokana na Biblia. Katika Kumbukumbu la Torati, kwa mfano (na hicho ni katika vitabu vitano vinavyohisabiwa kuwa ndiyo Torati inayoaminiwa na Mayahudi na Wakristo) Musa anasema:

Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuwawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.

Kumbukumbu 24.16

Hali kadhaalika tunasoma neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia:

Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi.

Yeremia 31.29-30

Tena Neno la Mungu linaendelea kusema katika kitabu cha Ezekieli kwa uwazi zaidi:

Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi. Roho itendayo dhambi, ndiyo itayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe; haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

Ezekieli 18.19-20

Hayo tuliyoyanukulu kutokana na vitabu vya Yeremia na Ezekieli ni maneno ya Bwana Mungu, na yale yaliyotoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati ni maneno ya Musa, ambaye alileta sharia itokayo kwa Bwana Mungu na ambayo Yesu alisema kuwa yeye hakuja kuitengua hata nukta moja bali amekuja kuitimiza tu. Ni wazi kabisa kuwa nadhariya ya Paulo ya dhambi ya asili ya kurithiwa inagongana na neno la Mungu kama lilivyo katika Biblia. Na haya yametajwa na Mwenyezi Mungu katika Qur'ani:

Au hakuambiwa yaliyomo katika vitabu vya Musa, na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi, ya kwamba habebi mwenye kubeba mzigo wa mwengine? Na ya kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya? Na kwamba amali yake itaonekana?

(Qur'ani) An Najm 53.36-40

Katika Injili pia upo ushahidi ya kuwa Yesu mwenyewe anapinga hiyo nadhariya ya imani ya Dhambi ya Asili, yaani wanaadamu wamerithi dhambi aliyotenda Adam:

Hata (yesu) alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.

Yohana 9.1-3

Neno "Rabi" kama lilivyo hapo juu kuitwa Yesu maana yake kwa lugha ya Kiyahudi ni Maalim au Shekhe, sio kama wanavyotumia Waislamu kuwa ni Mola Mlezi. Hata katika Kiarabu pengine hutumiwa kwa maana ya "bwana", kama kusema: Rabbi lbait, yaani Bwana wa nyumba.

Kinyume na mafunzo ya Kanisa linalojiita kwa jina lake, ya kwamba watoto wote waliozaliwa wamezaliwa katika dhambi, mwenyewe Yesu Kristo anathibitisha kuwa watoto hawana dhambi. Tunaona hayo zaidi katika maneno haya yaliyotajwa katika Injili ya Mathayo:

Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Mathayo 18.2-3

Maana ya maneno hayo ya Yesu ni kuwa vitoto havina dhambi ya kurithi wala yo yote. Kwa hivyo nini linalolazimisha kuwa mtoto hataokoka ila abatizwe?
Au kuwa kila mtu anahesabiwa kuwa ana dhambi mpaka aamini kuwa Mwenyezi Mungu kamgeuza mwanawe wa pekee auliwe kama dhabihu kondoo imwagike damu yake, ndio Mwenyezi Mungu awe radhi na amsamehe huyo mwenye dhambi?
Huyu ni Mungu mwenye rehema na mapenzi kwa viumbe vyake, au ni Mungu aliye katili kwa waja wake na hata kwa mwanawe?
Kwanza awasingizie wanaadamu wote kuwa wana dhambi kwa jambo wasilolitenda, kisha kuwasamehe kwake ni kwa kumwuua mwanawe mwenyewe! Makosa mawili hayafanyi moja lisibu.

Basi tunaona kuwa nadhariya ya imani ya kuwa dhambi hurithiwa iliyoanzishwa na Mt Paulo kama ilivyo katika barua yake ya mwanzo kwa Wakorintho tulionukulu hapo juu, inapingwa na ushahidi wenye nguvu zaidi kutokana na Biblia,

yaani kwa maneno ya Musa yaliyomo katika Kumbukumbu la Torati, na maneno ya Bwana Mungu yaliyomo katika Yeremia na Ezekieli, na maneno ya Yesu kama yaliyomo katika Injili ya Mathayo na Injili ya Yohana.

