😀😀😀 Huu mjadala ushakuwa mzito kwako Mkuu. Nakushauri nenda Kwa mwalimu wako WA dini
Isaya 42:8
Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Msikilize Musa maana Hakuwa mjinga, anajua anaongea na Mungu lakini anamuuliza huyo Mungu jina lake,
Kutoka 3:13
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini?
Kutoka 3:14
Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.
Kutoka 3:15
Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
Mungu anaendelea huku Sura ya 6 ya kutoka
Kutoka 6:2
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
Kutoka 6:3
nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.