Kama chanzo cha uhai kinaweza kubadilika basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti hadi sasa. Je, ni upi msingi wa uhai?

Uko sahihi mkuu
 
Sijasema muda haupo, nimesema muda si kitu cha msingi, si kitu fundamental, ni derivative, ni kitu kinachotokana na kitu kingine.

Muda ni kama kivuli ambacho hakiwezi kimuwepo bila ya kuwepo mwanga na kitu cha kuukinga huo mwanga.

Na kitu kisipokuwa fundamental, kikiwa derivative tu, inakuwa si lazima kiwepo.

Kama wewe ni lazima uzaliwe na mama yako ili uwepo, mama yako asipokuwepo hivyo na wewe huwezi kuwepo.

Ndiyo maana unaweza kuwa na mwanga ukakosa kitu cha kuukinga huo mwanga usiwe na kivuli.

Unapoongelea chanzo, kwa maana halisi, unaongelea kitu absolute, kitu fundamental.

Sasa utakuwaje na chanzo absolute na fundamental, ambacho kinategemea muda, kinategemea cause and effect, ambayo inakuwepo kutokana na muda, wakati muda wenyewe si absolute ni relative?

Unawezaje kushona nguo ya bluu wakati kitambaa chako cha kushonea nguo ni chekundu na hakibadiliki rangi?
 
Kwa nini unadhani kila kitu lazima kiwe na msingi?

Kwa nini unadhani uhai una msingi?

Kwa nini hudhani kwamba uhai unaweza kuwepo bila msingi?

Kama uhai lazima uwe na msingi, Je msingi wa "msingi wa uhai" ni nini?
Sidhani kama lazima Kila kitu kiwe na msingi ila nadhani ya kwamba Kila chenye chanzo lazima kiwe na msingi.

Ndio maana hoja ya andiko imejengwa juu ya neno "Mungu ni chanzo cha uhai", na ndio nikaanzia hapo kuelezea.

Na kutokana na hilo na kwakuzingatia muktadha huo pia inamaana kama chanzo cha uhai ni Mungu basi uhai utakua uko na msingi wake ambao Mimi na wewe bado hatujaujua.

Na msingi ni mwanzo wa chanzo.

Lete maneno mkuu...
 
Hebu fikiria mambo ambayo watu wanayafanyanya hapa duniani
haya mambo ya Sayansi ,katika nyanja mbalimbali
Mambo makubwa ya kushangaza
na kila mvumbuzi anashangazwa na uvumbuzi wa mwingine
kwa hiyo kumbe watu wanavumbua vitu villivyo fichika,wapi kwenye fiikra

na fikra hazionekani kwa macho haya ya damu na nyama
kwa hiyo lazima kuna chanzo ambako watu wanatoa haya mambo

huko kwenye nguvu ya asili,ulimwengu wa roho(fikra) au ufahamu unaoishi
 
Kama msingi ndio huunda vyanzo mbalimbali, Je msingi unaanza tu from nowhere?
Hili swali unaweza kujijibu labda kwa kuanza Kutafakari na kujiuliza maswali ya hapa na pale kwa mfano msingi wa nyumba unayokaa msingi wake ni nini?😅😅😅.

Ajali ambayo ilitokea na kuua watu ni msingi na hutengeza vyanzo mbalimbali vya habari, je, msingi wa ajali hiyo ni nini?😅😅😅

Wacha kwanza tutrace back kutoka kwenye chanzo hadi kwenye msingi halafu tukifika hapo kwenye msingi tutarudi tena ubaoni tuone kama msingi unaweza kuwa na msingi
 
Sidhani kama lazima Kila kitu kiwe na msingi ila nadhani ya kwamba Kila chenye chanzo lazima kiwe na msingi.
Kama si lazima kila kitu kiwe na msingi, Basi uhai na wenyewe hauna msingi.
Ndio maana hoja ya andiko imejengwa juu ya neno "Mungu ni chanzo cha uhai", na ndio nikaanzia hapo kuelezea.
Kwanza Mungu hayupo.

Na kama Mungu hayupo, Basi uhai chanzo chake sio Mungu.
Na kutokana na hilo na kwakuzingatia muktadha huo pia inamaana kama chanzo cha uhai ni Mungu basi uhai utakua uko na msingi wake ambao Mimi na wewe bado hatujaujua.
Chanzo cha uhai sio Mungu.

Chanzo cha uhai ni viumbe hai.

Pasipo viumbe hai hakuna uhai.
Na msingi ni mwanzo wa chanzo.
Kama msingi ni mwanzo wa chanzo, Je huo msingi ulitokea tu wenyewe?
Lete maneno mkuu...
 
