Ukiambiwa shule muhimu unafikiri wanaosema hivyo ni wajinga?
Musa kabla hajafa soma kwenye kitabu cha Hesabu kinaeleza wazi Mungu alimuambia Amuandae Joshua kuwa mrithi wa kiti chake/kuongoza Israel.
Hivyo alizidisha kumuweka Yoshua Karibu ili amfundishe kazi.
Jibu la swali lako limetokea hapo.
Biblia imeandikwa na watu wenye akili, Wanafalsafa wenye upeo WA juu.
Ndio maana data muhimu karibu zote waliziingiza.
Vipi Quran iliandikwa na watu wa Aina gani?
Kwa maana data muhimu kama asili ya watu, mahali walipozaliwa, routes walizopita, miaka yote walioishi, mahali walipozikwa zote Quran haina hizo data.
Hivyo moja Kwa moja kitabu cha Quran hakiwezi kutumika Kama rejea kuu mahakamani au mahali popote PA maana walipo watu wenye akili za juu
DHAMBI YA ASILI
Katika Agano la Kale kitabu cha kwanza, kinachoitwa Mwanzo, imo hadithi ya kuumbwa mtu na kuanguka kwake. Hivyo ndivyo inavyosimuliwa alivyoanguka Adam kutokana na kukosa neema:
Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 2.15-17
Juu ya hivyo lakini Adam kwa kushawishiwa na mkewe, Hawa, aliasi amri ya Mungu na akala matunda ya mti wa ujuzi aliyokatazwa. Mungu akawalaani wote wawili:
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, na mavumbini utarudi.
Mwanzo 3.16-19
Kwa ajili ya dhambi yao hiyo, Kanisa linasema, Adamu na Hawa wakakosa neema ya kutakaswa, haki ya kuwapo Mbinguni na vile vipawa vyao mahsusi; ndio ikawa waweza kufa, kuteseka, na kuwa na matamanio makubwa kutenda maovu na wakafukuzwa kutoka bustani ya Paradisio (Firdausi). Kwa sababu ya dhambi ya Adamu wanaadamu wote wakizaliwa wanakosa neema ya utakaso na wanarithi adhabu yake. Hii ndiyo inayoitwa dhambi ya asili.
Thiologia, yaani ilimu ya Ungu, ya Mtakatifu Paulo iliikuza hiyo imani ya Dhambi ya Asili kuthibitisha imani nyengine, yaani imani ya kuokoka kwa kifo cha Yesu msalabani. Katika barua yake aliyowapelekea Warumi Paulo aliandika hivi:
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
Warumi 5.12-15
Pia vile vile Paulo aliwaandikia Wakorintho:
Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhaalika na katika Kristo wote watahuishwa.
1 Wakorintho 15.22
Paulo anakusudia kusema kuwa wanaadamu wote, wameingia makosani kwa vile Adam alivyovunja amri ya Mwenyezi Mungu, ndio maana ya kufa kwao; mpaka kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo ndiko kumeleta uhai kwa wenye kumuamini kuwa yeye ni Mwana wa Mungu aliyekuja duniani kwa ajili ya kuwaokoa walimwengu kwa kuteswa na kutundikwa msalabani na kufa na kuingia Jahannam na kisha kufufuka na kupaa mbinguni.
Haya ni mafunzo ambayo Paulo amejaribu kufunza katika barua zake. Lakini imani aliyofunza Paulo ya Dhambi ya Asili ya kurithiwa inapingwa na vifungu vingine kutokana na Biblia. Katika Kumbukumbu la Torati, kwa mfano (na hicho ni katika vitabu vitano vinavyohisabiwa kuwa ndiyo Torati inayoaminiwa na Mayahudi na Wakristo) Musa anasema:
Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuwawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.
Kumbukumbu 24.16
Hali kadhaalika tunasoma neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia:
Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi.
