Mpaka Mtume anakufa Qur'an ilikuwa teyari ishakamilika watu waliihifadhi kichwani na wengine waliandika kwenye mawe huko lakini ilikuwa teyari, kilifanyika baadaye ni kuikusanya sehemu moja na kuandikwa hivyo hakukuwa na huo uchaguzi wa sura ipi tuamuwe tuiweke na ipi tusiweke. Ila kwenye kuunda kitabu cha biblia watu walikaa na kuamua kuchagua kipi kiwepo kwenye biblia na kipi kisiwepo na kuweka na mambo mengine halafu wewe unakuja kusema et Yesu alisoma hicho kitabu!
Nipe maandiko nukuu hata kwenye Quran hayo maelezo yako. Kwamba Quran ilikuwa tayari Muhammad kuwa hai.
Alafu ukimqliza, msikilize Yesu akisoma chuo cha Nabii Isaya;
Luka 4:17
Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
Luka 4:18
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Luka 4:19
Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
Luka 4:20
Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
Maandiko yenyewe ya Isaya ni haya
Isaya 61:1
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Isaya 61:2
Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Ukiwa mahakamani Unatakiwa uwe na vielelezo vinavyothibitisha maneno yako.
Yesu alisoma Biblia, na wewe mwenyewe umejionea.
Sasa nitakuuliza swali,
Kitabu/chuo cha Nabii isaya hakipo kwenye Biblia au kipo?