Lakini wazee wa Kanisa wamehiari kuukataa ushahidi wazi wa kukataa wa Nabii Musa, wa Bwana Mungu, na wa Yesu, uliomo katika Torati na Manabii na Injili, na kufuata badala yake ubishi wa barua za Mt Paulo.
 

Unajua Paulo na Muhammad ni Kama wewe na Mimi tuu?
Unajua maoni na mtazamo wa Muhammad na Paulo hauwezi kubadilisha Torati ya Musa?

Kwa mfano Muhammad kusema Watu waabudu siku ya ijumaa unajua hayo ni maoni yake kutokana na tayari Kwa wakati ule Makureshi walikuwa wanaabudu miungu yao pale Alkaaba katika siku ya ijumaa?
Maana Torati haisemi hivyo.

Kwa hiyo ukisoma maandiko hasa ya Dini tofautisha maoni na mtazamo wao na Katiba ya mungu wao aitwaye Yehova
 
WEWE CHIZI FRESH, UNACHOJIBU NA KILICHOULIZWA NI VITU VIWILI TOFAUTI
 
Huyo jamaa haelewi kitu, ana kopy na kupaste magazeti
 
WEWE CHIZI FRESH, UNACHOJIBU NA KILICHOULIZWA NI VITU VIWILI TOFAUTI


Hakuna Sabato



KWA kushikilia peke yake maelezo yaliyo katika Biblia, katika kitabu cha Kutoka 20:8-11; baadhi ya watu huamini kuwa baada ya siku sita za kuumba kwake vitu vyote, Mungu aliitenga siku iliyofuatia ya saba (sabato) kuwa ni siku tukufu (holiday) na ya ibada.

Aidha, itikadi ya kuadhimisha siku hiyo pia imebeba dhana kwamba Mungu alifanya kazi (ya kuumba) kwa muda wa siku sita na baada ya kuchoka kwa kazi hiyo siku ya saba akapumzika!

Kwa kigezo hicho ndio sasa inaaminiwa na baadhi ya Wakristo kuwa imekuwa ni amri kwa wanadamu wote kwamba kwa muda wa siku sita wafanye kazi na siku ya saba ambayo ndiyo Sabato (Jumamosi) wapumzike na wafanye ibada.

Kwa hali hiyo, kupitia makala hii tutathibitisha kwa maandiko kuwa:
• Nafasi ya kuiadhimisha Sabato kwa wakati tulionao sasa.
• Uhusiano wa Sabato na wasiokuwa Waisraeli.
•Dhana potofu iliyoambatanishwa na Sabato (ya Mungu kuchoka na kumpumzika).
• Siku ambayo wanadamu wanatakiwa wafanye ibada.

Hata hivyo, kabla atujazichambua nukta hizo, ni vyema hapa kwanza tukayarejea maandiko kadhaa yanayoelezea wazi amri ya kuiheshimu na kuishika siku ya Sabato.

Mwenyezi Mungu alisema:

"Ikumbukeni siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato akaitakasa".

Kutoka 20:8-11

Tunachojifunza kufuatana na maandiko hayo juu ni kwamba, pamoja na kuandikwa maelezo ya "kustarehe kwake" siku ya saba baada ya kuumba kwake vitu vyote, amri ya kuitukuza sabato ilitolewa moja kwa moja na mwenyewe Mungu.

Maelezo mengine ya amri hiyo yamerejewa pia katika rejea (reference) za Kutoka 31:12-17 na Kumbukumbu la Torati 5:12-15.

Hilo halina mjadala. pamoja na hivyo, lakini...

Sabato haikuwahusu watu wengine isipokuwa Waisraeli peke yao.

