Kama Biblia ni kitabu cha kutungwa, nani alikitunga na chanzo na kusudio lake ni nini?

Yaan queen of Sheba hujaisoma habari zake mpaka useme habari za waafrica hazimo mbona zipo nyingi tu kwenye Biblia
Unaweza nipa habari za waafrika watanzania, wakenya, waganda, wanyarwanda, warundi, wasudani, wazambia, wasouth Afrika, wa Angola, wa Malawi, wa Nigeria n.k Kutoka kwenye Biblia...
 

Mkuu nilijibu hoja yako hii hapo nyuma kwa ujumla tu, ila naona hakuna aliyejibu maswali yako. Leo nitajitahidi kujibu maswali yako kama ifuatavyo.

Kwanza kabisa neno 'Biblia' linamaanisha mkusanyiko wa vitabu vya maandishi au historia ya kale ya wayahudi. Mkusanyiko huo, wakristo wao huutambua kama maandiko yao matakatifu.

1. Uandishi wa vitabu vya imani ya kiyahudi ulianza zamani sana. Inakadiriwa ni kuanzia karne ya 12 kabla ya kuzaliwa Kristo mpaka karne ya kwanza baada ya kuzaliwa Kristo.

Zoezi la kuanza kuvikusanya na kufanya uchambuzi kwa lengo la kuviweka pamoja ulianza rasmi mwanzoni mwa karne ya 3 mpaka 4 mwanzoni baada kufariki Kristo.

2. Watunzi walioandika vitabu vilivyomo kwenye biblia wanakadiriwa kufikia 40 kwa kipindi cha miaka 1,500.

3. Watunzi wa vitabu vilivyomo kwenye Biblia walikuwa wa mataifa mbali mbali, lugha tofauti tofauti na wenye tamaduni tofauti tofauti na katika nyakati tofauti.

4. Uamuzi wa kutunga hadithi ulikuwa ni maamuzi binafsi ya mtunzi. Uamuzi wa kuweka mkusanyiko wa hadithi hizo ulitokana na mgongano wa kiimani na kimaslahi wa Makundi ya viongozi wa imani ya wayahudi wakati huo kiasi cha kundi moja kuomba nguvu ya kisiasa kwa mfalme wa rumi kulishinda kundi shindani.

5. Kama nilivyoeleza hapo juu, uamuzi wa kutunga kitabu ulikuwa wa mtunzi mwenyewe. Hapakuwahi kuwepo kikao cha kuelekeza maudhui na majina ya vitabu.

Vipo vitabu ndani ya biblia mathalan Waebrania, Ester, Joshua, Samwel, Wafalme, Ruthi na Ayubu havijulikani mtunzi wake ni nani mpaka leo.

6. Kuanzia kitabu cha kwanza kwenye Biblia hadi cha mwisho imepita wastani wa miaka 2,000 hivi.

7. Hakuna aliyetoa majina hayo isipokuwa kikao cha mwaka 382 cha baraza la Roma chini ya papa Damascus ndicho kilichopitisha vitabu 73 viwemo ndani ya Biblia.

8. Kuna watunzi wengi na vitabu vingi zaidi ya 200 ambavyo kwa mtazamo wa kanisa la Roma la wakati huo na utawala wa Rumi enzi hizo havikukubaliana nao. Kwa hiyo vilichomwa na watunzi wengi kuuawa na kanisa la Roma, hiko ndiko kile kipindi cha giza!

Mkuu natumaini nimekujibu vizuri maswali yako. Nawasilisha.
 
Neno la Mungu ni kweli na hakika, jua ndo linaizunguka dunia na sio dunia kulizunguka jua.
 
Neno la Mungu ni kweli na hakika, jua ndo linaizunguka dunia na sio dunia kulizunguka jua.
Mkuu sehemu ya kwanza ya sentence yako hapo juu inaweza kuwa kweli kwa imani na mtazamo wako ila sehemu ya pili sio kweli.