Intelligent how ? Ninavyoongelea Nishati ninamaanisha ni kama wewe unavyojaza mafuta kwenye gari lako mafuta ndio baada ya ile spark kubadilisha form na kuwa gasi ni Nguvu kubwa sana inatokea ili iweze kuendesha Piston..., sasa tukija kwenye information ukienda at a deeper level wala sio ngumu ni kama unatoa photocopy ukichukua nakala moja unazalisha nyingine kama ulikuwa unakula mihogo kwa bahati mbaya ukachafua lile karatasi basi huenda kuanzia muda huo kukawa na nakala zenye alama ya dole gumba lako....
Ila si unajua kwamba Dunia nzima tunaweza kukubaliana kwamba jambo fulani ni fact lakini kumbe kiuhalisia wote tupo wrong?
Kukubaliana wote huenda ikawa ngumu na hata tukikubaliana haimaanishi the underlying truth inabadilika (Argumentum Ad Populum) ; Na hapo ndio Sayansi comes into it's own hata wewe mmoja leo ukija na ukatwambia kwamba tulikuwa tumekosea sababu ya A, B, C basi wote tutakuunga mkono; Tufauti na Imani itabadilisha premise nzima na kukwambia kwamba you were right all along ni basi tu ulishindwa kuelewa maelezo yako mwenyewe...
Yaani kimsingi ni kwamba baada ya kudadisi tunafikia hitimisho at a certain point in time na kuona kwamba tumefikia ukweli even though hicho tunachoita ukweli sio ukweli halisia!
It a journey and we seeker of knowledge hatufiki bali tunaendelea na mpaka sasa tuna known knowns, known unknowns na unknown unknowns... And the journey continues until the day we stop breathing ambapo watakuja wengine watakaoona further sababu ya kusimama kwenye Shoulders za Giants of the Past....
 
Hili swali unaweza kujijibu labda kwa kuanza Kutafakari na kujiuliza maswali ya hapa na pale kwa mfano msingi wa nyumba unayokaa msingi wake ni nini?😅😅😅.
Msingi wake ni ardhi ambapo nyumba imejengwa juu yake.

Bila ardhi huwezi kujenga nyumba.
Ajali ambayo ilitokea na kuua watu ni msingi na hutengeza vyanzo mbalimbali vya habari, je, msingi wa ajali hiyo ni nini?😅😅😅
Kwanza hakuna msingi wa ajali.

Kuna vyanzo mbalimbali vinavyoweza kusababisha ajali.

Hakuna msingi wa ajali.

Ndio maana nilikuuliza mwanzoni, Je unadhani kila kitu lazima kiwe na msingi?

Ukajibu "Sidhani".

Hivyo uhai hauna msingi.

Pia ajali haina msingi.
Wacha kwanza tutrace back kutoka kwenye chanzo hadi kwenye msingi halafu tukifika hapo kwenye msingi tutarudi tena ubaoni tuone kama msingi unaweza kuwa na msingi
Hakuna msingi wa kila kitu.

Kuna vyanzo mbalimbali vya kitu.

Una elewa hilo?
 
Mungu ni mwanzo na mwisho sio Chanzo Halisi.

Kuna tofauti kubwa kati ya mwanzo na Chanzo au kwa kingereza genesis na Source.Unaposema Mungu unamaanisha mwanzo na mwisho au alfa na omega.

But unaposema Chanzo unamaanisha umilele (eternity) hana mwanzo wala mwisho.
 
Ni kweli ya kwamba muda kulingana na fizikia, si kitu fundamental bali ni derivative kwa maana unatokana na mwingiliano wa mwanga, nafasi, na blah blah nyingine, lakini mkuu hii haiwezi kupingana na hoja ya kwamba si kila kitu kinachotokana na kitu kingine basi lazima kiwe cha kipuuzi au hakina umuhimu kabisa.

Kwa mfano hapo umesema kivuli hakiwezi kuwepo bila mwanga na kitu cha kuukinga mwanga, lakini je, hiyo inamaanisha kivuli hakina maana?

Kwasababu hatuwezi kupima mwanga bila kuwepo kivuli kwenye baadhi ya hali na ili uweze kuthibitisha hili basi unaweza kurejea ile dhana ya event horizon kwenye black holes.

Kwahiyo inawezekana ni kweli muda si fundamental, lakini kama unaleta uhalisia wa vitu vinavyotokea, sasa kwanini tusiuweke kuwa sehemu ya dhana ya chanzo?.

Kwa maana nadhani Dunia iko na dhana nyingi zisizo fundamental na zinaathiri ulimwengu kwa namna ambayo inafanya ziwe (ingawa naweza kukosa mifano yake kwa sasa ila kama tukishirikiana Mimi na wewe tunaweza kukubalina juu ya hili).

Kwahiyo basi katika hoja yako ya kusema chanzo kwa maana halisi ni kitu absolute na fundamental, kwa maana ya kwamba huwezi kuwa na chanzo kinachotegemea muda kwa sababu muda si absolute.

Nami naomba nikuulize swali hapo hapo, Je, kila chanzo lazima kiwe absolute?(Na kama ndivyo basi naomba unieleweshe kwa kina hapa).