Pamoja na kukiri amri ya kuishika sabato kwamba ilikuwa ni ya Mungu mwenyewe kama tulivyoona hapo juu, maandiko ya Biblia yanaeleza wazi kuwa amri hiyo haikuwa na uhusiano wowote na watu wa mataifa mengine, yasiyokuwa ya Israeli. Lakini iliwahusu tu Waisraeli na vizazi vyao peke yao. Ukweli huu unadhihirishwa na maandiko yafuatayo:

"BWANA akasema na Musa, na kumwambia, kisha nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na nyinyi katika vizazi vyenu vyote, ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi:

"Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika sabato, kuiangalia sana hiyo sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alikufanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika".
Kutoka 31:12-13 na 16-17.

Kwa maandiko hayo, kinachodhihirika hapa ni kwamba hakuna watu wa mataifa mengine waliopewa amri ya kuishika sabato isipokuwa wana wa Israeli na vizazi vyao peke yao. Ambapo maandiko yanaeleza vile vile kwamba sababu ya msingi ya wana wa Israeli kupewa amri ya kuishika sabato ilikuwa ni ishara ya kuonyesha uhusiano wao mwema wa utiifu katika kuheshimu na kufuata amri za Mwenyezi Mungu.

Kisha Mungu alitoa tahadhari kwa Muisraeli atakayevunja Sabato
Baada ya Mungu kuwaamuru wana wa Israeli kuishika sabato, ili kutilia mkazo amri hiyo, aliwatahadharisha kwa kutoa adhabu ya kuuawa kwa yeyote miongoni mwao atakayethubutu japo kwa mzaha kuinajisi (kuivunja) au kufanya kazi yoyote siku ya sabato. Mungu aliwaambia wana wa Israeli:

"Basi mtaishika hiyo sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia najisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi yake itakataliwa mbali na watu wake. Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yoyote katika siku ya sabato, hakika yake atauawa".
Kutoka 31:14-15

Muisraeli mmoja aliuawa kwa kukusanya kuni tu siku ya Sabato!
Ili kuonyesha ulazima wa kutii amri ya kuiheshimu na kuishika sabato na kutotii tahadhari ya kutofanya kazi yoyote siku hiyo, maandiko ya Biblia hayakuacha kumuelezea Muisreli mmoja aliyehukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la kukusanya tu kuni siku ya sabato.
Biblia inasema:
"Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwa jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya sabato. Hao walimwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote. Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa. BWANA akamwambia Musa, mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote wakampiga kwa mawe huko nje ya marago. Basi mkutano wote wakampeleka ya marago, nao wakampiga mawe, akafa; kama BWANA alivyomwagiza Musa".

Hesabu 15:32-36

Kwa ufupi, haya yalikuwa ndio matokeo ya mtu (Muisraeli) anayeivunja sabato. Na ni dhahiri Bwana Yesu alipokuja alilijua hili.

Hata hivyo, uovu ulipokithiri Mungu aliamua kuivunja Sabato

Pamoja na mtu yule kupondwa kwa mawe hadi kufa kwa kosa la kuvunja sabato, hatimaye katika siku za usoni, zama za Nabii Isaya (a.s.), Mungu aliamua mwenyewe kuivunja sabato kutokana na kukithiri kwa maovu, hali iliyopelekea amri za Mungu, ikiwemo ile ya kuheshimu siku ya sabato kuchanganywa na mila na desturi potofu za watu, kiasi kwamba ya Mungu na ya watu hayakutofautishwa.

Ndipo Mungu mwenyewe kupitia Nabii Isaya alipoamua kukata shauri kwa kuwaambia:

"Msilete tena matokeo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano, siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa; nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua".
Isaya 1:13-14

Kufuatana na maandiko hayo juu, imedhihihirika kwamba kwa kuchukizwa mno na maovu ya watu hao, Mungu alifikia kuishutumu sabato kuwa ni sehemu ya "maovu" kama inavyoonekana katika maandiko hayo hapo juu. Na hili Bwana Yesu alipokuja naye alilijua. Na ndio hakuona ulazima wa kuiheshimu tena sabato, kama tutakavyokuja kuona hapo baadae.
 