Ndugu, ukweli usio na shaka ni kwamba dunia ndio inayolizunguka jua. Usidanganye watu!
 
Hakuna kitabu Cha mungu kinachoitwa biblia vitabu vinavo julikana ni 4 na vilishushwa Kwa kila zama
1.Zaburi
2.Torati
3.Injili
4.Quran
Endeleeni kufata wazungu na warabu mkija kujua ukweli wa dunia inavoeenda mmechelewa
KAMA HAKUNA KITABU CHA MUNGU ULIJUAJE KAMA HIVYI VINNE VIMESHUSHWA??
 
Unaweza nipa habari za waafrika watanzania, wakenya, waganda, wanyarwanda, warundi, wasudani, wazambia, wasouth Afrika, wa Angola, wa Malawi, wa Nigeria n.k Kutoka kwenye Biblia...
Kama mwaka 1960 watanzania wote walikuwa ni milion 12. Unategemea miaka ya Biblia walikuwa wangapi kama sio hili eneo lilikuwa pori tupu. Tutajuaje kama hawa wakenya wasudan Wacongo sio waafrica waliotokea sudani misri Ethiopia Libya nk. Ambao kimsingi wameandikwa kwenye Biblia. Na hilo eneo lilikuwa la blacks kabla mwarabu kutushinda na kulichukua.
 
Nilikitunga mimi
 

Kila mtu alitunga biblia yake

Your browser is not able to display this video.
 
Hakuna mtu anaweza kutunga biblia Kwa jinsi ilivyoandikwa vile ,nasema Tena hakuna mwenye hiyo IQ

Even Sir Isack Newton mwenyewe aliichambua biblia hasa kitabu cha Daniel ,kuliko hata Calculus na huyo alikuwa na IQ nyingi
 
Kakuambia huwezi kutunga hicho kitabu, Kama unambishia basi nenda kakitunge na sisi tukisome labda kitatuvutia cha kwako!

unadhani mambo ni rahisi hivyo?
Isack Newton mwenye IQ kubwa ,moja ya watu waliotokea duniani ,alikisoma kitabu cha Daniel akakichambua ,jinsi kilivyoandika habari za mbeleni ,
 
Hakuna mtu anaweza kutunga biblia Kwa jinsi ilivyoandikwa vile ,nasema Tena hakuna mwenye hiyo IQ
Nimependa ulivoandika kuwa "hakuna mwenye hiyo IQ" Nimewaza Sana. Kuwa Kwa kweli kama imetungwa basi walioitunga watakuwa na IQ kubwa Sana na kipimo chake nadhani kitakuwa siyo hiki tunachopimiwa sisi.
 
Unaweza nipa habari za waafrika watanzania, wakenya, waganda, wanyarwanda, warundi, wasudani, wazambia, wasouth Afrika, wa Angola, wa Malawi, wa Nigeria n.k Kutoka kwenye Biblia...
Taifa la Tanzania limepata kuwepo tangu mwaka gani?
 
JE UNAIJUA BIBLIA YAKO KIASI GANI??

