Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Kama Biblia na Quran zingeletwa Mahakamani zithibitishe yaliyomo ndani yake, Quran ingeangukia pua

Ukisikiliza watu wanavyosisitiza wanasema ”allah ni mmoja tu” tena kwa ishara ya kidole kimoja ila in reality ukisoma kwenye kitabu au hao hao wanaosema alah ni mmoja watakuambia kwa wingi!!!

Unaweza kuniambia huu ”WINGI” unatokana na nini?

Nb:hiyo para ya mwisho kwenye bold,hiyo lugha ya hovyo mtoto wa kiume usipende kuitumia kwenye mijadala ya watu timamu inakuonyesha una kiwango gani cha ustaarabu!it's disgusting!
Umesikia au umesoma mahali iyo Allah kwa wingi? Ndio nasikia kwako .
 
Bora umesema ukweli ,,,na ukweli humuweka mtu huru,,sisi kwetu huku unaweza kuhoji kila Jambo na ukapewa majibu....kiongozi wa dini na waumini wote Ni sawa ,,hakuna mkubwa zaidi ya Muumba...pia tunapeana nasaha juu ya kutenda wema kwhy Ni juu ya mtu mwenyewe kufuata...akifa Bado tutamzika Kama km muislam hata km alikuwa Cha pombe...

Sadaka yangu ninayoitoa lazma nijue inapokwenda na matumizi yake yawe yanaeleweka ....lkn kutoa hatulazimishwi ....


Ukija kwenye mambo ya ndoa mahali Ni simpo na mke ndio anaruhusiwa kumtoza mahari hooneymoon wake...Tena waelewane wenyewe wawili kwa upendo....hata muoaji asipokuwa nacho kitu ndoa ruksa....

Hayo na mengine mengi utayapata ktk uislamu tu...
Hata kama huko kuna kwenu kuna maelezo ya kutosha ukihoji unajibiwa bado kuna mambo ya ajabu kupitiliza kuliko ukristu. Hata kwa bunduki siendi kwenye uislam.
 
Kwema Wakuu!

Kutokana na mjadala fulani uliokuwa unaendelea katika Jukwaa la Intelligence nimeona nianzishe uzi huu kwa lengo la kujifunza na kuweka mjadala huru. Pia kupima katika mizania ya kimahakama/kuthibitisha ukweli wa masimulizi yaliyomo kwenye Biblia na kwenye Quran.

Nani mkweli na nani muongo kati ya Biblia na Quran?

Sipo hapa kumfanya yeyote awe sijui Mkristo au Muislam au Myahudi, bali nipo kujadili nani mkweli kati ya Biblia na Quran katika mizani ya kimahakama, majaji mtakuwa ninyi wasomaji.

Mahakamani siyo kila kesi inayopelekwa mahakamani ni kesi ya uvunjifu wa sheria, hasha! Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki.

Hivyo hata Biblia na Quran vinaweza pelekwa mahakamani na ukweli ukajulikana tuu. Sema kwa vile mambo haya yanagusa imani za watu jambo hilo linaweza kuwa gumu.

Zifuatazo ni hoja kwa nini Biblia ni kitabu cha kweli na kinapaswa kuwa rejea kuu zaidi ya Quran, kwa sababu;

1. Biblia kwa sehemu kubwa haina maneno ya 'Hearsay' wakati Quran kwa 90% maneno yake ni 'Hearsay'. Kimahakama maneno ya 'hearsay' hayasikilizwi na hayawezi kuchukuliwa kama ushahidi mzito, au kama rejea muhimu. Hoja hii ndiyo hoja nzito kuliko zote zinazoifanya Biblia kiwe kitabu kikuu chakweli kinachoiacha Quran Kwa mbali Sana.

a) Waandishi wengi wa Biblia wanaandika matukio yaliyokuwa yanawatokea wao wenyewe. Mfano Musa anasimulia jinsi anavyowatoa Waisrael Misri kwenda Kanaani, Daudi anasimulia hekaheka zake, Suleiman, Daniel, Yona n.k.

Wakati msimuliaji wa Quran yeye anasimulia habari ambazo yeye hakuwepo. Mfano Muhammad, anasimulia habari za Musa ambaye hayupo na ni miaka zaidi ya elfu iliyopita. Muhammad hajawahi kumuona Musa wala Daudi, wala Suleiman wala Yesu.