Huyo jamaa haelewi kitu, ana kopy na kupaste magazeti


Yesu alidhihirisha kuvunjwa kwa Sabato

Biblia inaonyesha maneno na matendo ya Bwana Yesu yalidhihirisha kwamba amri ya kuiheshimu na kuishika siku ya sabato ilikuwa haina nguvu tena kama ilivyokuwa hapo katika siku za kale. Na huu ni uthibitisho mwingine wa wazi kuwa sabato lkuwa imekwishavunjwa.

Maandiko yafuatayo yanayoweka bayana ukweli huu:
"Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenzake? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao? Wala hamkukusoma katika Torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia? Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato".
Mathayo 12:1-8

Tunachojifunza kutokana na maandiko hayo juu ni kwamba tofauti na mtu yule aliyeuliwa kwa kosa la kukusanya kuni siku ya sabato, Bwana Yesu pamoja na kutowakemea kwa kuvunja kwao masuke siku ya sabato, bado anawatetea wanafunzi wake kwa "kosa" hilo tena kwa kulijengea hoja tofauti. Kubwa zaidi anawadharau wale wote wanaowaona kuwa ni wakosaji wale wanaoivunja sabato, pale alipowaambia:
"... kama mngalijua maana yake maneno haya msingeliwalaumu wasio na hatia (waliovunja masuke siku ya sabato)".

Aidha, kauli ya Yesu hapa kwamba "Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato" haina maana nyingine zaidi ya kuonyesha kwamba yeye (Yesu) ndiye anayehusika zaidi na sabato kwa kuwa kwanza yu Muisraeli (Marko 2:27), pili, ilikuwa kielelezo kwa wanadamu wengine, yeye ndiye anayestahiki zaidi kuwa mtu wa kwanza katika kutii amri za Mungu. Kwa maana hiyo, alijua vyema kwamba wakati ule sabato haikuwepo tena. Ndio maana kama tulivyokwishakuona hakuwachukulia hatua wanafunzi wake hatua inayostahiki walipovunja masuke siku ya sabato, kwa kuwa wakati ule kilikuwa tena si kipindi cha "sadaka" bali cha "rehema", kama mwenyewe (Yesu) alivyosema hapo juu.

Zaidi ya kutowachukulia hatua yoyote wanafunzi wake kama alivyoadhibiwa mtu yule wa kuni, Biblia pia inaonyesha kuwa Bwana Yesu aliruhusu siku ya sabato kufanya kazi, kama zile za kuokoa uhai wa viumbe, kama tunavyosoma maandiko yafuatayo:

"Akaondoka huko, akaingia katika sinagogi lao. Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza, wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya mtu siku ya sabato? Wapate kumshitaki. Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa? Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda wema siku ya sabato.Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaonyoosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili".
Mathayo 12:9-12

Ukichunguza kwa makini mafundisho haya ya Bwana Yesu utagundua ukweli kwamba sabato ilikwishavunjwa, kwani kama anavyosema (Yesu) kuwa ni halali kutenda wema siku ya sabato, kukusanya kuni pia na katika mambo mema vile vile, lakini kwa vile zama hizo sabato ilikuwa bado haijavunjwa, mhusika aliadhibiwa kwa kuuawa.

