Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

..Njia unayopendekeza wewe ni ngumu.

..Cdm wamerahisisha kazi ya kuwaondoa kina Halima bungeni kwa kuwafukuza uanachama.
 
Kama hivyo ndivyo, basi CDM hawana sababu ya kuhangaika na Mdee na wenzake. Kwanini wanapoteza muda kupeleka barua NEC na kwa Speaker huku wakijua hata wakitafuta relief mahakamani hawataipata?

..aliyefikisha suala hili mahakamani ni Halima na wenzake sio Cdm.
 
Sawa, lakini si unaona CDM wanavyohangaika kupeleka barua NEC na kwa Speaker? To what end are they doing that?

..sasa si wamepata ahueni huko mahakamani?

..kwanini wasi-take advantage kwa ahueni waliyoipata wakati mahakama zimekuwa zikiwakandamiza ktk mashauri mengi?
 
..sasa si wamepata ahueni huko mahakamani?

..kwanini wasi-take advantage kwa ahueni waliyoipata wakati mahakama zimekuwa zikiwakandamiza ktk mashauri mengi?

Swala la msingi ni kwamba hawana imani na hizi institutions. Kwa hiyo, kufanya jambo ambalo wana prior knowledge kwamba halitaleta tofauti ni kupoteza muda!
 
..Njia unayopendekeza wewe ni ngumu.

..Cdm wamerahisisha kazi ya kuwaondoa kina Halima bungeni kwa kuwafukuza uanachama.

Urahisi wa hiyo njia uko wapi? Ni zaidi ya mwaka sasa tangu CC ya CDM ilipoamua kuwavua unachama, lakini bado wako mjengoni.
 
Unajua, na kila mtu anajua, kwamba JPM hatunaye tangu March 2021. Hiyo NEC bado inamuogopa JPM kusema kwamba haijui chochote kuhusu uteuzi wa Mdee na wenzake?

Kwa taarifa yako, serikali hii imepatikana kwa ulevi wa madaraka wa Magu. Usitegemee serikali hiyohiyo itajitokeza hapo hapo na kuondoa uchafu ule. Hii mbegu aliyopandikiza ya kutoheshimu sheria itachukua muda mrefu kuondoka.
 
Kama hivyo ndivyo, basi CDM hawana sababu ya kuhangaika na Mdee na wenzake. Kwanini wanapoteza muda kupeleka barua NEC na kwa Speaker huku wakijua hata wakitafuta relief mahakamani hawataipata?

CDM sio waliofungua kesi huko mahakamani, wanakwenda mahakamani kuzuia akina Mdee kulazimisha kuwa wao ni wabunge wa cdm.
 
CDM sio waliofungua kesi huko mahakamani, wanakwenda mahakamani kuzuia akina Mdee kulazimisha kuwa wao ni wabunge wa cdm.

Watawazuiaje iwapo tayari wanajua hiyo mahakama haitatenda haki?
 
Ni wajibu wao CDM kulinda chama chao kisitumike na watu wasio na uhalali huo. Hao NEC, bunge na wabunge wao waendelee na interest zao, lakini CDM isitumike kusafisha uhuni.

Watalindaje iwapo wanaamini taasisi zinazopaswa kuwapa huo ulinzi hazitafanya hivyo?
 
Kesi ya Jinai malalamikaji ni Serikali Chadema wanatakuwa kuwa mashahidi tu
 
Urahisi wa hiyo njia uko wapi? Ni zaidi ya mwaka sasa tangu CC ya CDM ilipoamua kuwavua unachama, lakini bado wako mjengoni.

..Cc ya Cdm inaaminika zaidi kufanya uamuzi unaoendana na mitizamo ya chama kuliko mahakama zetu ambazo ziko controlled na Ccm.
 
Wanakwenda kuweka rekodi sawa kuwa hao sio wabunge wao bila kujali mahakama itaamua nini.

Kuweka record sawa ni kufanikiwa kuifanya mahakama itamke hivyo. Tofauti na hivyo, kama ni kusema hao sio wabunge wao, wameshasema kwa zaidi ya mwaka sasa!
 
Kuweka record sawa ni kufanikiwa kuifanya mahakama itamke hivyo. Tofauti na hivyo, kama ni kusema hao sio wabunge wao, wameshasema kwa zaidi ya mwaka sasa!

CDM hawaipangii mahakama iamue vipi maana maamuzi ya mahakama hayaagizwi na CDM. Wao CDM wanasimamia wanachokiamini sio kinachoaminiwa na mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…