Kitabu / Waandishi
1) Mwanzo: Musa
2) Kutoka: Musa
3) Mambo ya Walawi: Musa
4) Hesabu: Musa
5) Kumbukumbu la Torati: Musa
6) Yoshua: Yoshua
7) Waamuzi: Samweli
8) Ruthu: Samweli
9) 1 Samweli: Samweli; Gadi; Nathan
10) 2 Samweli: Gadi; Nathan
11) 1 Wafalme: Yeremia
12) 2 Wafalme: Yeremia
13) 1 Mambo ya Nyakati: Ezra
14) 2 Mambo ya Nyakati: Ezra
15) Ezra: Ezra
16) Nehemia: Nehemia
17) Esta: Mordekai
18) Ayubu: Musa
19) Zaburi: Daudi na wengine
20) Mithali: Sulemani; Aguri; Lemueli
21) Mhubiri: Sulemani
22) Nyimbo za Sulemani: Sulemani
23) Isaya: Isaya
24) Yeremia: Yeremia
25) Maombolezo: Yeremia
26) Ezekieli: Ezekieli
27) Danieli: Danieli
28) Hosea: Hosea
29) Yoeli: Yoeli
30) Amosi: Amosi
31) Obadia: Obadia
32) Yona: Yona
33) Mika: Mika
34) Nahumu: Nahumu
35) Habakuki: Habakuki
36) Sefania: Sefania
37) Hagai: Hagai
38) Zekaria: Zekaria
39) Malaki: Malaki
40) Mathayo: Mathayo
41) Marko: Marko
42) Luka: Luka
43) Yohana: Mtume Yohana
44) Matendo: Luka
45) Warumi: Paulo
46) 1 Wakorintho: Paulo
47) 2 Wakorintho: Paulo
48) Wagalatia: Paulo
49) Waefeso: Paulo
50) Wafilipi: Paulo
51) Wakolosai: Paulo
52) 1 Wathesalonike: Paulo
53) 2 Wathesalonike: Paulo
54) 1 Timotheo: Paulo
55) 2 Timotheo: Paulo
56) Tito: Paulo
57) Filemoni: Paulo
58) Waebrania: Haijulikani
59) Yakobo: Yakobo (ndugu Ya Yesu)
60) 1 Petro: Petro
61) 2 Petro: Petro
62) 1 Yohana: Mtume Yohana
63) 2 Yohana: Mtume Yohana
64) 3 Yohana: Mtume Yohana
65) Yuda: Yuda (ndugu Ya Yesu)
66) Ufunuo: Mtume Yohana

TAKWIMU ZA BIBLIA

Ukweli wa Kushangaza wa Biblia na Takwimu
๐Ÿผ Idadi ya Vitabu katika Biblia: 66
๐Ÿผ Sura: 1,189
๐Ÿผ Aya: 31,101
๐Ÿผ Maneno: 783,137
๐Ÿผ Herufi: 3,566,480
๐Ÿผ Idadi ya Ahadi zilizotolewa katika Biblia: 1,260
๐Ÿผ Amri: 6,468
๐Ÿผ Utabiri: zaidi ya 8,000
๐Ÿผ Unabii Uliotimia: Aya 3,268
๐Ÿผ Unabii Usiotimia: 3,140
๐Ÿผ Idadi ya Maswali: 3,294
๐ŸผJina refu zaidi: Mahershalalhashbaz (Isaya 8:1)
๐Ÿผ Mstari mrefu zaidi: Esta 8:9 (maneno 78)
๐Ÿผ Mstari mfupi zaidi: Yohana 11:35 (maneno 2: "Yesu alilia" .
๐Ÿผ Vitabu vya Kati: Mika na Nahumu
๐Ÿผ Sura ya Kati: Zaburi 117
๐Ÿผ Sura Fupi (kwa idadi ya maneno): Zaburi 117 (kwa idadi ya maneno)
๐Ÿผ Kitabu kirefu zaidi: Zaburi (Sura 150)
๐Ÿผ Kitabu kifupi zaidi (kwa idadi ya maneno): 3 Yohana
๐Ÿผ Sura ndefu zaidi: Zaburi 119 (aya 176)
๐Ÿผ Idadi Ya Neno "Mungu" linatokea mara: 3,358
๐Ÿผ Idadi ya neno "Bwana" linatokea mara: 7,736
๐Ÿผ Idadi ya waandishi tofauti: 40
๐Ÿผ Idadi ya lugha ambazo Biblia imetafsiriwa katika: zaidi ya 1,200