La muhimu kuzingatia hapa ni kwamba "ruhusa" hiyo ya Bwana Yesu ya kufanya kazi siku ya sabato ameitoa wakati ambao yapo yale maandiko yanayoitaja wazi marufuku ya kufanya kazi yoyote siku ya sabato, pia yanatahadharisha Muisraeli atakayevunja sabato kwa kufanya kazi yoyote katika siku hiyo, isitoshe, yanamuelezea mtu yule aliyeuawa kwa kosa la kukusanya kuni tu siku ya sabato. Hii inaonyesha dhahiri kuwa alikuwa akionyesha kuwa amri ya kuishika sabato imekwishafutwa. (Isaya 1:13-14)
 


Kwa hiyo hakuna siku maalum ya ibada


Baada ya kuona Bwana Yesu jinsi alivyoonyesha kutokuwepo tena taadhima ya siku ya sabato, kwa kweli sikukuu hiyo ilibaki kuwa ni historia tu, kama Mungu mwenyewe anavyotukumbusha katika maandiko yafuatayo:

"Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. Mimi ni BWANA, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda, zitakaseni sabato zangu, nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na nyinyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu".

Ezekieli 20:18-20

Hivi ndivyo sabato ilivyosalia. Na baada ya hapo kwa kweli hakuna siku nyingine yoyote ambayo Mungu aliiteua badala ya sabato kuwa ni siku ya mapumziko na ya ibada. Haipo!

Na kwa kweli mwongozo sahihi na ulio wazi juu ya ibada upo katika Qur’an tukufu peke yake ambamo Mwenyezi Mungu anasema:

"Na umuabudu Mola wako mpaka ikufikie hiyo yakini (nayo ni mauti)".

Qur’an 15:99

Hapa haikuwekwa tena siku maalum ya ibada. Maana yake ni kuwa anatakiwa kila mwanadamu katika kila nukta ya uhai wake ajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuwa katika ibada.

Na labda tatizo la msingi lililopo kwa watu wengi ni la kutokuelewa maana sahihi ya ibada na kwa upana wake. Ambapo kimakosa neno hilo wanalihusisha na kuswali (kusali) peke yake. Yaani kwa wengi inapozungumzwa "ibada" hudhania ni "kuswali" tu! Hapana!

Labda jambo ambalo ingepasa watu hawa waelimishwe ni kwamba neno "ibada" siyo neno la Kiswahili. Lakini ni neno la Kiarabu lenye maana kwa Kiswahili ya "kutumika". Na kwa upana wake ni kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu kwa kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake yote. Na kwa hiyo, kuswali ni sehemu ya ibada na siyo ndio ibada yenyewe kamili.

Kwa mantiki hiyo, mtu huhesabika kuwa anaabudu (anafanya ibada) iwapo tu atatenda yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na kuacha yote aliyoyakataza. Na jambo hilo (la ibada) ni lazima kwa muumini wa kweli alifanye kila siku na siyo kwa siku maalum.
 
USIMJIBU, ANATAKA KUPINDISHA MJADALA NA KUANZISHA WAKE , ANGALIA ANACHOFANYA

SASA HIVI KAHAMIA KWENYE SABATO

HUWA NDIO YUPO HIVO WENGI WANAOMJUA HUWA HAWAMJIBU
 
IBADA YA KWANZA YA IJUMAA ,(CHIMBUKO LA IBADA YA IJUMAA)

Ibada ya siku ya ljumaa huelezwa mwanzo
wake katika kitabu kilicho andikwa na
jumuiya ya vijana wa Ki Ansaar.
HISTORlA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)
NA:- MUHAMMAD
ABDALLA RIDAY ANSAAR MUSLIM YOUTH
ORGANISATION
UK. No. 47.


Hebu tuone maelezo mafupi katika ukurasa huo wa kitabu, katika kichwa Kisemacho.

IJUMAA YA KWANZA ALIYOSWALI MTUME.

Mtume aliondoka Qubaa kwenda Yathriba
ilikuwa ni ljumaa, na jua lilipo chomoza alifika katika maskani ya Bani Salim bin Awf ; katika Wangwa wa Ronunaa , hapo ndipo Muhammad aliposwali swala ya ljumaa kwa mara ya kwanza katika Uislam Na huo ni mwaka 622 uitwao mwaka wa
Hijra kwa Waislam (mwanzo wa kalenda ya
Kiislam).

