Sijasema muda haupo, nimesema muda si kitu cha msingi, si kitu fundamental, ni derivative, ni kitu kinachotokana na kitu kingine.
Muda ni kama kivuli ambacho hakiwezi kimuwepo bila ya kuwepo mwanga na kitu cha kuukinga huo mwanga.
Na kitu kisipokuwa fundamental, kikiwa derivative tu, inakuwa si lazima kiwepo.
Kama wewe ni lazima uzaliwe na mama yako ili uwepo, mama yako asipokuwepo hivyo na wewe huwezi kuwepo.
Ndiyo maana unaweza kuwa na mwanga ukakosa kitu cha kuukinga huo mwanga usiwe na kivuli.
Unapoongelea chanzo, kwa maana halisi, unaongelea kitu absolute, kitu fundamental.
Sasa utakuwaje na chanzo absolute na fundamental, ambacho kinategemea muda, kinategemea cause and effect, ambayo inakuwepo kutokana na muda, wakati muda wenyewe si absolute ni relative?
Unawezaje kushona nguo ya bluu wakati kitambaa chako cha kushonea nguo ni chekundu na hakibadiliki rangi?
Ni kweli ya kwamba muda kulingana na fizikia, si kitu fundamental bali ni derivative kwa maana unatokana na mwingiliano wa mwanga, nafasi, na blah blah nyingine, lakini mkuu hii haiwezi kupingana na hoja ya kwamba si kila kitu kinachotokana na kitu kingine basi lazima kiwe cha kipuuzi au hakina umuhimu kabisa.
Kwa mfano hapo umesema kivuli hakiwezi kuwepo bila mwanga na kitu cha kuukinga mwanga, lakini je, hiyo inamaanisha kivuli hakina maana?
Kwasababu hatuwezi kupima mwanga bila kuwepo kivuli kwenye baadhi ya hali na ili uweze kuthibitisha hili basi unaweza kurejea ile dhana ya event horizon kwenye black holes.
Kwahiyo inawezekana ni kweli muda si fundamental, lakini kama unaleta uhalisia wa vitu vinavyotokea, sasa kwanini tusiuweke kuwa sehemu ya dhana ya chanzo?.
Kwa maana nadhani Dunia iko na dhana nyingi zisizo fundamental na zinaathiri ulimwengu kwa namna ambayo inafanya ziwe (ingawa naweza kukosa mifano yake kwa sasa ila kama tukishirikiana Mimi na wewe tunaweza kukubalina juu ya hili).
Kwahiyo basi katika hoja yako ya kusema chanzo kwa maana halisi ni kitu absolute na fundamental, kwa maana ya kwamba huwezi kuwa na chanzo kinachotegemea muda kwa sababu muda si absolute.
Nami naomba nikuulize swali hapo hapo, Je, kila chanzo lazima kiwe absolute?(Na kama ndivyo basi naomba unieleweshe kwa kina hapa).
Kwasababu ukiangalia sana hoja yako mkuu, imebezi kwenye absolute truth kuliko relative, na kama huko ndiko ulikojikita basi hapa duniani yapaswa kila kitu kingine kinachotegemea chanzo cha kitu fulani kiwe derivative ya kitu hiko, lakini sasa katika mfumo wa maisha ya kawaida na hata kwenye sayansi nadhani, kikawaida huwa tunaweza kuwa na vyanzo vya mlinganisho kwa maana ya relative sources, ambavyo huwa vina maana ndani ya muktadha fulani (hii nayo unaizungumziaje mkuu).
Lakini pia niseme tu, ya kwamba nimeupenda mfano wako wa kushona nguo ya bluu kwa kutumia kitambaa chekundu, lakini vipi kama tunaweza kupaka kitambaa hicho rangi ya bluu? 😅😅
Mimi sio mtaalam sana wa mambo ya quantum (ila kuanzia sasa nitajikita zaidi huko kwa maana inawezekana baadhi ya puzzle zinasolvika kirahisi huko), ila naelewa jambo moja ya kwamba katika ulimwengu wa quantum, kuna mifano mingi inayoelezea kitu kuweza kuwa na hali mbili tofauti kwa wakati mmoja.
Kwa hiyo, kutokana na hilo basi swali lako liko na dhana ya ukweli wa moja kwa moja, iilhali ukweli mara nyingi huwa ni wa mlinganisho kulingana na muktadha.