Kisa cha Yesu ndani ya Biblia tunaweza kukikubali kwa sababu kiliandikwa na baadhi ya wanafunzi wake akiwepo Marko, Mathayo na Yohana. Hivyo hata mahakamani tunaweza watumia watu waliyoshuhudia matukio ya Yesu aliyoyafanya. Ila tunaweza kukitoa kitabu cha Luka kwa sababu yeye alisimuliwa.

Hata hivyo ulikuwa ni wakati ule ule hivyo naye anaweza akasimulia kitu kikaeleweka. Tofauti na Quran ya Muhammad ambayo inasimulia tukio ambalo ni miaka zaidi ya 500 tangu litokee na anayeandika hajawahi mshuhudia huyo Yesu/Issa.

2. Waandishi wa Biblia walikuwepo maeneo tajwa kwenye Biblia, lakini Quran aliyeandika hajawahi kufika maeneo anayoyasimulia. Yaani Muhammad anasimulia habari za Israel na Waisrael ambapo hajawahi kufika, hajui pakoje, hajui watu wake wakoje.

Muhammad anasimulia habari za Jerusalem ya Suleiman halafu hajawahi kufika Jerusalem na hajawahi kumuona Suleiman, wakati Suleima mwenyewe kaandika habari zake mwenyewe. Kumbuka kutoka Suleiman mpaka Muhammad ni zaidi ya miaka 1000.

Quran kisheria hakiwezi kutumika kama rejea kwa maana msimuliaji anasimulia habari za eneo ambalo hajawahi kufika wala kushuhudia. Wala wakati matukio yanatokea hakuwepo.

3. Biblia ni muunganiko wa vitabu vingi vilivyoshushwa kwa manabii tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti, wakati Quran licha ya kuwa na vitabu vingi lakini vitabu vyote ameshushiwa Muhammad.

Embu shangaa, kisa cha Adamu kashushiwa Muhammad, kisa cha Nuhu kashushiwa Muhammad, kisa cha Ibrahimu kashushiwa Muhammad, kisa cha Yakobo na Yusufu kashushiwa Muhammad, kisa cha Waisrael kashushiwa Muhammad, mpaka kisa cha Yesu. Na visa vyote hakuwepo!😀😀

Upande wa Biblia
Ila wenzake Kisa cha Musa aliandika mwenyewe Musa, kisa cha Ayubu aliandika mwenyewe Ayubu, kisa cha Daudi aliandika Daudi mwenyewe, Kisa cha Yona kaandika Yona mwenyewe, kisa cha Yesu waliandika watu wake wakaribu (wanafunzi waliomshuhudia), kisa cha Daniel kaandika Daniel mwenyewe.

Vitabu hivi ni ushahidi wa wazi kwasababu wanaosimulia ni wahusika wenyewe. Ni kama vile kitabu cha Mzee wetu Mwinyi au Mzee wetu Mengi.

Muhammad kashushiwa vitabu ambavyo anasimulia hadithi za kusimuliwa (Hearsay), kitu pekee ambacho Quran inaweza kuwa ukweli na ikachukuliwa kama ukweli ni masimulizi ya kile alichokifanya Muhammad kwani alikuwepo na anasimulia tukio linaloendelea au alilolifanya.

4. Biblia imeandikwa na Wayahudi kwa kiasi kikubwa na wanasimulia habari zao wenyewe. Lakini Quran imeandikwa na Waarabu kwa lugha ya Kiarabu lakini inasimulia habari za wasiyo Waarabu, inasimulia habari za watu wengine ambao hawakuwaona.

Yaani mimi Mpare wa zama hizi nisimulie mambo ya Wasukuma ya kale ambayo sikuwepo. Hivi ninyi mtanisikiliza mimi Mpare ninayesimulia habari za kale za Wasukuma au mtasikiliza Wasukuma wenyewe?

Muhammad Muarabu aliyezaliwa Makka na akafia Madina hajawahi kufika Jerusalem, hajui hata Rama, Bethlehemu alipozaliwa Kristo halafu yeye anakwambia alizaliwa kwenye mtende halafu kuna mtu Myahudi aliyekuwa rafiki wa Yesu anakuambia Yesu rafiki yake kazaliwa kwenye hori la ng'ombe.