Nini sababu ya Muhammad kusali siku hii na kuanzisha siku hii katika ummah wa kiislam?.

- Mkazo mkubwa wa Ummah wa Kiislam juu ya siku ya ljumaa, unaanzia
katika tukio hilo tu, maandiko ya Qur-an
yanaonyesha wazi kuwa kabla ya hapo
hata Muhammad mwenyewe alikuwa
akifuata kawaida za ibada alizofundishwa na Wayahudi.


- Wayahudi walikuwa na desturi ya kusali kwa kuangalia Yerusalemu, kawaida hii ndiyo iliyotawala maisha ya Muhammad kwa takriban zaidi ya mwaka mmoja na nusu naye alikuwa akiabudu kwa kuangalia Yerusalemu.
(Qur-an 2:144 fafanuzi uk 33

Tukio la mwaka 610 BK ndilo lililoleta mabadiliko makubwa kwa Muhammad, mwaka huo ndio ambao Muhammad alipokea mafunuo yake mapya katika mapango ya Jabal hilaa tofauti za kimafundisho, mwenendo, n.k zilianza kuonekana katika maisha ya Muhammad mara tu baada ya kuanza kupokea mafunuo hayo. (maisha ya Muhamadi uk 16 shekhe Farsy).

- Hilo lilimfanya Muhammad kuanza kupingwa na wayahudi hao, Haswa sababu kuu ni pale Muhammad alipoanza kupinga mafundisho waliyompa kama vile.

~ Kutia mkazo wa Kiibada katika jengo lenye asili ya upagani
Al-Kaaba. Qur-an 22:29 [27:9]

~Kuanza kutangaza imani mpya ya uislam na kuwa na mafundisho
yaliyo onekana kutofautiana na yale ya
kibiblia.
- Kutokana na mafunuo hayo mapya hoja kuu ya Wayahudi ilikuwa ni juu ya mashaka waliyonayo, kuwa mafunuo haya ya Muhammadi hayakuwa ya kweli, Aya ifuatayo ya Qur-an maonyesha hilo.
Qur-an Al-Baarah 2:97 Ufafanuzi uk 24 aya 97

hapa wayahudi wanampinga Malaika Jibril
amhaye ndiye aliyeleta mafunuo hayo kwa Muhammad.

Ibada ya IJUMAA inatokana na ugomvi wa
Wayahudi na Muhammad.
- Kutokana na hali hiyo mahusiano baina ya
Muhammad na Wayahudi yaliharibika,
Fuatilia katika aya zifuatazo:-

Qur-an 5_:82 Maadui wa Uislam ni Wayahudi

Qur-an 2:I04 [Ufafanuzi] Wayuhudi
walihitirafiana na Muhammad na kurushiana maneno.

Tangu hapo Muhammad hakupenda kamwe kuwiana na kile
wanachofanya wayahudi katika mifumo ya kidini, na ndipo anaitangaza rasmi siku ya ljumaa kama siku ya sala katika Ummah wa Kiislam wakati huo akiwa Yathrib (Madina),

- Lakini pamoja na hayo Muhammad hakuipa siku hii nafasi ya Sabato
yaani siku ya 7 ya juma (Jumamosi)
ambayo ndiyo haswa iliyo siku ya Ibada ya kweli kama QURAN INAVYOKIRI

- Kumbuka siku ile ya kweli ya Ibada
ilitengwa na Mungu yote iwe
siku ya ibada tu na si kufanya kazi
yeyote ya kimaisha.
(Qur-an 7 : 163 Kutoka 20 : 8 )

- Siku ya ljumaa haikutolewa ili kushika
mahala pa Jumamosi [Sabato] maana
pamoja na kufanya ibada Muhammad
anaruhusu Waislam kufanya kazi siku hiyo mara baada ya swala, hebu tuone-

Qur-an 62:9-10 Enyi mlioamini Kukiadhiniwa kwa ajili ya sala siku ya ljumaa, enendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara kufanya hivi ni bora kwenu ikiwa mnajua basi fanyeni, Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika
ardhi mtafute fadhira……

hivyo ndivyo Muhammadi alivyoeleza juu ya siku hii ya ljumaa, kamwe siyo siku ya mapumziko kama ilivyo Sabato(Jumamosi) zaidi ya yote ljumaa
si siku yenye mkazo wa kiibada kama
ilivyo Sabato (Jumamosi).