Yeremia 31.29-30
Tena Neno la Mungu linaendelea kusema katika kitabu cha Ezekieli kwa uwazi zaidi:
Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi. Roho itendayo dhambi, ndiyo itayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe; haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
Ezekieli 18.19-20
Hayo tuliyoyanukulu kutokana na vitabu vya Yeremia na Ezekieli ni maneno ya Bwana Mungu, na yale yaliyotoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati ni maneno ya Musa, ambaye alileta sharia itokayo kwa Bwana Mungu na ambayo Yesu alisema kuwa yeye hakuja kuitengua hata nukta moja bali amekuja kuitimiza tu. Ni wazi kabisa kuwa nadhariya ya Paulo ya dhambi ya asili ya kurithiwa inagongana na neno la Mungu kama lilivyo katika Biblia. Na haya yametajwa na Mwenyezi Mungu katika Qur'ani:
Au hakuambiwa yaliyomo katika vitabu vya Musa, na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi, ya kwamba habebi mwenye kubeba mzigo wa mwengine? Na ya kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya? Na kwamba amali yake itaonekana?
(Qur'ani) An Najm 53.36-40
Katika Injili pia upo ushahidi ya kuwa Yesu mwenyewe anapinga hiyo nadhariya ya imani ya Dhambi ya Asili, yaani wanaadamu wamerithi dhambi aliyotenda Adam:
Hata (yesu) alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
Yohana 9.1-3
Neno "
Rabi" kama lilivyo hapo juu kuitwa Yesu maana yake kwa lugha ya Kiyahudi ni Maalim au Shekhe, sio kama wanavyotumia Waislamu kuwa ni Mola Mlezi. Hata katika Kiarabu pengine hutumiwa kwa maana ya "bwana", kama kusema:
Rabbi lbait, yaani Bwana wa nyumba.
Kinyume na mafunzo ya Kanisa linalojiita kwa jina lake, ya kwamba watoto wote waliozaliwa wamezaliwa katika dhambi, mwenyewe Yesu Kristo anathibitisha kuwa watoto hawana dhambi. Tunaona hayo zaidi katika maneno haya yaliyotajwa katika Injili ya Mathayo:
Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 18.2-3
Maana ya maneno hayo ya Yesu ni kuwa vitoto havina dhambi ya kurithi wala yo yote. Kwa hivyo nini linalolazimisha kuwa mtoto hataokoka ila abatizwe?
Au kuwa kila mtu anahesabiwa kuwa ana dhambi mpaka aamini kuwa Mwenyezi Mungu kamgeuza mwanawe wa pekee auliwe kama dhabihu kondoo imwagike damu yake, ndio Mwenyezi Mungu awe radhi na amsamehe huyo mwenye dhambi?
Huyu ni Mungu mwenye rehema na mapenzi kwa viumbe vyake, au ni Mungu aliye katili kwa waja wake na hata kwa mwanawe?
Kwanza awasingizie wanaadamu wote kuwa wana dhambi kwa jambo wasilolitenda, kisha kuwasamehe kwake ni kwa kumwuua mwanawe mwenyewe! Makosa mawili hayafanyi moja lisibu.
Basi tunaona kuwa nadhariya ya imani ya kuwa dhambi hurithiwa iliyoanzishwa na Mt Paulo kama ilivyo katika barua yake ya mwanzo kwa Wakorintho tulionukulu hapo juu, inapingwa na ushahidi wenye nguvu zaidi kutokana na Biblia,
yaani kwa maneno ya Musa yaliyomo katika Kumbukumbu la Torati, na maneno ya Bwana Mungu yaliyomo katika Yeremia na Ezekieli, na maneno ya Yesu kama yaliyomo katika Injili ya Mathayo na Injili ya Yohana.
Lakini wazee wa Kanisa wamehiari kuukataa ushahidi wazi wa kukataa wa Nabii Musa, wa Bwana Mungu, na wa Yesu, uliomo katika Torati na Manabii na Injili, na kufuata badala yake ubishi wa barua za Mt Paulo.