Huyo Rafiki wa Yesu Yohana, ni Myahudi mwenzake Yesu, anapajua Bethlehem, anapajua Jerusalem ndani nje. Je utamsikiliza nani?

Haya Quran na hadithi za Kiyahudi kama anavyosimulia Mtume na maswahaba wake wanakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini. Kumbuka huyo Muhammad anasimulia habari za watu wa taifa jingine ambao wanatofautiana lugha na tamaduni, hajawahi kufika Jerusalem mji wa Daudi na mwanaye Suleiman, hajui Kiyahudi, haabudu dini ya Wayahudi anayoabudu Suleiman.

Anakuambia Suleiman alikuwa anafuga majini, lakini Suleiman mwenyewe katika hadithi zake au hadithi za mwanaye Yerobohamu hajawahi kusema kitu kama hicho. Pia utamaduni wao hauruhusu kufuga madudu hayo majini. Wewe utamuamini huyo Muhammad au utamuamini Suleiman mwenyewe aliyeandika katika vitabu vyake vilivyopo katika Biblia? Jibu utabaki nalo.

5. Mungu wa kwenye Biblia ni Jehova/Yahwe ambaye ni Mungu wa Waisrael wanaosimuliwa ndani ya kitabu hicho. Lakini Quran mungu wake ni Allah, Mungu wa Waarabu wa kabila la Wakurdi wa zamani lakini cha ajabu huyo Allah, ati huyo Allah kuna sehemu anamuagiza kina Musa (Myahudi na dini yake Uyahudi) wakati kimsingi Musa Mungu wake ni Yahweh mpaka anakufa.

Hata hivi leo Mungu wa Wayahudi hajabadilika ni Yahwe na mpaka hivi Mungu wa waarabu hajabadilika ni yule yule Allah. Lakini Quran inapotosha kuwa Mungu anayewaagiza Wayahudi ni Allah hii ni kutokana muandishi wa Quran alikuwa Muarabu.

Wahusika kuanzia kwa Yakobo mpaka kwa Yesu ni Wayahudi na dini yao ni Uyahudi na Mungu wao ni Yahweh, lakini Quran imepuyanga katika eneo hilo.

6. Biblia imetangulia miaka mingi kabla ya Quran. Hivyo kwa kuwahi imeshuhudia na inaweza kusimulia matukio yaliyotokea zamani zaidi kuliko Quran, siyo ajabu Quran yenyewe ndiyo imenakili baadhi ya visa ingawaje inajimilikisha.

Biblia inaweza kujitegemea bila ya uwepo wa Quran kwani yenyewe ndiyo baba/chanzo cha Quran. Lakini Quran kama ukitoa visa ilivyovinakili kutoka kwenye Biblia na maandiko yote ya Kiyahudi basi Quran inabaki bila ya nguvu yoyote Ile.

Quran ambacho ingefanya ni kutoa nondo kuanzia wakati wa Muhammad kuja mbele na siyo kurudia hadithi zilizokwisha kuwepo. Mbona Injili haujarudia visa? Quran haiwezi kuchukuliwa kama rejea kuu kuzidi Biblia kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Majaji mjadili kwa hoja.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Nukuu

"Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki"

Tuende hivyo hivyo na tumuulize jaji iwapo atapokea ushahidi wa Quran ulioleta.

Jaji anaingia mahakamani.

Quran kama mshitakiwa anaanza kujenga hoja.

(AL - MAIDA - 116)
Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu(YESU)! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.


Suali; anaulizwa Mshitaki.

Ni wapi yesu kasema "Mimi Yesu, Mimi Mungu.

Jibu kwa kutumia matukio yaliyotokea
 
Kwa
Hata kama huko kuna kwenu kuna maelezo ya kutosha ukihoji unajibiwa bado kuna mambo ya ajabu kupitiliza kuliko ukristu. Hata kwa bunduki siendi kwenye uislam.
Kwa sababu umezaliwa katika ukristo
 
ANDIKO NDANI YA BIBLIA YENYEWE... NDILO LINALOHITAJI... SIO BLAA BLAA HIZO...
17 Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Maandiko haya Matakatifu yana maana gani basi? Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!
Soma pia Luka 4 yote.