Katikabmafunuo ya Qur-an.
- Siku hii ya ljumaa ni siku ya ibada ya
kawaida tu inayo ambatana na kufanya
kazi za kutafuta kipato, hilo linaifanya
kuwa na tofauti ya mbali sana na siku
ya kweli ya Ibada ya Jumamosi.

EWE MWISLAMU NJOO KWA YESU UFATE IBADA YA KWELI YA SIKU YA SABATO.

YESU ANASEMA

na kondoo wengine ninao ambao sio wa zizi hili .
 
YESU ALITABIRI KUENDELEA KUTUNZWA SABATO MIAKA YA MBELE

Mathayo 24:20 “Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.”

Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Danieli lilikuwa ni kuangamizwa kwa hekalu la Yerusalemu. Danieli (9:27) alitabiri kwamba: “Naye (Masihi) atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.”

Kwamba baada ya Masihi kuuwawa msalabani, angeikomesha sadaka na dhabihu, yaani, angekomesha utoaji wa kafara ya mnyama kwa ajili ya dhambi. Kisha mahali pake, yaani, Yerusalemu, lingesimama chukizo la uharibifu, na ghadhabu kumwagwa juu yake, kwa sababu Wayahudi walikuwa wamemkataa Mwana wa Mungu. Chukizo la uharibifu lilisimama mwaka 66 BK; ambapo Wakristo waliitambua ishara na wakakimbilia milimani, kisha ghadhabu yenyewe ilimwagwa katika mwaka 70 BK; ambapo hekalu na mji wa Yerusalemu viliharibiwa kabisa kama Yesu alivyokuwa ametabiri kwamba halitasalia jiwe juu ya jiwe katika hekalu la Yerusalemu.

Mathayo 24:1-2 “Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.”

“Mnamo 66BK wakati Cestius alipokuja dhidi ya mji [wa Yerusalemu], lakini bila kuelezeka alirudi nyuma, Wakristo waliigundua ishara iliyokuwa imetabiriwa na Kristo na kukimbia wakati Wayahudi 1,100,000 ilisemekana waliuwawa katika maangamizi ya kutisha ya mwaka 70BK.” –(Eusebius, Church History, book 3, chap. 5).
 
Huyo jamaa haelewi kitu, ana kopy na kupaste magazeti


Mungu wa kweli kamwe hana sifa ya kuchoka


Kwa bahati mbaya tumeona katika Biblia kuna mgongano mkubwa na wa kimsingi wa maandiko yake mengi. Miongoni mwa hayo ni kuhusiana na dhana ya Mungu kufanya kazi akachoka akahitaji kupumzika siku ya sabato, kama tulivyoona katika utangulizi wa makala hii.

Hata hivyo, kwa upande mwingine zipo shuhuda nyingine nyingi katika Biblia zinazoonyesha kuwa Mungu kamwe hana sifa kama hiyo (ya kuchoka na kupumzika). Shuhuda mojawapo ni kama ile iliyothibitishwa na Nabii Isaya (a.s.) kwamba:

"Je! Wewe hukujua, hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA Muumba miisho ya dunia, hazimii, HACHOKI, akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo".
Isaya 40:28-29

Kwa shuhuda hizi, Nabii Isaya (a.s.) anakanusha kata kata Mungu kuwa na sifa yoyote ya kuchoka hata kupumzika (astarehe). Lakini yeye ndiye huwapa nguvu wale wasiokuwa na uwezo wa kukabiliana au kuhimili msukosuko wowote.
Na ndio maana katika Qur’an tukufu mwenyewe Mwenyezi Mungu akatilia mkazo kwamba:

"Na tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao katika nyakati sita, wala hayakutugusa machovu".
Qur’an 50:38

Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu mwenyewe katika Qur’an tukufu anakanusha vikali dhana ya kwamba alipumzika siku ya saba baada ya kuumba kwake vitu vyote. Aidha, hiyo pia Mwenyezi Mungu anaipinga kwa hoja zake zifuatazo:

"Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawa sawa?"
Isaya 46:5
 
ACHA KUMSINGIAZIA YESU ,ACHA KUMZULIA UONGO

YESU alikataa kwamba alikuja kuzitangua sheria za Mungu ikiwemo Sabato,

Mathayo.5:17,18 “msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”


Yesu alisema hata mbingu zitakapoondoka nukta ya amri zake haitaondoka.


Mitume nao wakiongozwa na Paulo baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu walikuwa na Desturi kama ya Yesu ya kupumzika siku ya Sabato, Matendo.17:2 “Na Paulo kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko Sabato tatu,” Hivyo hapa tunaona Paulo akiwa na desturi kama ya Yesu kwenda katika nyumba ya ibada siku ya Jumamosi, akitoa hoja toka katika neno la MUNGU Matemdo.18:4. Biblia inasema pia, Matendo.16:13 “Siku ya Sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.” Mafungu haya yanaonesha Sabato ilivyotunzwa baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu (Luk.23:54-56, Matendo.13:14,27,43-44; 15:21; 18:4)
 
UNAKOPI KOPI NA KUBANDIKA MADA TU

NAKU IGNORE RAMSI
 


Kwa hiyo hakuna siku maalum ya ibada


Baada ya kuona Bwana Yesu jinsi alivyoonyesha kutokuwepo tena taadhima ya siku ya sabato, kwa kweli sikukuu hiyo ilibaki kuwa ni historia tu, kama Mungu mwenyewe anavyotukumbusha katika maandiko yafuatayo:


"Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. Mimi ni BWANA, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda, zitakaseni sabato zangu, nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na nyinyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu".

Ezekieli 20:18-20


Hivi ndivyo sabato ilivyosalia. Na baada ya hapo kwa kweli hakuna siku nyingine yoyote ambayo Mungu aliiteua badala ya sabato kuwa ni siku ya mapumziko na ya ibada. Haipo!

Na kwa kweli mwongozo sahihi na ulio wazi juu ya ibada upo katika Qur’an tukufu peke yake ambamo Mwenyezi Mungu anasema:

"Na umuabudu Mola wako mpaka ikufikie hiyo yakini (nayo ni mauti)".
Qur’an 15:99

Hapa haikuwekwa tena siku maalum ya ibada. Maana yake ni kuwa anatakiwa kila mwanadamu katika kila nukta ya uhai wake ajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuwa katika ibada.
Na labda tatizo la msingi lililopo kwa watu wengi ni la kutokuelewa maana sahihi ya ibada na kwa upana wake. Ambapo kimakosa neno hilo wanalihusisha na kuswali (kusali) peke yake. Yaani kwa wengi inapozungumzwa "ibada" hudhania ni "kuswali" tu! Hapana!

Labda jambo ambalo ingepasa watu hawa waelimishwe ni kwamba neno "ibada" siyo neno la Kiswahili. Lakini ni neno la Kiarabu lenye maana kwa Kiswahili ya "kutumika". Na kwa upana wake ni kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu kwa kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake yote. Na kwa hiyo, kuswali ni sehemu ya ibada na siyo ndio ibada yenyewe kamili.

Kwa mantiki hiyo, mtu huhesabika kuwa anaabudu (anafanya ibada) iwapo tu atatenda yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na kuacha yote aliyoyakataza. Na jambo hilo (la ibada) ni lazima kwa muumini wa kweli alifanye kila siku na siyo kwa siku maalum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…