Kwasababu ukiangalia sana hoja yako mkuu, imebezi kwenye absolute truth kuliko relative, na kama huko ndiko ulikojikita basi hapa duniani yapaswa kila kitu kingine kinachotegemea chanzo cha kitu fulani kiwe derivative ya kitu hiko, lakini sasa katika mfumo wa maisha ya kawaida na hata kwenye sayansi nadhani, kikawaida huwa tunaweza kuwa na vyanzo vya mlinganisho kwa maana ya relative sources, ambavyo huwa vina maana ndani ya muktadha fulani (hii nayo unaizungumziaje mkuu).

Lakini pia niseme tu, ya kwamba nimeupenda mfano wako wa kushona nguo ya bluu kwa kutumia kitambaa chekundu, lakini vipi kama tunaweza kupaka kitambaa hicho rangi ya bluu? 😅😅

Mimi sio mtaalam sana wa mambo ya quantum (ila kuanzia sasa nitajikita zaidi huko kwa maana inawezekana baadhi ya puzzle zinasolvika kirahisi huko), ila naelewa jambo moja ya kwamba katika ulimwengu wa quantum, kuna mifano mingi inayoelezea kitu kuweza kuwa na hali mbili tofauti kwa wakati mmoja.

Kwa hiyo, kutokana na hilo basi swali lako liko na dhana ya ukweli wa moja kwa moja, iilhali ukweli mara nyingi huwa ni wa mlinganisho kulingana na muktadha.
 
Chanzo cha uhai ni viumbe hai.
Nadhani hapa umeleta kitu kingine tena, na hii ni puzzle pia, na kama usemavyo ni kweli ya kwamba chanzo cha uhai ni viumbe hai basi bado msingi wa uhai haujulikani.
 
Najua kuna utofauti kati ya chanzo na mwanzo lakini pia unaposema ninaposema chanzo inamaanisha kutokua na mwanzo wala mwisho hii inamaanisha ni infinity loop na ndio kitu ambacho kimefanya nilete hili andiko kwa maana nyingine si kwamba msingi wake haupo ila ni loop yenye mlolongo mrefu hadi kufikia msingi wake.
 
Again, sijasema muda hauna maana, nimesema muda si fundamental, si kitu cha msingi.

Na unapoongelea chanzo, kitu ambacho ni fundamental, hutakiwi kuongelea kitu kinachotegemea kitu derivative, unatakiwa kuongelea kitu fundamental, si kitu derivative.
 
Nadhani hapa umeleta kitu kingine tena, na hii ni puzzle pia, na kama usemavyo ni kweli ya kwamba chanzo cha uhai ni viumbe hai basi bado msingi wa uhai haujulikani.
Si lazima kila kitu kilichopo kiwe na msingi wake.

Kama uhai lazima uwe na msingi wake, Hata huo msingi wa uhai, lazima uwe na msingi wake mwingine.

Msingi huo wa uhai, Hauwezi kuwepo tu bila msingi wowote.
 
Namimi nimekubaliana na wewe lakini pia nimekupa sababu za kwamba kutokua kitu cha msingi haimaanishi hakipaswi kutumika katika muktadha huo.
 
Si lazima kila kitu kilichopo kiwe na msingi wake.

Kama uhai lazima uwe na msingi wake, Hata huo msingi wa uhai, lazima uwe na msingi wake mwingine.

Msingi huo wa uhai, Hauwezi kuwepo tu bila msingi wowote.
Ndio maana nikakwambia kwanza tuanzie hapo turudi nyuma hadi kufikia msingi halafu tutaanzia hapo kujadili tena kama msingi ni lazima uwe na msingi.

Kwahiyo hoja yako ya msingi kuweza kuwa na msingi hakuwezi kuondoa hoja ya chanzo kuwa na msingi, kwahiyo kabla hatujarudi hapo kwenye msingi kuwa na msingi kwanza tujadili msingi wa uhai ni nini.
 
Namimi nimekubaliana na wewe lakini pia nimekupa sababu za kwamba kutokua kitu cha msingi haimaanishi hakipaswi kutumika katika muktadha huo.
"Muktadha huo" ni muktadha gani?

Hutakiwi kuongelea kitu cha msingi kama chanzo kwa kutumia kitu derivative.

Habari ya chanzo si habari fundamental, inaweza kuwa na maana katika muktadha fulani tu.

Kwa hivyo, unapoongelea chanzo, ni lazima uweke muktadha.
 
Kwa nini ujadili msingi wa uhai ni nini, wakati hujui msingi wa msingi wa uhai ni nini?

Kwa sababu kuna vitu vipo lakini havina msingi.

Hata uhai na wenyewe hauna msingi.

Kuwa na chanzo si lazima kuwe na msingi.

Chanzo kinaweza kuwepo bila msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…