2 Timotheo 3:16
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

Alafu kamalizie Joshua 1:1-12
 
Kwa

Kwa sababu umezaliwa katika ukristo
Hata ningezaliwa uislam kwa akili yangu hii nisingeuelewa. Nimezaliwa mkristu mbona sijauelewa hadi sasa?

Hizi dini mbili ni za kipuuzi na za kibinafsi...hawajui kama kuna watu wanaoabudu mti na ni mungu wao...watamuona mshirikina.

Mungu mwenyewe haeleweki anatuchanganya tu hadi tunauana kisa imani. Kama sio upuuzi ni kitu gani hiki
 
Makubadhi ni sandal, na Kipedo huwa wanamaanisha nguo ambazo zipo chini ya goti.
Sasa hizo sendos mbona tuna vaa hadi tusio waislamu lakini when it comes to religion debate kubazi zinakuwa kama ni utambulisho wa waislamu pekee?
 
Nukuu

"Bali yapo mambo huweza kupelekwa mahakamani kama kutaka uthibitisho, ukweli, mbali na haki"

Tuende hivyo hivyo na tumuulize jaji iwapo atapokea ushahidi wa Quran ulioleta.

Jaji anaingia mahakamani.

Quran kama mshitakiwa anaanza kujenga hoja.

(AL - MAIDA - 116)
Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu(YESU)! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.


Suali; anaulizwa Mshitaki.

Ni wapi yesu kasema "Mimi Yesu, Mimi Mungu.

Jibu kwa kutumia matukio yaliyotokea

Biblia hakuna sehemu inayomtaja Mariam kama mungu, unachojaribu kukieleza Wewe na hiyo Quran yako ni kile walichonacho Wafuasi WA Kikristo na sio kilichomo kwenye Biblia.

Waliopelekwa mahakamani sio Wakristo au waislam Bali ni vitabu viwili Biblia na Quran.

Hoja ya bikra Maria kuaombewa au kufanyiwa mungu haipo kwenye Biblia yoyote Ile unayoijua. Hivyo hoja zako ni mfu hasihusiani na hoja zilizotolewa hapo juu.

Nilitegemea utapangia hoja moja baada ya nyingine katika ya zilizotolewa.
 
Allah alivyo mkubwa alijua Kuna vilaza nyoyo zao migumu Kama miamba tuwaambie hivi " nyinyi mna dini yenu na sisi tuna dini yetu wala atuwafosi tunacho abudu
 
Hata ningezaliwa uislam kwa akili yangu hii nisingeuelewa. Nimezaliwa mkristu mbona sijauelewa hadi sasa?

Hizi dini mbili ni za kipuuzi na za kibinafsi...hawajui kama kuna watu wanaoabudu mti na ni mungu wao...watamuona mshirikina.

Mungu mwenyewe haeleweki anatuchanganya tu hadi tunauana kisa imani. Kama sio upuuzi ni kitu gani hiki
Baki na Imani yako.
 
SASA BASI, kama kweli Injili ilitiwa MKONO, naomba mnijibu maswali yafuatayo.

1. Nileteeni Injili ambayo haijatiwa mkono iliyo teremshwa kabla ya Quran.

2. Nileteeni Taurat ambayo haijatiwa mkono iliyo teremshwa kabla ya Quran. Kumbuka mimi sina muda na aya za Quran kwasababu Quran sio BIBLIA - Mkusanyiko wa vitabu. Ipo wapi Taurat iliyo teremshwa kabla ya Quran na inayo thibitishwa na Injili?

3. Nileteeni Zaburi ambayo haijatiwa mkono iliyo teremshwa kabla ya Quran. Kumbuka mimi sina muda na aya za Quran kwasababu Quran sio BIBLIA - Mkusanyiko wa vitabu. Ipo wapi Zaburi iliyo teremshwa kabla ya Quran na inayo thibitishwa na Injili?
Ukisema kuteremshwa mna maana gani?
 
Kwa uelewa wako ni ngumu sana mimi kujadiliana na wewe!!!

Balanced dialogue inahitaji wahusika wawe na uelewa mpana wa jambo wanalolijadili...

Sasa wewe Qur'an unaisikia unaleta vihoja dhaifu hivyo NAKUSHAURI IKIWEZEKANA KASOME KWANZA....