TAKWIMU ZA AGANO LA KALE:
------------------------------------------
๐Ÿผ Idadi ya Vitabu: 39
๐Ÿผ Sura: 929
๐Ÿผ Aya: 23,114
๐Ÿผ Maneno: 602,585
๐Ÿผ Herufi: 2,278,100
๐Ÿผ Kitabu cha Kati: Mithali
๐Ÿผ Sura ya Kati: Ayubu 20
๐Ÿผ Mistari ya Kati: 2 Mambo ya Nyakati 20:17,18
๐Ÿผ Kitabu Kidogo kabisa: Obadia
๐Ÿผ Mstari mfupi zaidi: 1 Mambo ya Nyakati 1:25
๐Ÿผ Mstari mrefu zaidi: Esta 8:9 (maneno 78)
๐Ÿผ Sura ndefu zaidi: Zaburi 119

TAKWIMU ZA AGANO JIPYA:
=======================
๐Ÿผ Idadi ya Vitabu: 27
๐Ÿผ Idadi ya Sura: 260
๐Ÿผ Idadi ya Aya: 7,957
๐Ÿผ Maneno: 180,552
๐Ÿผ Herufi: 838,380
๐Ÿผ Kitabu cha Kati: 2 Wathesalonike
๐Ÿผ Sura za Kati: Warumi 8, 9
๐Ÿผ Mstari wa Kati: Matendo 27:17
๐Ÿผ Kitabu Kidogo Zaidi: 3 Yohana
๐Ÿผ Mstari mfupi zaidi: Yohana 11:35
๐Ÿผ Mstari mrefu zaidi: Ufunuo 20:4 (maneno 68)
๐ŸผSura ndefu zaidi: Luka 1
*****************************

Kuna maneno 8,674 tofauti ya Kiebrania katika Biblia, 5,624 tofauti
Maneno ya Kigiriki, na maneno 12,143 tofauti ya Kiingereza katika King James Version.

*****************************
โ€ข Biblia Imeandikwa na Takriban Waandishi 40
โ€ข Imeandikwa kwa kipindi cha miaka 1,600
โ€ข Imeandikwa zaidi ya vizazi 40
โ€ข Imeandikwa katika lugha tatu: Kiebrania, Kigiriki na Kiaramu
โ€ข Imeandikwa katika mabara matatu: Ulaya, Asia na Afrika
โ€ข Imeandikwa katika maeneo tofauti: nyikani, shimoni, ikulu, gereza, uhamishoni, nyumbani.
โ€ข Imeandikwa na wanadamu kutoka kazi zote: wafalme, wakulima, madaktari, wavuvi, watoza ushuru, wasomi, nk.
โ€ข Imeandikwa katika nyakati tofauti: vita, amani, umaskini, ustawi, uhuru na utumwa
โ€ข Imeandikwa katika hali tofauti: urefu wa furaha hadi kina cha kukata tamaa
โ€ข Imeandikwa kwa makubaliano ya upatanifu juu ya anuwai ya mada na mafundisho anuwai.

****************************

Vitabu 10 virefu zaidi katika Biblia

1) Zaburi - Sura 150, mistari 2,461, maneno 43,743
2) Yeremia - sura 52, mistari 1,364, maneno 42,659.
3) Ezekieli - sura 48, mistari 1,273, maneno 39,407
4) Mwanzo - sura 50, mistari 1,533, maneno 38,267.
5) Isaya - sura 66, mistari 1,292, maneno 37,044.
6) Hesabu - sura 36, mistari 1,288, maneno 32,902
7) Kutoka - sura 40, mistari 1,213, maneno 32.602
8) Kumbukumbu la Torati - sura 34, mistari 959, maneno 28,461.
9) 2 Mambo ya Nyakati - sura 36, mistari 822, maneno 26,074
10) Luka - sura 24, mistari 1,151, maneno 25,944.

****************************
Vitabu 10 vifupi zaidi katika Biblia
1) 3 Yohana - sura ya 1, mistari 14, maneno 299
2) 2 Yohana - sura ya 1, mistari 13, maneno 303
3)
 
Mkusanyiko wa vitabu au siyo?

Nani aliviita "biblia" kwa mara ya kwanza? Kwanini isiwe babcheka?
Ungejiuliza kwanza kwa nini Allah huwa anasema "enyi watu wa KITABU " nadhani usingeendelea kusumbua watu humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