Nimekuuliza jambo hapa INAKUWAJE BIBILIA INA MITUME AMBAO WANA PANDE MBILI YAANI UPANDE MOJA WEMA NA UPANDE MWINGINE WAOVU SANA LAKINI QUR'AN INAWAELEZEA WAKIWA NA TABIA NJEMA NA YA HALI YA JUU KABISA HALAFU UJE NA DAI QUR'AN IMENAKILI KWENYE BIBILIA????

Yaani source iwe shallow kuliko nakala 😂😂😂😂😂😂😂

Ndio maana nikakuambia Quran hauwezi kuwa kitabu cha Rejea, afadhali umeniongezea hoja ya Saba hapo.

Quran haiwezi kukua pande zote WA wahusika/mitume Kwa sababu muandishi wake hajawahi kuwaona wahusika wenyewe, na hajui eneo waliokuwa wanaishi kijiografia.
Kitendo cha kusema tuu mitume wa jitahidi walikuwa na upande mmoja wa wema tuu kinadhihirisha kuwa Quran haiwezi kuwa kitabu cha rejea.

Biblia ipo wazi inaelezea bila kuficha pande zote mbili za mtu. Kumbuka Binadamu sio Malaika hivyo lazima akosee.
Na makosa yake yanapimwa kwenye sheria.
Kuanzia Abrahamu mpaka mitume wote wanadhambi na Biblia imeweka hayana makosa Yao.

Sasa Quran Kwa vile anayesimulia anahadithia hadithi asizozijua ni rahisi kupuyanga
 
Umesikia au umesoma mahali iyo Allah kwa wingi? Ndio nasikia kwako .
Hii ni hatari kubwa,kitu umeandika mwenyewe na yumkini wewe ndiye unayekijua zaidi halafu tena unakikataa?

Post yako uliyoyazungumza hayo hii hapa, ikiwezekana nifundishe nielewe

 
Ndg wasikilizaji na watazamaji mpaka ktk huu mtifuano nimefanikiwa kuyaona yafuatayo;

1. Mtoa mada ameweka wazi kuwa analinganisha hivi vitabu 'kimahakama'. Nilivyoelewa mimi hapo ni 'kidunia'.......i.e kipeter kibatala au kitundu lissu au kigenerali ulimwengu. 'Udunia' na 'Uroho' kuna wakati km vinapishana hv; siajabu ndo maana mtoa mada ameona kujirudia kwa baadhi ya habari za Biblia ktk Qur'an ni upuuzi tu kwake. Xiahabu ndo maana mtoa mada ameshangaa kwanini Muhammad amehangaika kuwazungumzia watu wengine badala ya Waarab wenzake tu (wa Mekka au Madina, bila shaka).

2. Kwakuwa kichwa cha habari chake kimeidunisha Qur'an, basi wale wasioipenda na wasiowapenda wafuasi wake wameibuka kwa shangwe kwelikweli huku wakisahau kupitia kwa kina habari nzima, tena neno kwa neno, ili waone jinsi gani upande wao ulivyoelezwa kuwa sio wao.

3. Mada imesheheni tuhuma kuwa Waislamu hawawapendi/wana chuki na Wakristo, lakini ajabu wanaosema hivyo wao ndo wameshindwa hata kujuzuia na chuki zao kwa Waislamu kiasi kwamba wanaweka kabisa maandishi ya kuwaprovoke. Hiyo huju mtandaoni, ukienda nje sote tuna majibu kuwa ni maeneo ya watu wa imani gani huwa kunakuwa kumesheheni matendo ya kikatili na ddhulma zaidi......

4. Mada ni kubwa kuliko mtoa mada. Sijasoma dini, sina uzoefu wa kubishana katika dini lakini ninaona kabisa baadhi ya hoja zinashangaza kidogo.

5. ........

Tuendelee kuwasikilizia wajuzi........

Kama hujasoma dini na hujui masuala ya kisheria huwezi elewa lolote humu.

Ila mtu aliyesoma sheria hata Kama hajasoma dini hoja zilizotolewa zinaweza kumpa picha halisi ya vitabu hivyo viwili na kutoa maamuzi ya kisheria.
 
Back
Top Bottom